Ngono
kinyume na maumbile au wengine husema Ngono kwa nyia ya haja kubwa, ni hali ya
kingono ambayo muhusika huingiza uume katika njia ya haja kubwa kwa lengo la
kufanya mapenzi kwa njia hiyo ili kujirishiza hisia zake.
Watu
ambao wanajishughulisha na kushiriki katika ngono ya nia hii ya kinyume na
maumbile wapo katika hatari kubwa ya kiafya, kwa sababu njia ya haja kubwa
inazungukwa na mishipa/neva nyingi sana zipo eneo hilo ambalo kazi zake si
maalumu kwa tengo la ngono kwa kuingiziwa kitu ambacho hakistahiri eneo hilo.
Ambapo
kwa utafiti uliofanyika Nchini Tanzania uliohusisha wasichana na wanawake wa
rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na iliyohusisha kada tofauti katika jamii
kama wanafuzi, wafanyakazi, wahudumu wa baa, wauguzi, makahaba na kina mama wa
majumbani katika maeneo tofauti. Watu waliojitokeza ni 903 wakiwemo pia wanaume
walihusika katika tafiti hiyo.
Utafiti
huo ulisema wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema kuwa wamewahi kufanya
tendo la kujamiiana kinyume na maumbile ambao ni sawa na asilimia 27 huku
asilimia 73 ya waliohojiwa walidai kufahamu njia hiyo ya kufanya mapenzi
kinyume na
maumbile, katika Utafiti huo ulifanywa na Irene Mremi kutoka Taasisi
ya utafiti wa magonjwa ya binadamu Nchini Tanzania.
Pia, Inakadiriwa
kuwa asilimia 90% ya wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao (mashoga) huwa
wanajihusisha na ngono kinyume na maumbile.
JE,
NGONO KINYUME NA MAUMBILE NI SALAMA?
HAPANA,
Ngono kinyume na maumbile si salama kwa sababu ina madhara mengi kiafya kama
yafuatavyo;
MOJA,
Njia ya haja kubwa haina vilainishi/lubrication asilia kama jinsi Uke ulivyo.
Hivyo
wakati wa tendo la ngono husasani wakati wa uingizaji wa uume huwa inasababisha
kuchubuka kwa tisu/ngozi laini ndani ya njia ya haja kubwa hiyo, na hivyo
kupelekea michubuko ambayo
bacteria, virusi na hata vimelea vingine kuweza
kupenya wakati wa majeraha hayo ya michubuko na hivyo kuingia katika mfumo wa damu
kupitia majeraha hayo.Hii inaweza kusababisha kuenea kwa
magonjwa ya zinaa
pamoja na VVU.
Tafiti
zinaonyesha ya kuwa Ngono kwa Njia ya
haja kubwa ipo katika hatari kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa zaidi
ya asilimia 30% kuliko watu wanaotumia njia ngono kwa njia ya Uke.
Vile
vile mtu anakuwa katika hatari kubwa ya kupata
virusi vya human papillomavirus (HPV ) ambavyo huweza kumpelekea mtu
anayejihusisha na ngono kinyume na maumbile kupata muwasho katika eneo hilo la
haja kubwa na hata kupelekea kupata kansa.
PILI,
Tishu ndani ya njia ya haja kubwa, haijakingwa na kulindwa kwa ngozi ngumu kama
ilivyo sehemu za nje za mwili. Tishu zote za nje ya miili yetu zina ngozi
ambayo ni seli zilizokufa ambazo hutusaidia kutukinga dhidi ya maabukizi ya
vimelea na vile vile hutulinda na vitu tofauti katika mazingira.
Hivyo
ndani ya njia ya haja kubwa hakujakingwa na ulizi huo wa asili wa seli hizo ili
kuweza kuhimili, hivyo kuifanya iwe katika hatari kubwa ya kusuguliwa na hivyo
kuchanika ambayo hupekea kusababisha maambukizi kuwa rahisi kutokea.
