Tuesday 17 June 2014

MAUMIVU YA SHINGO NA MGONGO

Tatizo hili huwasumbua baadhi ya watu wake kwa waume na zaidi ni watu wazima. Tatizo huwapata zaidi watu wa umri wa kati, yaani miaka 35 hadi 45 na huwa makali zaidi katika umri zaidi ya miaka 45.
Kazi ambayo mtu anaifanya huchangia kwa kiasi kikubwa hali hii ya maumivu. Zipo sababu mbalimbali zinazochangia hali hii ya maumivu ambazo tutakuja kuziona.

CHANZO CHA MAUMIVU
Maumivu ya shingo na mgongo hutokana na matatizo kwenye mishipa ya fahamu inayotokea katika uti wa mgongo. Mishipa ya fahamu inasimamiwa na uti wa mgongo na ubongo.
Matatizo katika ubongo husababisha maumivu makali ya kichwa na shingo na mambo yanayochangia ni malaria, homa ya uti wa mgongo, uvimbe kwenye ubongo na kuumia kichwa kutokana na ajali ya aina yoyote.
Maumivu ya shingo na mgongo husababishwa na maambukizi kama yale ya kichwani, mfano malaria na homa ya uti wa mgongo, uvimbe shingoni, kuumia shingo na mgongo, uvimbe, kufanya kazi ya kuinama kwa muda mrefu. Hali hii huwatokea zaidi watu wanaobeba vitu vizito kichwani, wanaokaa kwenye kiti muda mrefu na kiti ambacho hakipo katika kiwango kizuri cha kufanya mgongo na shingo vikae vizuri.
Kuumia pia kunaweza kusababishwa na gari kufunga breki ghafla na endapo hujafunga mkanda na kiti hakina ‘brace’ ya kusaidia kichwa, hivyo shingo itatikiswa kwa nguvu. Vilevile unaweza kuumia kwa kugonga kichwa sehemu ngumu, mfano kwenye bwawa la kuogelea au sehemu nyingine yoyote, kulala vibaya pia kunaweza kukusababishia uamke ukiwa na maumivu ya shingo na mgongo.
Uwepo wa magonjwa kama kisukari na shinikizo la juu la damu huchangia kuhisi maumivu hayo ya shingo na mgongo. Uchovu wa mwili kutokana na kazi za kila siku au msongo wa mawazo pia husababisha upate maumivu ya shingo na mgongo ambayo yanaweza kuwa makali sana au wastani.
Maumivu ya wastani huchukua muda mrefu na huendelea taratibu tofauti na yale makali ambayo huchukua muda mfupi lakini pia huweza kuchukua muda mrefu.
DALILI ZA TATIZO
Maumivu ya shingo huweza kuanza ghafla au taratibu, maumivu husambaa kichwani au kushuka kwenye uti wa mgongo chini kidogo ya shingo. Mgonjwa huhisi maumivu ya kichwa kisogoni au kama kichwa kimechoka, hukosa usingizi na kichwa kuwa kizito.
Shingo pia huhisi inauma na imechoka, maumivu ya shingo husambaa hadi kwa mbele na wakati mwingine huhisi maumivu wakati wa kumeza chakula.
Maumivu husambaa mabegani na mgongoni kwa juu, mgonjwa pia huhisi maumivu ya kifua na kila wakati hupenda kujinyoosha, wakati mwingine maumivu husambaa hadi mikononi na kwenye vidole.
Hali ikiwa mbaya, mgonjwa huhisi ganzi vidoleni, aidha mkono mmoja au mikono yote miwili. Mgonjwa huhisi homa au mwili huwa dhaifu muda wote ila akitumia dawa za kutuliza maumivu hupata nafuu ambayo ni ya muda.
Mgonjwa hupoteza hamu ya kula, mwili huwa mchovu na hupoteza hamu ya tendo la ndoa. Ufanisi kazini hupungua na muda mwingi unapenda kupumzika.
 UCHUNGUZI
Uchunguzi hufanyika katika hospitali kubwa ambapo mgonjwa atafanyiwa vipimo mbalimbali kuangalia kwa undani visababishi vya tatizo. Mfano vipimo vya damu, shinikizo la damu, vipimo vya moyo na kipimo cha ‘MRI’ ili kuangalia kama ana uvimbe kwenye shingo au kichwani au kama ana tatizo lingine lolote sehemu hiyo.
MATIBABU NA USHAURI
Baadhi ya uchunguzi wa kina na vipimo mbalimbali hufanyika kisha matibabu yatafuata. Tiba itakuwa katika chanzo cha kutuliza maumivu, epuka kunywa dawa za kutuliza maumivu bila ya kuwa na uhakika wa tatizo linalosumbua.

8 comments:

  1. Kwanza kazi yangu ni ufundi hasa wa Computer ni natatizo la maumivu ya mabega na shingo mara nyingine mpaka mkono wa kushoto unanilazimu kuushusha pindi nikiwa nimekaa kwa kiti na mikona nimeweka kwa meza hilitatizo limenianza muda mrefu sana sijui nini tatizo je kazi hii inaweza kuwa sababu au?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndio inachangia kukaa sehemu moja muda mrefu na kuinama sana pia kunachangia kupata maumivu ya shingo na mgongo.

      Delete
  2. Naomba kujua je maumivu ya shingo au kiuno ni moja ya dalili za UKIMWI??

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapana Maumivu ya Shingo na mgongo yanatokana na asidi kuzidi mwilini sio dalili ya ukimwi.

      Delete
  3. nasumbuliwa sana na msongo wa mawazo mpaka najihisi kuvurugwa

    ReplyDelete
  4. Samahani, asid ikizidi mwilini, utafanya nini ili isiongezeke na ipungue,nitumie nini?

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  6. jmn mi maumivu yameanza juzi yan jana na leo ndo yamezid nmehic labd nimelalia shingo vibaya ila mbn ndo yanzizid kadri cku zinavyozd kwenda badal kupungua?

    ReplyDelete