Monday, 5 May 2014

MWILI HUJITIBU WENYEWE, UPE VYAKULA SAHIHI TU!



NI ajabu lakini ndiyo ukweli wenyewe. Mwili wa binadamu hujitibu wenyewe iwapo unapewa virutubisho sahihi vinavyoweza kutengeneza kinga ya mwili na kutoa ulinzi stahiki.

Ni rahisi kulibaini hilo pale mtu anapopatwa na jeraha kwa kujiumiza sehemu ya mwili wake na jeraha kupona bila kutumia dawa yoyote, kama jeraha lilichuna ngozi linaziba lenyewe na kuacha alama tu. Hapo hapo, watu wenye ukosefu wa kinga imara mwilini jeraha alipatalo huweza kuchukua muda mrefu kupona.

Watu wenye kinga dhaifu ya mwili ni wale wenye afya mbovu ambao ama kwa makusudi au kwa kutokujua huujeruhi mwili kwa kula na kunywa vitu visivyo sahihi, kutofanya mazoezi ambayo husafisha damu na kuchangamsha ubongo na moyo.

Binadamu akijijua na kujijali afya basi hataumwa na akiumwa hataenda hospitali kwa sababu mwili utajitibu wenyewe tena kwa usahihi mkubwa na hata aendapo hospitali na kutumia dawa hupona haraka ndani ya muda mfupi. Hali hii huwezekana kwa sababu mwili huwa na virutubisho, vitamini, madini na tindikali za kutosha kutoa nguvu za mwili kujikinga (immune responses).

Aristotle ni miongoni mwa madaktari bingwa wa kale anayeheshimika sana katika medani ya tiba ambaye alizaliwa Stageira na aliishi Athens huko Ugiriki miaka ya (384-322BC), alipoulizwa kwa nini tiba za ubongo ni tata alijibu kuwa ubongo ndiyo unaohisi, kubaini na kutibu mwili wote na hata 

kuusemea kupitia mdomo, hivyo siyo rahisi ubongo kujitibu na kujisemea wenyewe, inawezekana mwisho wa dunia ukafika bila binadamu hajajua tiba ya ubongo.

Hii inaleta majibu kwa usahihi pale mgonjwa anapokutana na daktari na kutibiwa kwa maneno na akapona, au mgonjwa akasema vidonge havimsaidii na daktari akamchoma sindano yenye maji ya kuchanganyia dawa tu na akapona, au wapo pia walioripotiwa kufanya upasuaji hewa (fake surgery) na wakapona pia kwa imani tu.

Kitaalamu hii ni tiba (psychotherapy) japo haifanyi kazi mara zote lakini baadhi ya wagonjwa hupona kwa sababu tiba ipo kwenye hisia, fikra na imani ambazo huamsha seli za ubongo na kuamsha nguvu za uponyaji ambazo ndiyo tiba ya maradhi yote na hapo mwili huua vimelea vya kansa, virusi 

mbalimbali vikiwemo vya ukimwi, kuyeyusha na kutoa sumu za maradhi mwilini pamoja na kupambana na maambukizi mbalimbali!

Kama tunavyosema kila siku kwamba si rahisi kwa kila mtu wakati wote kuupatia mwili wake virutubisho sahihi vinavyohitajika mwilini kutokana na mazingira anayoishi binadamu. Hata hivyo, kuhakikisha unakula vyakula sahihi na kuupa mwili wako kinga imara ni jambo la lazima.

Kwa kulitambua hilo, makampuni mengi yameanzishwa duniani kutengeneza bidhaa mbalimbali za vyakula zenye lengo la kumrahisishia binadamu kupata virutubisho vitokanavyo na nafaka, matunda na mbogamboga.

Kuna bidhaa za vyakula zilizotengenezwa na kuwa kama unga au vidonge lakini ukivila unakuwa sawa na mtu aliyekula mboga za majani, matunda au nafaka zenye vitamini na madini yote yanayotakiwa mwilini.

Kwa kuwa makampuni ni mengi na bidhaa hizo ni nyingi pia, gazeti hili linaweza kukusaidia kukupa ushauri wa kupata bidhaa hizo na namna unavyoweza kuzitumia kujijengea kinga imara ya mwili, hasa kama hujaanza kuugua ugonjwa wowote.

Kwa wale wenye maradhi mbalimbali, nao watapewa ushauri wa kutumia bidhaa zinazoweza kuwapa nafuu haraka bila kuleta madhara mengine (side effects). Hivyo msomaji usisite kuwasiliana nasi kwa maswali na ushauri, kwani tunaamini uzima wako ndiyo uzima wetu pia na Uwazi pekee ndiyo linaloweza kukupa thamani ya pesa yako, kwani linaokoa maisha.

0 comments:

Post a Comment