Thursday 8 May 2014

TUMIA GILGILANI NA MANJANO KUONDOWA MADOWA MEUSI

Leo  kwenye safu yetu ya urembo tutaongelea ngozi zetu hasa usoni kwani wanawake wengi na hata wanaume hupendelea sana ngozi hasa ya usoni kwa sababu ndiyo sehemu inayoonekana kwanza.
Kwa kuilinda ngozi yako ya usoni isipate bakteria na chunusi, tumia kiungo cha giligiliani kitakusaidia kwa shida yako, hii ni kwa wale wanaosumbuliwa na chunusi pamoja na madoamadoa.
Jinsi ya kufanya
Ili kuondoa chunusi na madoa meusi.
Twanga au sigina majani ya giligiliani, chuja au kamua ili kupata maji yake. Pima vijiko vinne vya maji ya giligiliani kisha changanya na kijiko 1 cha chakula cha manjano (binzari manjano).
Baada ya maandalizi hayo, pakaa kwenye ngozi. Acha ikauke, kisha osha au nawa na maji ya vuguvugu.
Onyo: Usisugue ngozi paka kama kawaida tu kisha osha, ukisugua inaweza kukusababishia mchubuko wa ngozi na majeraha yasiyotakiwa.
***
Manjano na Maziwa ni maski nzuri ya kuondoa makunyanzi.
Vifaa 
Chukua vijiko 2 vya unga wa manjano,
kijiko kimoja kikubwa cha maziwa.
Changanya maziwa na manjano, utaona ni maziwa kidogo lakini ndiyo vizuri upate mchanganyiko mzito utakusaidia kukauka mapema kwenye ngozi
Baada ya hapo tumia mikono yako kupaka usoni, epuka kupaka eneo la macho. Ukishapaka acha kwa muda wa dakika 15-20.
Kama utasikia uso umeanza kukaza basi jua ndiyo inafanya kazi, osha kwa maji ya baridi.
Unaweza kutumia mask hii kwa wiki mara mbili tu, hii ni kwa ajili ya kuondoa makunyanzi na kuifanya ngozi iteleze na kuwa nyororo.

0 comments:

Post a Comment