Watafiti wa nchini Israel walibaini
kuwa, mtu anayekunywa chai mara
kwa mara ana uwezo wa kuishi
muda mrefu tofauti na yule
asiyependa chai.
Aghalabu maisha ya mwanadamu
yeyote yule yapo mikononi mwa
muumba wake, ambaye hujua lini
muda wa kuishi wa kiumbe wake
utakwisha. Lakini mtindo wa
maisha yetu usiojali kanuni za afya,
umeonyesha kuwa ndicho chanzo
cha watu wengi kuishi maisha
mafupi.
Kiwango cha maisha ya binadamu
sasa kinapunguzwa kutokana na
mabadiliko ya tabianchi, mtindo
wa maisha na mazingira, lakini
wanasayansi na wataalamu wa
afya wamekuja na mbinu ambazo
zinatajwa kusaidia kuongeza miaka
yako ya kuishi.
KUNYWA CHAI
Watafiti wa nchini Israel walibaini
kuwa, mtu anayekunywa chai mara
kwa mara ana uwezo wa kuishi
muda mrefu tofauti na yule
asiyependa chai.
Chai, hasa ya kijani (green tea) ina
ondoa sumu iitwayo ‘polyphenols’
ambayo husaidia mwili wako
kupambana na magonjwa ya
moyo.
Wataalamu hao wanasema, chai
iliyochemka vizuri au pakiti ya
majani ya chai kukorogwa vyema
katika majimoto, yafaa zaidi. Kwa
kifupi, chai ikolee majani.
KUSIMAMA KWA MGUU MMOJA KILA
ASUBUHI
Inaweza kuonekana kuwa ni jambo
la ajabu, lakini wanasayansi
wamebaini kuwa kusimama kwa
mguu mmoja asubuhi kunasaidia
kuimarisha misuli ya mgongo,
nyonga na tumbo na kuupa
uwiano uti wa mgongo.
Mtaalamu wa viungo
anasema, zoezi hili jepesi
likifanywa kila siku, linatoa
manufaa ya muda mrefu na
linakukinga kuvunjika mifupa kwa
urahisi hasa unapoanza kuzeeka.
Tafuta marafiki sita unaowaamini
Kuwa na marafiki wazuri na familia
ambayo unaiamini ni siri moja
kubwa ya kuishi miaka 100.
Utafiti uliofanywa na kitengo cha
Maisha na Mazingira katika Chuo
Kikuu cha Australia, ulionyesha
kuwa kupata watu wa kukupa
msaada na kukufariji wakati wa
huzuni kunasaidia kuongeza umri
wa kuishi kwa kuzalisha kemikali
ya ‘furaha’ inayofahamika kama
dopamine na oxtocyin ambavyo
huusaidia ubongo.
Mwanasaikolojia wa Chuo Kikuu
cha Dodoma,
anasema unapokuwa na tatizo,
kisha ukalihifadhi moyoni, unaunda
uchungu ambao unakuathiri.
Anasema, mwili wa mtu
unaathiriwa kutokana na tabia au
matendo ya moyoni, unapohifadhi
tatizo bila kupata ushauri unakuza
tatizo hilo.
“Marafiki au hata ndugu wa
kumweleza tatizo lako ni muhimu,
wanaweza kukupoza,” anasema
USISHIBE SANA
Wakazi wa kisiwa cha Okinawa,
nchini Japan, wanaongoza kwa
kuwa na kiasi kidogo cha watu
wenye unene uliopitiliza (obesity)
na wanasifika kwa kuwa na idadi
kubwa ya watu wanaoishi zaidi ya
miaka 100.
Siri yao kubwa ni kuwa hawali
wakashiba kwa zaidi ya asilimia 80.
Watafiti wa Marekani pia,
wamebaini kuwa, binadamu
wanaweza kuishi miaka mingi zaidi
iwapo chakula wanachokula
kinapunguzwa kwa robo tatu.
Ina maana kwamba kula kidogo
kunaufanya mwili wako usiwe na
kazi kubwa ya kumeng’enya, hivyo
kuupa nafasi ya kuwajibika na kazi
nyingine.
Mtaalamu wa chakula na lishe,
anasema, mtu
hatakiwi kula akashiba bali
anatakiwa aache njaa kwa mbali ili
kutoa nafasi ya maji na
mmengenyo kuchukua nafasi.
LALA KWA MUDA MREFU
Ukosefu wa usingizi unakuweka
katika hatari kubwa ya kupata
maradhi ya msongo wa mawazo
na moyo. Kupata makunyanzi na
mwili kuchoka.
Mabadiliko kidogo tu ya kitabia
yanaweza kuleta mapinduzi
makubwa katika afya yako.
