
Wanaume wasio na ajira wako katika hatrari ya kuathirika zaidi kutokana na ugomvi
Ugomvi wa mara kwa mara baina ya wapenzi, marafiki ama hata jamii unaongeza hatari ya kufa kwa watu wenye umri wa makamo.Haya ni kwa mujibu wa watafiti nchini Denmark.
Watafiti wamesema kuwa wanaume na wale ambao hawana kazi wako katika hatari Zaidi.
Pia kulingana na utafiti huo utu wa mtu na uwezo wa mtu binafsi kukabiliana na dhiki ilichangia katika matokeo ya utafiti huo.Utafiti huo katika jarida la 'Epidemiology and Community Health',unasema kuwa shughuli za kukidhi matakwa na mahitaji ya jamii pia zimehusishwa na idadi kubwa ya vifo vya mapema.
Ingawa watafiti hao kutoka chuo kikuu cha Copenhagen waliweza kupata uhusiano uliopo kati ya vifo vya mapema na kugombana, na kuwa ugomvi uliongeza hatari ya vifo vya mapema mara tatu, hawakuweza kuelezea kikamilifu sababu haswa ya hali hiyo.
Utafiti wa hapo awali ulionyesha kuwa watu wenye wasiwasi mwingi na mahitaji mengi
kutoka kwa wapenzi wao na watoto, pamoja na wale wanao gombana mara kwa mara na jamaa wao, wamo katika hatari kubwa zaidi ya kuugua magonjwa ya moyo na kiharusi.
Tafiti za hapo awali pia zaonyesha kuwa utangamano mwema na watu pamoja na marafiki wengi ina athari chanya katika afya, huku utu kwa kiasi kikubwa ukiamua jinsi mtu hupokea na kuguswa na hali za kijamii pamoja na mahusiano.
Wapendanao hawapaswi kugombana

Kumsumbua mpenzi wako pia kunahatarisha afya
Katika utafiti huu, watafiti walisema kuwa athari za kisaikolojia zinazosababishwa na dhiki, kama vile shinikizo la damu na ongezeko la athari ya magonjwa ya moyo, ndizo hasa zinaweza kueleza athari ya ongezeko la vifo vya mapema.
Utafiti umeonyesha kuwa wanaume wanapokabiliwa na hali za dhiki kwa kuongeza homoni inayokabiliana na hali ya dhiki na wasiwasi, jambo ambalo linazidisha athari ya kiafya.
Utafiti huo ulihusisha watu 9,875 wake kwa waume wenye umri wa kati ya miaka 36 na 52 na ulitumiwa kuchunguza uhusiano uliopo baina ya hali ngumu ya uhusiano wa kijamii na vifo vya mapema.
Wote walikuwa wameshiriki katika Utafiti ‘Denmark Longitudinal’ kuhusu Ajira, ukosefu wa ajira na afya , kuanzia mwaka wa 2000.
Utafiti uligundua kuwa wasiwasi wa mara kwa mara au mahitaji yanayotokana na wapenzi na watoto ulihusishwa na ongezeko la kufikia 50%- 100% la vifo vya mapema.
Ukosefu wa ajira ulionekana kuongeza athari hasi za uhusiano mgumu wa kijamii. Wale
ambao hawako kazini wameonekana kuwa katika hatari kubwa zaidi ya kifo kutokana na jambo lolote kinyume na wale walio na kazi.
wanaume pia wako katika hatari zaidi kutokana na mahitaji na wasiwasi unaotokana na wapenzi wao wa kike , huku wakiwa katika hatari kubwa zaidi ya kifo zaidi ya ile ambayo kwa kawaida imehusishwa na kuwa mwanamume.
Dakta Rikke Lund, wa kitengo cha afya ya u,mma katika chuo kikuu cha Copenhagen amesema kuwa wasiwasi na ugomvi ni sehemu ya maisha. Lakini akaongeza kuwa watu ambao wanakuwa na migogoro mara kwa mara wako katika hatari zaidi lakini wanaweza wakasaidiwa.chanzo.
Related Posts:
NI KWELI MAYAI HUSABABISHA UGONJWA WA MOYO?
UTAFITI uliofanywa nchini Marekani hivi karibuni unaonesha kuwa katika miaka ya 1950, wastani wa ulaji wa mayai ya kuku ulikuwa mayai 375 kwa mtu mmoja, lakini hadi kufikia mwaka 2007, kiwango hicho kimepungua hadi … Read More
CHAKULA NI TIBA NZURI, IJUE SIRI YAKE
Watu wengi tuna desturi ya kula ili tushibe. Katika ulaji huo wakati mwingine tunajitendea ukatili wenyewe kwa kula vyakula visivyo sahihi ambavyo vinapoingia mwilini hugeuka kuwa sumu.
Lakini vyakula pia ni dawa na leo… Read More
WHO YATOA TAHADHARI KWA WANAOTUMIA SUKARI NYINGI
WATAALAMU wa afya wametahadharisha kwamba juhudi zaidi zinahitajika kufanyika kupunguza kiwango cha sukari kinachotumiwa na watu.
Shirika la Afya Duniani (WHO), kushirikiana na washauri wa masuala ya … Read More
MIFUPA YA N'GOMBE TIBA YA KUONDOWA FLORAIDI MAJINI
UTAFITI mbalimbali uliofanywa na Wizara ya Maji
na Umwagiliaji, umebaini kwamba mifupa ya
ng’ombe ina uwezo mkubwa wa kupunguza kiasi
cha madini ya floraidi katika maji ya kunjwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijin… Read More
UHUSIANO WA KUKOROMA NA MAGONJWA YA MOYO
Iwapo utamtikisa au kumgusa hali hiyo hupotea kwa sekunde kadhaa na kama atapata tena usingizi mlio huo hujirudia tena.
Kukoroma, licha ya kuchukuliwa kuwa ni jambo la kawaida, lakini huenda likawa ni kero kubwa kw… Read More
0 comments:
Post a Comment