Saturday, 19 July 2014

FAIDA ZA KIAFYA ZA MTI WA MWEMBE


Mti wa mwembe mbali ya kuzaa tunda la embe ambalo hutumika kama chakula au kinywaji ( juisi ) chenye ladha ninayo vutia, una faida lukuki za kiafya kwa mwili wa mwanadamu.
Zifuatazo ni baadhi ya faida za kiafya za mti wa mwembe.


1. MAJANI YA MTI WA MWEMBE :
Majani machanga ya mti wa mwembe yakichemshwa huwa na faida zifuatazo ;
i. Hutibu pumu
ii. Hutibu kifua kikavu
iii. Hutumika katika kuoshea vidonda vitokanavyo na majeraha mbalimbali ( Majani ya maembe yamethibitika kuwa na uwezo mkubwa wa kukausha majeraha ya vidonda )
iv. Unga wa majani ya mwembe hutumika katika kutunza meno ambapo mtu mwenye matatizo ya meno atatakiwa kusukutua kwa kutumia unga unaotokana na majani ya mwembe.

2. KOKWA LA EMBE
Unga unaotokana na kokwa la embe husaidia kuzuia kuharisha na kuhara damu.





3. T UNDA LA EMBE
i. Ulaji wa tunda la embe husaidia kutibu minyoo na kuzuia uvujaji wa damu ovyo.
ii. Tunda la embe lina vitamin C na hivyo ulaji wake husaidia kuponesha vidonda kwa haraka, hivyo basi mlaji sana wa tunda la embe endapo atapata vidonda basi atapona kwa haraka sana kuliko mtu asiye tumia tunda hili mara kwa mara.
iii. Huwasaidia watu wenye matatizo ya kutokupata choo.
iv. Utumiaji wa maembe mabichi husaidia kuondoa mawe kwenye figo na hivyo kuepuka kufanyiwa upasuaji.
v. Embe bichi likichanganywa na chumvi na sukari na kasha kuchemshwa ni tiba ya tatizo la mapigo ya moyo kwenda kwa haraka.

MAGOME YA MWEMBE
Magome ya mti wa mwembe yakichemshwa ni dawa nzuri ya homa.

JUISI YA EMBE :
Juisi ya embe ikichanganywa na maziwa fresh husaidia kurejesha afya ya ,tu aliye dhoofika.
Vile vile kunusa juisi ya embe kunasaidia kuzuia tatizo la kutoka damu puani. Hivyo basi juisi ya embe inaweza kutumika kama huduma ya kwanza kwa mtu anaye tokwa na damu puani.

0 comments:

Post a Comment