Thursday, 19 June 2014

MAUMIVU CHINI YA TUMBO


Tatizo la maumivu chini ya tumbo huwasumbua baadhi ya wanawake huku vyanzo halisi vya maumivu vikiwa vingi tu.
Maumivu chini ya tumbo au chini ya kitovu huweza kusababishwa na mambo mbalimbali kama tutakavyoona.
Maumivu huwapata wasichana ambao tayari wameshavunja ungo na wanawake watu wazima, ingawa hata wasichana wadogo ambao bado hawajavunja ungo husumbuliwa.
CHANZO CHA TATIZO
Chanzo cha maumivu haya kinaweza kuwa maambukizi, uvimbe au kushikamana kwa viungo vya ndani ya uzazi kunakosababishwa na upasuaji wa tumbo wa siku za nyuma.

Maumivu haya pia yanahusiana na matatizo katika kibofu cha mkojo, mirija ya mkojo itoayo mkojo toka katika figo, matatizo katika mfuko wa haja kubwa na ngiri au henia ya kitovu.
Maumivu haya wengine huita chango la uzazi.

Uvimbe ndani ya kizazi unaweza kuwa fibroid, uvimbe wa mirija ya mayai ambayo inaweza kujaa maji au usaha. Uvimbe wa vifuko vya mayai na uvimbe kati ya kizazi na vifuko vya mayai. Maambukizi sugu ndani ya kizazi ni tatizo kubwa.
Ngiri ya tumbo inaweza kuwa usawa wa kitovu au katika mishono ya operesheni ya siku za nyuma na maumivu haya huwa zaidi nyakati za baridi.
DALILI ZA TATIZO
Maumivu chini ya tumbo yanaweza kuwa ya moja kwa moja ambayo hayana muda wa unafuu wakati wote mgonjwa huhisi maumivu.
Maumivu pia yanaweza kuja na kupotea.

Wengine huhisi maumivu hadi abonyezwe chini ya tumbo hasa anapopimwa na daktari, wengine hupatwa na maumivu haya baada ya kumaliza tendo la ndoa.
Maumivu yanaweza kuwa pande zote mbili, chini ya tumbo yaani kulia na kushoto au katikati tu.
Maumivu ya upande mmoja yanaweza kusambaa hadi mguuni au kumfanya mgonjwa apate shida kutembea hasa anaponyanyuka na kuanza kutembea lakini kadiri anavyotembea maumivu huisha yenyewe.

Hali ya maumivu pia husambaa hadi kiunoni au katika ubavu mmoja kutegemea na tatizo lipo sehemu gani.  Mgonjwa husumbuka kwa muda mrefu na huhisi mwili unachoka.
Vipimo vya mkojo havisaidii kupata jibu sahihi la tatizo hili. Kipimo cha Ultrasound kinaweza kionyeshe au kisionyeshe tatizo.

Tatizo likiwa kubwa huhisi mgonjwa ana tatizo la nyonga lakini vipimo vya X-ray, MRI vitakuwa sawa na hata vipimo vya damu havitaonyesha tatizo.
Mgonjwa hulalamika kutumia dawa nyingi za kutuliza maumivu bila mafanikio.

UCHUNGUZI
Tatizo hili linahitaji utaratibu na umakini katika kulichunguza. Vipimo mbalimbali vitafanyika kama vya damu, mkojo, Ultrasound na vipimo vya kuangalia ukeni ili kuona kama kuna tatizo kubwa linalohusiana na sehemu ya ndani ya kizazi.

MATIBABU NA USHAURI
Baada ya uchunguzi wa kina katika kliniki za magonjwa ya kinamama, vipimo kukamilika, matibabu hufanyika.
Tiba itatolewa kwa jinsi vipimo vinavyoonyesha.  Inashauriwa kuwahi hospitali na muone daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama katika hospitali za wilaya na mikoa kwa uchunguzi zaidi.

Related Posts:

  • SABABU ZA TATIZO LA KUTOKUPATA MIMBA-2 Leo nitaelezea matibabu na ushauri kwa wanandoa wanaokabiliwa na tatizo la mama kutopata mimba. Miongoni mwa mambo wanayopaswa kuelezwa  wanandoa hao ni kuwapa uzoefu kuhusiana na afya ya uzazi na jinsi ujauzito una… Read More
  • TATIZO LA UTOKWAJI MAJIMAJI MACHAFU KATIKA VIA VYA UZAZI VYA MWANAMKE-3 WIKI iliyopita tulijadili vyanzo vya tatizo hili linalowakabili wanawake wengi ambavyo ni maambukizo/mashambulio katika ya fangusi aina ya candida au bakteria aina ya chlamidia kwenye njia ya uzazi ya mwanamke, ulaj… Read More
  • TATIZO LA KUTOKWA NA HARUFU MBAYA MWILINI Harufu mbaya ni kitu kisichompendeza mtu yeyote. Unapotoa harufu mbaya toka mwilini mwako, haikupendezi wewe mwenyewe wala mtu wa jirani. Kama kitu hukipendi wewe na ukakiona hakifai basi usimlazimishe mwenzio akipende a… Read More
  • UGONJWA WA ZINAA WA TRICHOMONIASIS . Leo pia tutaendelea kuyajadili magonjwa ya zinaa ambapo tutazungumzia ugonjwa wa Trichomaniasis, ambao huwaathiri sana wanawake kuliko wanaume. I. Ugonjwa wa Trichomoniasis ni ugonjwa unaosababis… Read More
  • TIBA YA SARATANI YA MATITI - 6 Tumekuwa tukielezea ugonjwa wa saratani ya matiti kwa wiki tatu na hii ni sehemu ya mwisho nikiamini kuwa sasa wengi wameuelewa. Wiki iliyopita tulielezea tiba kwa kemikali na leo tunaendelea na tiba kwa njia ya homoni. … Read More

0 comments:

Post a Comment