Monday, 5 May 2014

PILIPILI HUIMARISHA UJASIRI NA NGUVU MWILINI!



Kama ilivyo kwa matunda na vyakula vingine kuwa na faida kiafya mwilini, pilipili nayo ni moja wapo. Licha ya kuogopwa na baadhi ya watu, lakini ina kiasi kingi cha vitamin C.

Umuhimu wa Vitamin C mwilini, 

humfanya mlaji awe imara na ndiyo maana wala pilipili siyo waoga, ni watu wenye kujiamini, hawaugui hovyo na huimarisha nguvu za mwili kwa ujumla.

Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo, pilipili ina asili ya Marekani. Wafanyabiashara wa Ulaya waliipeleka barani Asia ambako nako Waarabu katika pilikapilika za biashara ya utumwa wakajikuta wameileta Afrika Mashariki, ikiwemo Tanzania.
Aidha, pilipili 
inadaiwa kudhibiti uzito, ingawa haijathibitishwa rasmi kama inaweza kupunguza uzito wa mwili. Hata hivyo, pilipili ina faida lukuki za kiafya ambapo inajulikana kwa uwezo wake wa kudhibiti maumivu ya viungo na ugonjwa wa kisukari.
Utafiti 
uliowahi kufanywa nchini Marekani na Chama cha Watafiti wa Ugonjwa wa Saratani, umegundua kuwa upo uwezekano wa pilipili kuua na kutokomeza viini vya saratani ya uzazi na mapafu, endapo italiwa chini ya usimamizi na maelekezo ya daktari.
Ili kupata faida za pilipili 
kama zilivyoainishwa hapo juu, hakikisha mlo wako unakuwa na pilipili kwa kiwango utakachoweza kukimudu, na inapendekezwa pilipili iwe mbichi, na kama utaipika pamoja na kitoweo au mboga, hakikisha unatumia pilipili halisi na siyo ya kwenye makopo.
Hata hivyo, unaweza 
usiipate pilipili halisi kutokana na mazingira au usile kutokana na matatizo mbalimbali yakiwemo ya kiafya. Upo msaada wa tibalishe za ‘Go!’ ambazo zinaweza kufanya kazi mbadala wa pilipili. Zipo Go! za aina nne yaani, Man, Woman, Focus na Workout ambazo zipo madukani karibu nchi nzima.
Go! Man itakuongezea kinga 
ya kupambana na maradhi kwa mwaka mzima huku ikiboresha uhai wa moyo. Itafukuza maumivu ya mgongo, kiuno na miguu pia. Itakusafisha ubongo na kurejesha kumbukumbu na kuimarisha afya kwa ujumla.
‘Go! Woman’ 
itampa mwanamke vitu vyote hivyo ila imeongezwa vikorombwezo vitakavyomfanya mwanamke mrembo kwa kukarabati kucha zake, ngozi na nywele pia. Tibalishe ni msaada mkubwa wa kurekebisha afya zetu kwa sababu katika hali ya kawaida hatuwezi kukidhi mahitaji ya miili yetu kwa chakula pekee.
Tibalishe nyingi zipo madukani, 
iwapo utashindwa kuzipata tafadhali tuwasiliane tukusaidie kuzipata. Ila, kumbuka kula pilipili daima uwe THABITI.

Related Posts:

  • ZIJUE FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA Unaweza kuzidharau mbegu za maboga, lakini ni miongoni mwa mbegu zenye faida kubwa mwilini, zinazoweza kuzuia na kutibu hata magonjwa hatari yaliyoshindikana hospitalini. Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi uliok… Read More
  • JINSI YA KUTIBU UGONJWA WA PUMU (ASTHMA) JINSI YA KUTIBU UGONJWA WA PUMU Mahitaji:   Karafuu 6  Karafuu  Maandalizi: Zitowe vichwa vyake kisha loweka hizo karafuu katika nusu gilasi ya maji usiku kucha   Matumizi: &nbs… Read More
  • PILIPILI HUIMARISHA UJASIRI NA NGUVU MWILINI! Kama ilivyo kwa matunda na vyakula vingine kuwa na faida kiafya mwilini, pilipili nayo ni moja wapo. Licha ya kuogopwa na baadhi ya watu, lakini ina kiasi kingi cha vitamin C. Umuhimu wa Vitamin C mwilini,  … Read More
  • TIBA ASILIA YA TUMBO Watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na tumbo lisilo la vidonda wala ugonjwa wowote ila utasikia anakwambia tumbo linanikata, huenda akawa anavurugikwa na tumbo au imetokea linasumbua tu. Tiba hii hapa Kwanza k… Read More
  • KUONDOA CHUNUSI KWA KUTUMIA MANJANO Mahitaji  ya kuondoa chunusi kwa manjano - Vijiko viwili (2 tbs) vya unga wa binzari ya Manjano (Turmeric powder) - Kijiko kimoja (1 tbs) cha unga wa Riwa – wengine huita Liwa (Sandalwood) - Vijiko vinne… Read More

0 comments:

Post a Comment