Friday 2 May 2014

ZIJUE SABABU 3 KWA NINI MBU HAWEZI KUSAMBAZA VVU(HIV)


1. Kwanza mdomo wa mbu haupo kama
sindano za kawaida zinazotumika, mlija wa
mbu ambao hutumika kuingizia mate yenye  vimelea vya malaria ni tofauti na ule
unaotumika kufyonza damu kutoka kwa
binadamu, 
 kutokana na hili kwaiyo damu tu
ndio huingia kwenye mwili wa mbu kutoka
kwa binadamu alieng`atwa na mbu, na mate
tu ya mbu ndio huingizwa kwenye mwili wa
binadamu.


2. Pili magonjwa yote ambayo huambukizwa
na insekta kama, matende na malaria aya
magonjwa yanaweza kusambazwa na mbu
kwa sababu vimelea vya aya magonjwa
 
huweza kujizalisha(multiply) katika mwili wa
mbu, ambapo hivi vimelea huweza kusambaa
hadi kwenye mate ya mbu baada ya hapo
huweza kuingizwa kwa kung`atwa
 
binadamu. Tofauti ni kwamba vimelea yani
virusi vya ukimwi(vvu) vinapoingia kwenye
mfumo mzima wa mmeng`enyo wa mbu
 
humeng`enywa kama chakula cha kawaida
kisha hutoka kama uchafu, ili virusi vya
ukimwi viweze kujizalisha(multiply) ni lazima
viingie kwenye seli maalumu za binadamu.

3. Tatu, virusi vinavyosabisha ukimwi
huzunguka taratibu kwenye damu
ukilingansha na vimelea vinavyosababisha
magonjwa yatokanayo na insekta(mbu), hii
inamaanisha ata mbu anaponyonya damu
 
kwa binadamu ambaye tayari virusi
vya ukimwi hawezi kunyonya idadi kubwa ya
virusi.
Tafiti zaidi zinaonyesha kwamba ili
mbu aweze kueneza virusi vya ukimwi kwa
binadamu mtu huyo ina bidi ang`atwe na
 
mbu million kumi(10) idadi hii ya mbu ndio
inaweza kutengeneza uniti moja(1) ya kirusi
apo ndipo huenda kikasababisha kueneza
 
vvu, hii inamaanisha ata ikatokea kwa bahati
mbaya uka mmeza mbu aliye mng`ata
binadamu ambaye ana virusi vinavyosabisha
ukimwi huwezi kupata maambukizi.



MUHIMU
Achana na ngono zembe kwani
huchangia kwa asilimia kubwa maambukizi
ya VVU ambavyo usababisha UKIMWI…
jiondoe
kwenye mtandao wa kuwa na wapenzi
wengi mapema.

0 comments:

Post a Comment