Wanaopata usingizi wa kutosha si
rahisi kupatwa na kiharusi au
shinikizo la damu.
PIGA MSWAKI
Maradhi ya fizi, ni maradhi
yaliyopata umaarufu duniani. Dk
James Russel wa kituo cha tiba cha
Hope, anasema, meno na fizi ni
chanzo cha magonjwa mengi
ambayo wengi hudhani
hayahusiani na afya ya kinywa.
Maradhi ya fizi yanatajwa kuwa
chanzo cha saratani za aina fulani,
maradhi ya moyo, ubongo na hata
kisukari.
KUWA MAKINI
Utafiti uliofanywa na
Mwanasaikolojia wa nchini
Marekani, Dk Howard Friedman
unasema kuwa, umakini wa mtu ni
kigezo cha urefu wa maisha yake.
Watu ambao wapo makini na
maamuzi, matumizi ya fedha na
ambao wanapenda kuweka kila
kitu sawa na kufanya mambo yao
kwa uangalifu, wanaweza kuishi
kwa muda mrefu.
KWA NINI?
Dk Kitila Mkumbo, Mwanasaikolojia
wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu
(DUCE) anasema, unapokuwa
makini unafanya uamuzi mzuri
ambayo hupunguza kiwango cha
kuishi maisha hatarishi.
“Umakini unamsaidia mtu kuepuka
tabia hatarishi kwa mfano ngono
zembe, kuvuta sigara, mambo
ambayo yanahatarisha afya,”
anasema.
Anasema, mtu anayepangilia
mambo yake na kuwa makini kwa
mfano kutumia kinga wakati wa
tendo la ndoa kunakuepusha na
maambukizi ya maradhi
mbalimbali.
USIWEKE MATUNDA KWENYE JOKOFU
Unaweza kufikiri kuwa, kuyaweka
matunda katika jokofu, unayafanya
yadumu kwa muda mrefu, lakini
tafiti zinaonyesha kuwa, matunda
yaliyopoozwa kwa baridi ya jokofu,
yanapungukiwa vitamini muhimu
kuliko matunda yanayowekwa
katika hali ya kawaida.
Kwa mfano, nyanya na pilili ni
vyema kuwekwa katika bakuli
kuliko katika jokofu. Matunda
mengi yanasaidia kuondoa sumu
mwilini hivyo lishe zake zikibaki
bila kuharibiwa, husaidia kujenga
moyo imara na kupunguza
kiwango aina fulani za saratani.
KUFANYA TENDO LA NDOA ANGALAU
MARA MBILI KWA WIKI
Utafiti mkubwa na uliothibitishwa
wa Welsh na wenzake wa Hospitali
ya Royal Edinburgh, Uingereza
ulibaini kuwa wale wanaofanya
mapenzi mara moja kwa mwezi
wapo katika hatari ya kufa
mapema, ukilinganisha na wale
wanaofanya mapenzi mara mbili
kwa wiki.
Welsh anasema, tendo la ndoa
linapunguza msongo wa mawazo
na kumfanya mtu apate usingizi
mzuri. Msongo wa mawazo
unasababisha maradhi ya moyo na
kisukari.
Dk Mkumbo anasema, tendo la
ndoa ni jambo la afya na husaidia
katika kupunguza msongo wa
mawazo na kuupa mwili
uchangamfu.
Hata hivyo Dk Mkumbo anasema
hajawahi kusikia idadi ya siku za
kufanya mapenzi kama ni mara
moja au mbili kwa wiki, bali
anaamini kitendo chenyewe kina
umuhimu wake kiafya.
Kwa nini Wajapan wanaishi maisha
marefu?
Inaelezwa kuwa Wajapan ni taifa
linaloongoza kwa kuwa na watu
wanaoishi muda mrefu kuliko
mataifa mengine.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani
zinaeleza kuwa, raia wa Japan
wanaishi maisha marefu zaidi.
Kwa mfano, mwanaume mzee
kuliko wote aliyevunja rekodi ni
Jiroemon Kimura, kutoka Kyotango,
Kyotto, Japan aliyefariki dunia
akiwa na umri wa miaka 116.
Siri yao kubwa ni kula chakula
chenye afya ikiwemo samaki
badala ya nyama nyekundu.
Hawanywi maziwa, au bidhaa
zozote za ng’ombe. Nafaka jamii ya
soya ambazo zinasaidia kuondoa
maradhi ya moyo.
Wanakunywa chai kwa wingi, hasa
ya kijani, wanakula kiasi kidogo cha
chakula, hawatumii magari mara
kwa mara na wanatumia vyoo vya
kuchuchumaa badala ya vya kukaa.
Matatizo ya kuumwa na magoti tiba yake ni dawa gani ?
ReplyDelete