NINI HASA CHANZO NA TIBA YA UGONJWA WA RHEUMATOID ARTHRITIS
Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}
Arthritis ni nini?
Ni ugonjwa unaofanya viungo vyako kukauka na kuwa vigumu kuvisongesha kwani ukifanya hivyo, utasikia uchungu. Hali iliyo kawaida na kujitokeza sana sana ile inavamia viungo (Osteoarthritis) na ile inaathiri mwili mzima na kuufanya uvimbe ama kuleta mwasho viungoni. Mara nyingi, ugonjwa huu huwa haujitokezi bayana hadi pale ambapo mtu hufikia miaka arobaini au zaidi.
Ni nini dalili za ugonjwa huu? (Osteoarthritis)
Maumivu ya viungo baada ya mtu kufanya mazoezi ama shughuli za kutumia nguvu
Ugumu kwenye mikono, magoti, nyonga ama mgongo baada ya mtu kukaa kwa muda bila kusonga
Viungo kuvimba na kuwa vidhaifu na vyororo
Viungo kugongana na kutoa sauti mtu anajaribu kutembeatembea
Ugumu kwenye mikono, magoti, nyonga ama mgongo baada ya mtu kukaa kwa muda bila kusonga
Viungo kuvimba na kuwa vidhaifu na vyororo
Viungo kugongana na kutoa sauti mtu anajaribu kutembeatembea
Rheumatoid Arthritis
Viungo vyenye maumivu makali vyenye kukauka
Viungo kuwa na joto, vyekundu na kuvimba
Mtu kuwa na joto
Kuhisi mchovu na mdhoofu
Kukosa hamu ya chakula
Viungo kuwa na joto, vyekundu na kuvimba
Mtu kuwa na joto
Kuhisi mchovu na mdhoofu
Kukosa hamu ya chakula
Hutibiwaje?
Muone daktari kisha akufanyie uchunguzi. Unaweza kupata matibabu ya kumaliza maumivu na kufanya mazoezi ya kufanya viungo viwe vyepesi.
DAWA YA TIBA MBADALA:
Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}.
Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja.
Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya asali kwa kijiko cha chai cha mdalasini. Kunywa asubuhi na jioni ili kuondoa maumivu.
Katika tafiti iliyofanyika hivi karibuni na chuo kikuu kimoja huko Copenhagen, madaktari waliwapa wagonjwa 200, {syrup} mchanganyiko wa kijiko kimoja *cha chai* cha asali na kimoja cha mdalasini kila asubuhi kabla ya kifungua kinywa. Asilimia 73% yao waliripoti nafuu kubwa ya maumivu yao na ongezeko katika kufanya shughuli kama kujongea na kutembea vyema.
0 comments:
Post a Comment