Friday, 13 June 2014

KUTOKWA NA DAMU KATIKA UFIZI WAKATI WA UJA UZITO

Kuna wanawake wengine wakiwa wajawazito wanapatwa na hili tatizo la kutokwa na damu katika fizi, kuvimba kwa fizi au kuumwa kwa fizi. 

Hali hii ni ya kawaida kwa kuwa wakati wa ujauzito na hutokana na membrane za mucous mwilini kuwa sensitive sana, kuongezeka kwa mzunguko wa damu kwenye maeneo ya mdomo, na pia kuongezeka kwa hormone ya uzazi ya progesterone ambayo inaweza kusababisha fizi kuwa sensitive zaidi.

Kutatua tatizo hili unaweza ukamtembelea daktari wa meno kusaidia katika kusafisha meno vizuri. Pia jaribu kuongeza vyakula vyenye Vitamin  C katika diet yako kama matunda jamii ya machungwa. Piga mswaki mara mbili kwa siku, tafuta mswaki laini ili usiumize fizi wakati wa kupiga mswaki.

Pia jaribu kupunguza kula vitu vyenye sukari nyingi kama pipi, soda n.k Pia kama unatatizo la kusikia kichefu chefu na kutapika kwa wakati huu jaribu kupiga mswaki kila mara unapotapika ili kuzuia bacteria mdomoni.


Related Posts:

  • UGONJWA WA ZINAA WA TRICHOMONIASIS . Leo pia tutaendelea kuyajadili magonjwa ya zinaa ambapo tutazungumzia ugonjwa wa Trichomaniasis, ambao huwaathiri sana wanawake kuliko wanaume. I. Ugonjwa wa Trichomoniasis ni ugonjwa unaosababis… Read More
  • SABABU ZA TATIZO LA KUTOPATA MIMBA - 3 Kipimo cha upevushaji wa mayai kupima mirija ya uzazi, upasuaji mdogo kwenye tumbo na kumulika ndani ya mwili wake pia kipimo cha Ultrasound kitafanyika. Vipimo kwa upande wa wanaumeBaada ya kuchukuwa historia  ya … Read More
  • SABABU ZA TATIZO LA KUTOKUPATA MIMBA-2 Leo nitaelezea matibabu na ushauri kwa wanandoa wanaokabiliwa na tatizo la mama kutopata mimba. Miongoni mwa mambo wanayopaswa kuelezwa  wanandoa hao ni kuwapa uzoefu kuhusiana na afya ya uzazi na jinsi ujauzito una… Read More
  • TATIZO LA UTOKWAJI MAJIMAJI MACHAFU KATIKA VIA VYA UZAZI VYA MWANAMKE-3 WIKI iliyopita tulijadili vyanzo vya tatizo hili linalowakabili wanawake wengi ambavyo ni maambukizo/mashambulio katika ya fangusi aina ya candida au bakteria aina ya chlamidia kwenye njia ya uzazi ya mwanamke, ulaj… Read More
  • TATIZO LA KUTOKWA NA HARUFU MBAYA MWILINI Harufu mbaya ni kitu kisichompendeza mtu yeyote. Unapotoa harufu mbaya toka mwilini mwako, haikupendezi wewe mwenyewe wala mtu wa jirani. Kama kitu hukipendi wewe na ukakiona hakifai basi usimlazimishe mwenzio akipende a… Read More

0 comments:

Post a Comment