Pia
ngozi ndani ya njia ya haja kubwa iko tofauti na ile ya ukeni ambapo ngozi ya
ukeni huweza kuhimili ile misuguano pasipo kuweza kusababisha michumbuko kwa
sababu ya vilainishi asili vinavyoatikana ndian ya uke na gozi husika.
TATU,
Njia ya haya kubwa ni Maalumu kupitisha Kinyesi tu.
Kwa
jinsi ambavyo njia hii imeundwa ama kutengenezwa ni maalumu kwa kuhimili na
kupitisha kinyeshi tu na si vinginevyo.
Njia
ya haja kubwa imezungukwa na kama misuli mfano wa ringi ama kwa kitaalamu
huitwa (Anal sphincter) ambayo kazi yake
ni kukaza eneo hilo kabla na baada ya kujisaidia tu.
Kipindi
ambapo misuli hiyo (anal sphincter)imekazwa ama kubwa kwa kuingiziwa kitu
kingine kigumu huweza kusababisha maumivu makali kwa muhusika.
Panapoendelea
kuwa na mrudio wa mara kwa mara wa ufanyaji wa
Ngono kwa njia hii ya haja kubwa ama kinyume na maumbile hufanya misuli
hiyo ya njia ya haja kubwa kuwa dhaifu ama kulegea
na isiwe na uwezo tena
wakukaza kama kazi yake inavyotakiwa kufanya. Na hivyo kuwa vigumu kuweza
kuzuia kinyesi kuweza kupita mpaka utapokuwa tayari kuweza kukitoa hivyo
kusababisha utokaji ovyo wa kinyesi.
NNE,
Njia ya haja kubwa imejaa bacteria wengi.
Njia
ya haja kubwa imejaa bacteria wengi sana tofauti na Ukeni kulivyo hata kama
wapenzi hawana maambukizi yeyote ya zinaa au ugonjwa wowote bacteria huwa wapo
tu eneo hilo na hawa ni bacteria wa kawaida (Normal flora).
Mtu
anapokuwa naingiza uume ndani ya njia ya haja kuwa anakuwa anaingiza vimelea
vingine vya bacteria katika eneo hilo na wanapokutana na wale bacteria wengine
waliopo katika eneo hilo husababisha madhara.
Pia
pale unapohamisha uume toka katika njia ya haja kubwa na kupeleka katika Njia
ya Uke badi bacteria hao utawapeleka
katika eneo Uke ambapo Njia ya haja kubwa inakuwa na bacteria wengi na hivyo
kupelekea maambukizi ukeni na pia maambukizi katika njia mkojo.
Ngono
kwa njia ya haja kubwa inaweza kusababisha madhara mengine kwa afya ya watu
wanaojihusisha na Njia hii ya ngono na wanaweza kupata madhaara kama haya
yafuatayo,
Pale
mdomo unapogusana na njia ya haja kubwa au kugusa uume uliotoka kwenye njia ya
haja kuwa kwa mdomo kunaweza kupelekea kupata kwa wote mtu na mpenzi wake kuwa
katika hatari ya kupataa magonjwa ya HEPATITIS C, HERPES/ malengelenge, kupata
virusi vya human papillomavirus (HPV) na maambukizo mengine.
Hata
hivyo, majeraha makubwa wakati wa ngono kwa njia ya haja kubwa mara nyingine
ingawa sio kila mara hali hii kutokea inaweza kupelekea Damu kuvuja kwa ndani (hemorrhoids)
baada ya tendo
hilo kufanyika ambalo
inaweza kusababisha au kupasuka ama kuchanika kwa misuli/nyama ndani ya njia ya
haya kubwa kwa sababu ya msuguano mkali na muda mwingine hupelekea kuweza
kutoboka kwa utumbo mpana(colon) hii huweza kwa ni tukio la hatari zaidi ambalo
huhitaji msaada wa kitabibu haraka kwa matibabu na hata kufanyiwa upasuaji
zaidi na hata kupoteza maisha kunaweza kutokea.
