Utafiti huo uliangalia faida za matunda chachu (Citrus Fruit)
pekee kwa
mara ya kwanza tofauti na tafiti nyingi ambazo tumezizoea
zinazoangalia umuhimu wa matunda na mboga za majani kwa afya kiujumla.
Utafiti
huu umehusisha maelfu ya wanawake wanaoshiriki katika tafiti ya manesi
Nurse’s Health Study lakini wataalamu wanaamini faida hizo za
machungwa na zabibu pia zinapatikana kwa wanaume.
Timu
ya watafiti katika chuo cha Norwich Medical School katika Chuo Kikuu
cha East Anglia wamechunguza umuhimu wa kemikali aina ya flavonoids ambayo ni jamii ya
antioxidant
(kemikali zinauwa kemikali hatari za kwenye mwili) inayopatikana
katika matunda, mboga za majani, chocolate nyeusi na wine nyekundu.
Utafiti
huu ulifuatilia takwimu za miaka 14 za wanawake 69,222 ambao walikuwa
wakishirki katika tafiti kwa kuandika kiwango chao cha kula matunda na
mboga za majani kwa kila kipindi cha miaka 4. Timu hiyo ya utafiti
iliangalia uhusiano wa aina sita ya flavonoids -
flavanones, anthocyanins, flavan-3-ols, flavonoid polymers, flavonols na flavones na hatari ya aina mbalimbali za kiharusi kama Ischaemic, Hemorrhagic na Total Stroke.
Ilionekna wanawake waliokula kiwango kikubwa cha flavanones
kwenye matunda chachu walikuwa na asilimia 19 ya uwezekano wa
kupunguza kiharusi kulinganisha na wanawake ambao walikula kiwango
kidogo cha matunda hayo.
Kiwango kikubwa cha flavanones kilikuwa 45mg kwa siku kulinganisha na kiwango kidogo cha 25mg kwa siku. Utafiti huu ulichapishwa katika jarida la Medical Journal Stroke umesema flavanones
hupatikana kwa asilimia 82 kwenye machungwa na juisi ya
machungwa na
hupatikana kwa asilimia 14 kwenye zabibu na juisi ya zabibu. Hata hivyo
watafiti hao wamesema kwa wale wenye kusudio la kuongeza kiwango
kikubwa cha flavanones itawalazimu kula tunda la chungwa kwa wingi na
si juisi za machungwa
zinazotengenezwa kiwandani kutokana na kiwango
kikubwa cha sukari kinachopatikana katika juisi hizo za viwandani.
Professa Aedin Cassidy wa masuala ya lishe bora (nutrition)
na ambaye alikuwa kiongozi wa utafiti huo amesema “kula kwa wingi kwa
matunda, mboga za majani, na hasa Vitamin C uhusishwa na kupunguza
uwezekano wa kupata kiharusi”. Flavanones
hutoa kinga dhidhi
ya kiharusi kutokana na kuongeza ufanisi wa mishipa
ya damu kwenye ubongo na kutokana na kuwa na uwezo wa kuzuia
maambukizi mwilini (Anti-inflammatory effect).
Utafiti
uliofanyika hapo awali ulionyesha ya kwamba ulaji wa matunda chachu na
juisi yake na si matunda ya aina nyingine yoyote hupunguza uwezekano
wa kupata kiharusi aina ya Ischaemic Stroke na kuvuja damu kwenye ubongo (Intracerebral Haemorrhage).
Utafiti
mwingine uliofanyika kipindi cha nyuma ulionyesha hakuna uhusiano
wowote wa matunda ya njano na machungwa katika kupunguza uwezekano wa
kupata kiharusi lakini ulionyesha ya kwamba kuna uhusiano wa zabibu na
mapeasi wa kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi.
Katika utafiti mwingine uliofanyika nchini Sweden umeonyesha ya kwamba wanawake ambao walikula kiwango kikubwa cha antioxidant
karibia asilimia 50 kutoka kwenye matunda na mboga za majani, ni
wachache tu kati yao waliopata kiharusi ikilinganishwa na wanawake ambao
walikuwa na kiwango kidogo cha antioxidant.
Matokeo
ya utafiti huu yasiwafanye watu kuacha kula matunda ya aina nyingine
pamoja na mboga za majani kwani nayo yana faida kubwa katika mwili wa
binadamu.
Kupunguza
uwezekano wa kupata kiharusi inawezekana kama mtu atakula lishe bora
iliyo na virutubisho vyote muhimu, kula matunda na mboga za majani kwa
wingi, kufanya mazoezi mara kwa mara, kupunguza kiwango cha ulaji chumvi
(kwani watu wenye asili ya
Kiafrika wana kiashiria cha asili
kinachojulikana kama salt retention gene ambacho hufanya
kiwango kidogo cha matumizi ya chumvi mwilini kuonekana kama kiwango
kikubwa na
hivyo kuongeza hatari ya kupata kiharusi), kupunguza uzito
(kuwa kwenye uzito unaotakikana kiafya kulingana na umri na urefu
wako), kupunguza kiwango cha matumizi ya mafuta katika chakula, kulala
masaa ya kutosha na kupunguza msongo wa mawazo.
0 comments:
Post a Comment