Tuesday, 6 May 2014
NJIA ZA HARAKA ZA KUEPUKANA NA KUKABWA NA JINAMIZI
KUKABWA NA JINAMIZI NINI MAANAA YAKE?
Kukabwa na Jinamizi katika ndoto kama tunavyoita ni kitendo ambacho kinawatokea watu wengi sana.
Watu wengi hufikiri kwamba anayewakaba ni Jini lakini Tendo hilo kwa kitaalamu linajulikana kama “Mwili kupooza katika usingizi” (Sleeping Paralysis)
Tendo hilo huwa linakutokea katika muda wa sekunde 20 lakini wewe unayehusika utahisi kama dakika 5 au dakika 10.
Matukio hayo ya kijinamizi yanatofautiana na yanakutokea wakati ukiwa nusu usingizini na nusu macho.
Ukweli ni kwamba hayana madhara yoyote, ila yanakupa khofu kwa muda fulani.
Unapokabwa unakuwa na fahamu nusu. Unaweza kufungua macho, na utahisi kupiga kelele lakini watu hawakusikii, Mwili wako unakuwa hauwezi kufanya lolote na viungo vya mwili wako vinakuwa havifanyi kazi,
Inapokutokea unakuwa huwezi kunyanyua mguu wala mkono wala kichwa. Kwa ujumla unakuwa kama uliyepata “ugonjwa wa Kupooza”.
Hali hii ya kukabwa inapotokea unaweza ukamuona mtu anayetisha akiingia ndani chumbani kwako, wengine wanaona kama wanatekwa nyara au kuchukuliwa, wengine wanahisi wanabakwa, wengine wanaona wakipigwa au kukimbizwa na matukio mbali mbali ya kutisha.
Kukabwa na Jinamizi kama tunavyoiita kunatokana na sababu nyingi, ya kwanza kabisa ni jinsi wewe mwenyewe ulivyolala, mara nyingi unapolala chali mambo hayo yanakutokea, au ukiwa na jambo linalokusumbua kimaisha ambalo huwezi kulitatua linaweza kukuletea kukabwa na Jinamizi.
Sababu nyingine ni mazingira unayoishi au eneo ulilopo kama kuna makelele, au chumba kisicho na hewa ya kutosha au kuwa na mawazo kuhusu jambo fulani, au kulala na njaa au ukiwa umelala umekasirika au ndoto unazoota.
Njia ya kwanza ya kupambana na tatizo hili ni kujaribu sana lisikutokee, unatakiwa ujaribu kujua kitu gani kinakusababashia wewe kupata matatizo hayo, mfano ukijua kwamba kila ukilala chali unakabwa basi badilisha ulalaji wako, lala upande au lalia tumbo.
Ikiwa unakabwa ukiwa umelala usiku sana, au umefanya kazi ngumu, Jaribu kubadili muda wako wa kulala au punguza kufanya kazi mpaka ukachoka.
Njia nyingine ni kuhakikisha unapata muda mrefu wa kulala na umepunzika kabla ya usingizi haujakuja.
NJIA ZA HARAKA ZA KUEPUKANA NA KUKABWA NA JINAMIZI
1.Ikikutokea hali hiyo jaribu kuvuta pumzi nyingi ndani kwa sababu pumzi peke yake ndio unayoweza kuidhibiti ukiwa umekabwa.
2.Jiepushe kulala chali.
3.Punguza mawazo mengi.
4.Lala katika muda mzuri na jaribu kupata muda mrefu wa usingizi masaa 8 mpaka 10.
5.Jaribu kuwa na muda maalum wa kulala ikiwa ni saa 3 basi iwe muda huo wakati wote.
6.Jaribu kula vizuri kabla hujalala.
7.Kumbuka kwamba pamoja ya kuwa hali hii inatisha lakini haina hatari yoyote.
8.Ukihisi unakabwa jaribu sana kujitingisha, hali ya kukabwa itakwisha.
9.Ukiona kama unataka kukabwa amka kaa chini kwa dakika 5 halafu lala tena.
Related Posts:
MAGONJWA SUGU YASIYO YA KUAMBUKIZA ILI UJIEPUSHE NAYO-2 Shinikizo kubwa la damu Shinikizo kubwa la damu hutokea pale panapokuwa na ongezeko la nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa inayochukua damu kutoka kwenye moyo kwenda kwenye viungo na tishu mwilini. … Read More
IFAHAMU TOFAUTI YA UGONJWA WA KASWENDE NA KISONONO Ndugu msomaji nimeona ni muhimu kuandika tofauti ya ugonjwa wa kaswende na kisonono kwa sababu kumekuwa na idadi kubwa ya wagonjwa ambao wanapotoa maelezo au malalamiko yao wamekuwa wakichanganya ugonjwa wa kasw… Read More
MADHARA YA KIAFYA YASABABISHWAYO NA KUFANYA NGONO KINYUME NA MAUMBILE. Ngono kinyume na maumbile au wengine husema Ngono kwa nyia ya haja kubwa, ni hali ya kingono ambayo muhusika huingiza uume katika njia ya haja kubwa kwa lengo la kufanya mapenzi kwa njia hiyo ili kujirishiza hisia zak… Read More
SEHEMU YA PILI; MAGONJWA YA AKILI YA NGONO YANAYOSUMBUA WATANZANIA WENGI ( EXHIBITIONISM) Inaendelea toka makala sehemu ya kwanza nah ii ni sehemu ya pili endelea Kuwabaka wanyama Hili limeshawahi kuandikwa na vyombo kadhaa vya habari na kuwashangaza watu wengi duniani ikiwemo pia katika Tanzania. Zip… Read More
MAGONJWA SUGU YASIYO YA KUAMBUKIZA ILI UJIEPUSHE NAYO-3 Ugonjwa wa saratani Saratani ni ugonjwa unaotokana na seli za mwili zilizopoteza mfumo wake wa kugawanyika na hivyo hazipo katika hali yake ya kawaida. Seli huweza kugawanyika bila mpangilio maalum na kuha… Read More
mzizi mkavu mimi jambo hili linanisumbua sana, cha ajabu kwangu halichgui staili ya kulala, yani nikilalia tu itatokea, nikilalia ubavu itatokea, na chali vilevile,, alafu most inanitokea mchana, naweza nikakabwa hadi nikataja majina ya watu walio kalibu na wanasikia, na nikiamka wananiambia kwa uliota utaita jina fulani,,
ReplyDelete