Thursday, 1 May 2014

MAAMBUKIZI YA VIRUSI HUMAN PAPILLOMA [HUMAN PAPILLOMA VIRUS(HPV)]


 

HPV ni Virus ambavyo husababisha maambukizi kwenye chembe-hai ya keratin(keratinocyte) za ngozi na utando telezi(mucous membrane). Asilimia kubwa ya maambukizi ya virusi hivi huwa havionyeshi yoyote, ila baadhi ya aina husababisha dutu/chujua(wart), ama kigwaru(genital wart) kwa HPV type 6 na 11. Pia, HPV wanaweza kusababisha saratani ya shingo ya kizazi(cervical cancer), uke, uume, mkundu na hata pia koo, hasa kwa HPV type 16 na 18.
 
MAAMBUKIZI
HPV huambukizwa kwa njia ya mgusano wa moja kwa moja wa ngozi kwa ngozi(direct skin-to-skin contact).
i) Kuna zaidi ya aina 30 hadi 40 ya virusi hivi huambukizwa kwa njia ya ngono na kusababisha vigwaru(genital warts), na hata kusababisha saratani ikitegemea na aina ya kirusi.
ii) Pia virusi hivi vinaweza kuambukizwa kutoka kwa mama kwenda kwa motto wanati wa kujifungua kama mama ana maambukizi haya kwenye via vya uzazi.
iii) Mikono pia inaweza kusaidia maambukizi endapo itakusa sehemu yenye maambukizi na kasha kugusa popote, hasa sehemu za siri.
iv) Kushirikiana baadhi ya vitu inaweza pia ikasababisha maambukizi endapo mmoja kati ya wanaoshilikiana atakuwa na maabukizi haya.
Maambukizi ya virusi hivi sehemu nyingine ya mwili si tatizo sana. Nitazungumzia maambukizi ya HPV sehemu za siri ambapo husababisha genital wart(Kigwaru).
 
GERNITAL WART (KIGWARU)
• Hii pia hujulikana kitaalam kama veneral wart, ama anogenital wart, ama anal wart ikitegemea na eneo.
• Husababishwa na HPV type 6 na type 11. Virusi hivi huambukizwa kwa njia ya mgusano kingono, iwe ni ngono ya mdomo, via vya uzazi ama ngono ya mkundu kutoka kwa mwenzi mwenye maambukizi.
• Japokuwa 90% ya wanaopata maambukizi hawapati genital warts, ila bado wanaweza kueneza virusi hivi. Pia, japokuwa HPV wanaosababisha saratani ya shingo ya kizazi ni tofauti na wasababishao vigwaru, upatapo vigwaru ina maana upo hatarini pia kupata HPV wasababishao saratani, ambao ni HPV type 16 na 18.

DALILI (pia tazama picha)
Kwa kuwa hakuna maumivu yoyote, dalili kuwa ni kuota vigwaru ambavyo vinaweza kuwa ni vidogo na kimoja kimoja, ama vikubwa na kukaa kwa makundi
Kwa mwanamke vinaweza kukaa nje ama ndani ya uke, kwenye shingo ya kizazi ama hata tumbo la uzazi. Pia vinaweza kukaa nje ama ndani ya mkundu.
Kwa mwanaume mara nyingi hukaa kwenye ncha ya uume, ila pia vinaweza kukaa kwenye mpini(shaft), korodani(scrotum) na maeneo ama ndani ya mkundu.
Pia kwa wote, vinaweza kukaa mdomoni ama kwenye koo kwa mtu aliyefanya ngono ya mdomo(oral sex) na mtu mwenye maambukizi.
Pamoja na dalili hizo, maambukizi yanaweza yasionyeshe dalili yoyote na mtu mwenye maambukizi akakaa nayo kwa muda wa hata miaka miwili. Katika kipindi chote hicho, mtu mwenye maambukizi anaweza kuambukiza wengine akikutana nao kimwili. Unapojamiiana na mtu mwenye maambukizi haya, kuna uwezekano wa 70% wa kupata maambukizi.
 
TABIA HATARISHI
• Kuanza kushiriki ngono katika umri mdogo
• Kuwa na wapenzi wengi

KUJIKINGA
Kuepuka kuanza kujamiiana katika umri mdogo
Kuepuka kuwa na wapenzi wengi
Kutumia kondom, japokuwa siyo msaada sana. Maana kondom huwa haikingi eneo lote la siri na kuwepo uwezekano wa kutokea maambukizi sehemu ambazo hazijakingwa.
Pia HPV ina chanjo ambayo humkinga aliyechanjwa dhidi ya aina zote ziletazo tatizo, ambazo ni HPV type 6 na 11 ambazo husababisha genital wart, na HPV type 16 na 18 ambazo husababisha saratani ya shingo ya kizazi(cervical cancer).
 
MATIBABU
Hakuna dawa inayoua moja kwa moja HPV, ila kuna njia ya kutibu vigwaru(warts) vionekanavyo na kupunguza uwezekano wa kuleta madhala zaidi, ama kuambukiza.
Ikitegemea na ukubwa pamoja na eneovilipo, daktari anaweza kuamua
i) Kutumia dawa ambayo itaviunguza na kuvitokomeza, ama
ii) Kuvikata kwa na kuvitoa
Ushauli, ukiona dalili yoyote ya maambukizi ya HPV, wahi sehemu za kutolea tiba na umweleze mtaalam tatizo lako ili lipatiwe ufumbuzi mapema kabla halijaleta madhala zaidi, na ushauli wa kitiba.

Related Posts:

  • SABABU ZA TATIZO LA KUTOPATA MIMBA - 3 Naendelea kuelezea mambo yanayosababisha mwanamke kutopata mimba. Endelea... Kipimo cha upevushaji wa mayai kupima mirija ya uzazi, upasuaji mdogo kwenye tumbo na kumulika ndani ya mwili wake pia kipimo cha Ultrasound kit… Read More
  • SABABU ZA TATIZO LA KUTOPATA MIMBA TATIZO la kutopata mimba linawasumbua wengi na huwapata wanawake kadhaa katika jamii, huweza kumpata mtu mmoja kati ya wanandoa 12 na ni tatizo linalowapata watu zaidi ya milioni 24 duniani kote. Uchunguzi uliofanyika n… Read More
  • MATATIZO YANAYOSABABISHA MWANAMKE ASISHIKE MIMBA MWANAMKE kutoshika mimba kumegawanyika katika makundi makubwa mawili. Kwanza ni hali iitwayo ‘primary Infertility’ ambapo mwanamke hana historia ya kupata ujauzito. Pili kuna hali iitwayo ‘Sekondari Infertility’, hapa m… Read More
  • NJIA YA KUPUNGUZA MAUMIVU WAKATI WA KUJIFUNGUWA MTOTO-3 Mpenzi msomaji, leo namaliza makala haya niliyoyaanza wiki tatu zilizopita. Ungana nami ili upate darasa kuhusu njia ya kupunguza maumivu wakati wa kujifungua... Katika Jarida la American Baby, mtaalamu mmoja aliwahi ku… Read More
  • SABABU ZA TATIZO LA KUTOPATA MIMBA - 2 Mpenzi msomaji, naendelea kuelezea sababu za mwanamke kutoweza kupata ujauzito. Tuwe pamoja...Wanaume wengi wanashindwa kumpa mimba mwanamke kutokana na kutumia dawa  hovyohovyo au kuwa na matatizo ya tezi za thyroid… Read More

0 comments:

Post a Comment