TANO,
pia kwa wanawake wengi wanaofanya ngono kinyume na maumbile wamekuwa wakipata
shida wakati wa kujifungua kwa misuli yao kushindwa kuhimili kukaza kwakati wa
kusukuma mtoto
na hivyo inaweza kupelekea utokaji wa kinyesi wakati wa kusukuma
mtoto. jambo ambalo huleta tabu kwa wahudumu wa afya kwa kutumia muda mwigi
kuwahudumia.
Njia
pekee ya kuepuka kabisa hatari hizo za ngono kinyume na maumbile ni kuacha
kabisa ngono kwa njia hiyo ya haja
kubwa.
shiriki
katika ngono kwa njia ya kawaida na ikibidi kwa kutumia kondomu ili kujilinda dhidi
ya kuenea kwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
Kuepuka
kuingiza uume ndani ya uke na kisha mdomoni ikiwa uume ulikuwa umeingizwa katika
njia ya haja kubwa.
Ikiwa
umepata michubuko na kutoka damu baada ya ngono ama
vidonda karibia na njia ya
haja kubwa na hata katika maeneo ya uke basi onana na daktari wako haraka
iwezekanavyo ili upatiwe tiba hii iakusaidi kuzuia maambukizi ya vimelea katika
eneo la jeraha.
MADHARA
ANAYOWEZA KUYAPATA MWANAUME ANAYEPENDA KUJIHUSISHA NA MCHEZO HUU WA NGONO NI
KAMA IFUATAVYO;
KWANZA,
Kunauwezekano wa Njia ya haja ndogo kuziba kiasi au
kuziba kabisa kwa sababu ya
vimelea kuingia na kuziba ama kuingia kwa kinyesi katika njia ya haja ndogo
hivyo kukuweka katika wakati mgumu utapohitaji kujisaidia haja ndogo.
PILI,unaweza
kupata magonjwa ya saratani(kansa) ya tezi tezi Prostate gland
TATU,Maambukizi ya Virusi vya ukimwi kwa sababu kuna
uwezekano mkubwa sana wa kupata maabukizi tofauti na kwenye njia ya Uke hii ni
kutokana na kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata michubuko kiurahisi.
NNE,
Kuathirika kisaikolojia hivyo mhusika kuandamwa na msongo wa mawazo kila wakati
kujutia tendo hili baya.
Nina
imanai ndugu msomaji wa makala hii umeweza kuona madhara mabaya sana ya tabia
hii mbaya. Inawezekana umezoea mchezo huo wa kuwaingilia wenzako ama kuingiliwa
kwa namna hiyo na kuona raha lakini umeziona hasara zake, amabazo kwa
hakika kama wewe ni mmoja wao, unatakiwa
kuacha mara moja kwa vile mwisho wake ni majuto na mateso.
Jiepushe
mkuiga mambo bila kujua hasara zake, pia
usimtie mwenzako majaribu kwa kumlazimisha kufanya kitendo hiki na wanaume kwa
kigezo cha kuachwa kwa lengo la kuwaingilia
kinyume na maumbile kwa kuwatishia
kuwaacha kama watakataa.
Kipi
bora kuharibiwa ama kuachwa? Jibu unalo mhusika!!
Kumbuka
baada ya kuharibwa thamani yako inashuka mbele ya jamii. Kasha kupelekea kuingia
katika msongo wa mawazo na mateso ya ugonjwa ama magonjwa utakayoyapata baada
ya kukubali kuingiliwa kinyume na maumbile.
UKWELI
MCHEZO HUU UMEWAATHIRI SANA WANAWAKE AMBAO WENGI WANAUJUTIA.
JIEPUSHE
NA NGONO KINYUME NA MAUMBILE!!!!!
0 comments:
Post a Comment