Ni wakati wa matazimio mapya. Miongoni mwa
maazimio(resolutions) zinazoongoza ni pamoja na ile ya kuishi maisha yaliyo na
afya bora zaidi na
furaha. Afya na furaha ni mambo mawili makubwa sana katika
maisha yetu.Ukichunguza sana takribani kila kitu tunachokifanya ni katika
mpambano wa kimaisha wa kuwa na afya bora zaidi na kuwa na furaha.
Sote
tunakubaliana kwamba afya bora ndio kila kitu.Ukiwa tajiri kupindukia halafu
ukawa na afya mgogoro,ni wazi kwamba huwezi kuzifurahia hizo hela zako.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo unayoweza kuyafanya
ili kuwa na afya bora katika maisha,
.Lakini kabla sijaendelea mbele sana,naomba niweke
wazi kwamba afya bora haihusu kula vizuri na mazoezi peke yake bali pia fikra
chanya(positive
attitude). Kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba siku zote unakuwa
na mawazo chanya na pia kuwa karibu zaidi na watu wenye mawazo chanya.
1.Kunywa Maji kwa wingi-
Bila shaka unakumbuka msemo “Maji ni Uhai”.Hiyo ni
kweli kabisa.Maji ni uhai sio tu kwa mazingira yetu na dunia kwa ujumla bali
pia kwa afya au
miili yetu.Maji ni kitu muhimu sana kwa afya zetu.Asilimia 60%
ya miili yetu imetengenezwa au imesheheni maji. Maji yanahitajika kwa ajili ya
kuondoa takataka au vitu visivyofaa kutoka mwilini.Maji ndio hubeba virutubisho
na oxygen.
Kiasi cha
maji anachohitaji mtu kinategemea na mambo kadhaa kama vile unyevu(humidity) wa
mahali ulipo,shughuli zinazohusisha mwili anazozifanya mtu na
pia uzito wa
mwili.Pamoja na hayo,kwa wastani miili yetu inahitaji lita 2 na nusu mpaka 3 za
maji.Vyakula tunavyokula
huchangia kama asimilia 20% za maji katika miili
yetu.Kwa hiyo tunahitaji kunywa maji kiasi cha lita 2 mpaka lita 2.4 au glasi
8-9 za maji kwa siku.
Njia
rahisi ya kujua kama mwili wako una maji ya kutosha ni katika kuangalia mkojo.
Mkojo wako unatakiwa kutokuwa na rangi(colorless) au
kuwa wa njano kidogo.Kinyume
cha hapo ni ishara kwamba hauna maji ya kutosha mwilini.Njia nyingine kutambua
ni pamoja na kukaukwa na midomo(lips) na hata ulimi na pia kupata kiasi kiduchu
cha mkojo.
2.Pata Usingizi
wa Kutosha:
Unakumbuka tulipokuwa wadogo wazazi wetu
walisisitiza sana kwamba twende tukalale mapema ili tukue? Bila shaka walikuwa
wanajua kwamba usingizi ni sehemu muhimu sana katika afya. Ukiachilia mbali
faida za usingizi kwa ajili ya afya za akili/ubongo wetu,usingizi au mapumziko
ya kutosha ni muhimu kwa miili.Afya njema huenda sambamba na mapumziko.Ni
wakati wa kuupa mwili nafasi ya kujijenga,kujiongezea nguvu na muhimu zaidi
kuhakikisha kwamba tunakuwa na akili timamu. Pia ukosefu wa usingizi ni chanzo
cha kuzeeka mapema.
3.Fanya Mazoezi-
Hili linaweza kupita bila maelezo ya ziada.Mazoezi
ni muhimu sana kwa afya bora. Fanya mazoezi angalau mara tatu katika
wiki.Jipatie muda wa kutembea japo kwa dakika 30. Kama inawezekana nenda
Gym.Badala ya kupanda lifti pale kazini kwako au mitaani,tumia ngazi za
kawaida.Egesha gari lako mbali kidogo na unapokwenda ili upate nafasi ya
kutembea nk. Muhimu zaidi ni kuchagua aina ya mazoezi unayoipendelea. Mazoezi
hayatakiwi kuwa adhabu.
Faida za
mazoezi ni pamoja na kujiepusha na magonjwa mbalimbali,kupunguza unene(bila
shaka unajua kwamba unene kupindukia sio afya bali ni ugonjwa na sababu kubwa
ya maradhi mengine)
4.Kula Matunda
Kwa Wingi
-Matunda ni chanzo kizuri sana cha madini na
vitamins ambazo miili yetu inahitaji sana kwa ajili ya afya bora. Unajua kwamba
machungwa,kwa mfano, yana faida kubwa zaidi kiafya kuliko vidonge vya Vitamin C
unavyobugia kila leo? Aina mbalimbali za matunda ambayo yana virutubishi vingi
zaidi kiafya ni Parachichi(Avocado),apple,matikiti
maji(cantaloupe),Zabibu(Grapefruit),Kiwi,Guava,mapapai,machungwa, strawberries
nk.
5.Kula mboga za
majani
Kama ilivyo
kwa matunda,mboga za majani(vegetables) ni muhimu sana kwa afya zetu. Wataalamu
wa afya wanashauri kwamba tule aina 5 mpaka 9 za mboga za majani na
matunda.Jitahidi kupata angalau zaidi ya aina 5 za mboga za majani na matunda.
6.Punguza Kula
Vyakula vya Makopo
Kutokana na
jinsi dunia inavyozidi kwenda mbio,watu wengi huwa tunakosa muda wa kupika.Matokeo
yake tunakimbilia kwenye vyakula vya kwenye makopo ambavyo ndivyo vimejaa
katika maduka na ma-supermarket. Jitahidi kuviepuka vyakula hivyo kwa kadri
unavyoweza.Mara nyingi vyakula vya
makopo huwa na ingredients ambazo hazifai
kwa afya zetu.Kwa mfano,vingi miongoni mwa vyakula hivyo huwa na chumvi nyingi
kitu ambacho ni chanzo
cha High Blood Pressure na maradhi ya moyo. Unaposhindwa
kabisa kujizuia kununua vyakula hivyo vya makopo jaribu kuangalia ambavyo
havina sukari au chumvi.
7.Jipende
Kama nilivyodokeza
hapo mwanzo,afya bora huenda sambamba na afya ya akili/ubongo.Njia mojawapo ya
kupata afya hiyo ni pamoja na
kujipenda.Pengine unajiuliza,kuna mtu ambaye
hajipendi? Ukweli ni kwamba pengine ni kweli kwamba hakuna mtu ambaye
hajipendi.Tofauti inakuja pale mtu anapofanya vitu ambavyo ni kinyume kabisa na
mapenzi ya mwili.
Mfano,uvutaji sigara,unywaji pombe kupindukia,kutojisafisha mwili wako
kwa mfano kuoga,kupiga mswaki na pia kupumzika nk.Hizo zote ni tabia
ambazo
zinaweza kuonyesha jinsi ambavyo hujipendi au huupendi mwili wako.Kama
unaupenda utautumia vibaya au kuuharibu?
0 comments:
Post a Comment