WANAWAKE
hupenda sana kutumia marashi na vitu vingine kama sabuni zenye kemikali kwa ajili ya kujirembesha.
Baadhi yao vitu wanavyovitumia kujisafishia sehemu zao nyeti ni sabuni zenye kemikali, pafyumu yaani deodorant au kupaka mafuta bila kujua madhara yake.
Wanawake hao wanaotumia vitu hivyo wana hatari ya kupata magonjwa ya zinaa au ya kuambukiza.
Watafiti katika Chuo Kikuu cha California, Marekani wanasema sabuni ngumu au hata za maji, pafyumu (deodorant) zinaharibu tishu muhimu zilizomo ndani kabisa ya uke.
Uharibifu huo wa tishu ndani ya sehemu za siri humweka mhusika katika hatari ya kupata malengelenge, fangasi vitu ambavyo huweza kusababisha kupata Ukimwi ikiwa watajamiiana na watu wenye tatizo hilo.
Sabuni au dawa zinazouzwa
na wafanyabiashara zikitangaza kuboresha au kuondoa harufu kwenye sehemu hizo nyeti nazo zina madhara.
Sabuni au mafuta yenye kemikali huchubua ngozi laini ya uke na ni rahisi vimelea vya magonjwa kuenea kwa urahisi.
Michubuko hiyo ambayo si rahisi kuonekana kwa macho ndicho chanzo cha kuingia kwa maradhi ya kuambukiza.
Kutokana na hayo ni wazi kwamba hakuna haja ya kuweka kemikali, au pafyumu ukeni. Hizo sehemu zinahitaji kuoshwa vizuri kwa maji safi.
Kemikali
inapoingia eneo hilo inavuruga hali ya kawaida na asidi inayolinda sehemu hizo, ni vyema wanawake wakaelimishwa kuhusu matumizi ya bidhaa zinazoweka harufu nzuri katika sehemu zao za siri, kurudisha bikira au mafuta ya kulainisha uke.
Wanawake wanaofanya usafi sehemu zao hizo za siri kwa kutumia vitu visivyofaa huweza kupata saratani ya shingo ya uzazi.
Bidhaa zenye kemikali
ya ‘coal tar,’ ambazo mara nyingine huwekwa kwenye sabuni ama manukato na kutumiwa ukeni na wanawake huweza kuchochea saratani hiyo.
Upo ushahidi wa kutosha kuwa kutumia sabuni za kuogea za maji au ngumu katika sehemu za siri za ndani za mwanamke kunaharibu uwiano wa bakteria na kusababisha bakteria kuzalishwa kwa wingi na kumweka mwanamke katika hatari ya kuambukizwa maradhi ya zinaa ikiwemo kansa ya shingo ya kizazi kama nilivyoeleza hapo juu.
0 comments:
Post a Comment