Saturday 7 June 2014

MIMBA KUCHOROPOKA (MISCARRIAGE)






Tatizo la mimba kuharibika na kutoka (kuchoropoka) kabla ya umri wake unaotakiwa kukamilika, limekuwa likiwasumbua wanawake wengi. Kutokana na maombi ya wasomaji wetu, tutalijadili kwa kina tatizo hili ambalo kitaalamu huitwa Miscarriage.


MISCARRIAGE NI NINI?


Kwa kawaida, ili mtoto azaliwe, ni lazima mwanamke afanye tendo la ndoa akiwa katika siku zake za kupata ujauzito ambapo mimba hutungwa. Baada ya mimba kutungwa, mtoto hukaa tumboni kwa muda wa miezi tisa ambapo hupitia hatua mbalimbali za mabadiliko hadi kuwa binadamu aliyekamilika.


Inapotokea kuwa kitoto kimetoka tumboni kwa namna yoyote ile, kikiwa na umri wa chini ya miezi mitano (wiki ishirini), tatizo hilo huitwa Miscarriage.


Katika hali hii, kitoto kinakuwa hakijakamilika na hakiwezi kujitegemea chenyewe kwa mahitaji muhimu kama kupumua, jambo ambalo husababisha kifo.


NB: Mtoto akitoka akiwa ameshapita umri wa miezi mitano, tatizo hilo huitwa Pre-mature birth (kuzaa njiti).

NINI HUSABABISHA MISCARRIAGE? 


Zipo sababu nyingi zinazosababisha ujauzito uchoropoke. 

Matatizo ya Vinasaba (Genetic Factors)



Hitilafu katika Kromosomu (Chromosomal abnormalities) ambayo husababisha vinasaba kuwa katika hali isiyo ya kawaida, inatajwa kuwa sababu kubwa zaidi inayosababisha ujauzito uchoropoke ukiwa na umri wa chini ya wiki 13.


Matatizo haya husababisha damu ya mama ishindwe kuendana na ya mtoto na kusababisha reactions ambazo humdhuru mtoto na kumfanya ashindwe kuhimili hali ya tumboni kwa mama. Hivyo ujauzito kuharibika. 

2. Upungufu wa Homoni (Progesterone Deficiency)



Homoni ya Progesterone hufanya kazi kubwa kuanzia mimba inapotungwa mpaka mtoto anapozaliwa. Progesterone 


ndiyo huchochea uimara wa ukuta wa Placenta ambao mtoto hujishikiza. Upungufu wa homoni hii husababisha ukuta wa 


mji wa mimba kushindwa kuhimili uzito wa mtoto, hali ambayo husababisha ujauzito kuharibika na kutoka kabla ya muda 
wake.



MIMBA KUCHOROPOKA (MISCARRIAGE)-2



NINI HUSABABISHA MIMBA KUCHOROPOKA?


Zipo sababu nyingi zinazoweza kusababisha mimba kuharibika kisha kuchoropoka. Baadhi ni kama zifuatazo:

UMRI MKUBWA
Kwa kawaida, mwanamke anapofikisha umri wa miaka 35 au zaidi, misuli (sphincters) ya mji wake wa uzazi hulegea na kupungua nguvu za kuweza kuhimili na kutunza kiumbe kinachokuwa ndani ya mji wa uzazi. Kulegea kwa misuli hii husababisha mimba kuchoropoka kwa urahisi.

MAGONJWA
Wanawake wanaosumbuliwa na magonjwa kama kisukari, unene kupindukia (obesity), Polycystic Ovary Syndrome, malaria kali, magonjwa ya zinaa na mengineyo huwa katika hatari kubwa ya mimba zao kutoka.

HITILAFU KATIKA KIZAZI
Baadhi ya wanawake huwa na mfuko wa mimba (uterus) ambao muundo wake siyo wa kawaida (T- Shaped Uterus). Wanawake wenye tatizo hili, huwa na hatari kubwa ya mimba zao kuharibika kabla ya kutimiza umri wa miezi tisa.

MAAMBUKIZI YA BAKTERIA AU FANGASI

Maambukizi ya bakteria au fangasi husababisha misuli ya kizazi kushambuliwa na kisha kupoteza uwezo wake wa kuhifadhi ujauzito, jambo ambalo husababisha mimba kuchoropoka.
Sababu nyingine ni pamoja matumizi ya pombe kali, uvutaji sigara, matumizi ya dawa za kulevya, kemikali, matatizo ya kurithi n.k

DALILI ZA MIMBA KUCHOROPOKA (Symptoms of a miscarriage):


1. KUTOKWA NA DAMU SEHEMU ZA SIRI
Dalili kubwa za miscarriage ni mjamzito kutokwa na damu (nzito au nyepesi) sehemu za siri kwa vipindi au mfululizo. Damu hizi hutoka kama zile zitokazo kwa mwanamke anapokuwa kwenye siku zake.



MIMBA KUCHOROPOKA (MISCARRIAGE)-3




DALILI ZA MIMBA KUCHOROPOKA (Symptoms of a miscarriage):

1. KUTOKWA NA DAMU SEHEMU ZA SIRI



Dalili kubwa za Miscarriage ni mama mjamzito kutokwa na damu (nzito au nyepesi) sehemu za siri kwa vipindi au mfululizo. Damu hizi hutoka kama zile zitokazo mwanamke anapokuwa kwenye siku zake na huambatana na maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu. 

2. MAUMIVU MAKALI YA VIUNGO

Dalili nyingine za mimba inayotaka kuchoropoka ni maumivu makali ya mgongo, kiuno, nyonga na tumbo chini ya kitovu. Maumivu haya huanza taratibu lakini huongezeka kadiri muda unavyozidi kusonga mbele. Pia huambatana na kutokwa na damu kama ilivyoelewa hapo juu.

3. KUTOKWA NA UCHAFU SEHEMU ZA SIRI
Dalili nyingine kubwa ya Miscarriage ni mama mjamzito kuanza kutokwa na uchafu wenye rangi sambamba na mabonge ya damu sehemu za siri.

ANGALIZO: Dalili hizi pekee hazitoshi kuashiria kuwa tayari ujauzito umeharibika ila mama mjamzito anapoona moja kati ya dalili hizi au zote, anashauriwa kuwahi hospitali kuonana na daktari haraka iwezekanavyo.
Endapo mama atachelewa, atakuwa anajisababishia matatizo zaidi kwani sumu za kiumbe kilichoharibika huharibu mfuko wa uzazi na kusababisha matatizo makubwa siku za mbeleni ikiwemo ugumba.

MADHARA YA MISCARRIAGE


Kuna madhara mengi kiafya kwa ujauzito kuharibika. Miongoni mwa madhara hayo ni kuharibika kwa kizazi ikiwa mama hatasafishwa vizuri tumbo baada ya ujauzito wa awali kuharibika. Madhara mengine ni kuugua mfululizo baada ya ujauzito 
kuharibika ambapo mwanamke hushambuliwa na maradhi mbalimbali ya tumbo.


Madhara mengine ya ujauzito kuharibika ni kuathirika kisaikolojia kwa mwanamke husika. Madhara ya kimwili yanaweza kuisha haraka na kusahaulika lakini madhara ya kisaikolojia huchukua muda mrefu kusahaulika.


Baadhi ya wanawake waliopatwa na tatizo hili, hujisikia vibaya sana wanapokutana na wanawake wenzao wakiwa wajawazito au wakiwa na watoto wao wachanga, jambo ambalo husababisha msongo.



0 comments:

Post a Comment