Sunday, 4 May 2014

MAAJABU YA KARAFUU (SYZYGIUM AROMATICUM) KUTIBU MAGONJWA MBALIMBALI.

 ​




Karafuu pamoja na Unga wa karafuu


Karafuu
ni tumba lililokauka la maua yasiyofunguka yanayopatikana kutoka mti mzuri wa kati na kijani. Mti huu una shina lilinyooka na hukua kufikia kimo cha mita 10 hadi 12.
Karafuu imekuwa ikitumiwa India na Uchina kwa zaidi ya kwa zaidi ya miaka 2000 kama kiungo cha kulinda kuoza meno na kutoa harufu mbaya yaaani pumzi mbaya.

Mti wa karafuu
una asili ya visiwa vya Molluca. Wachina walipata kiungo hiki mnamo karne ya 3 K.K (Kabla ya Kuzaliwa Kristo).

Karafuu ziliingizwa
Alexandria mapema mwaka 176 B.K (Baada ya Kuzaliwa Kristo). Mnamo karne ya 4 hivi B.K ulijulikana vema katika meditarrania na katika karne ya 8 ulaya nzima.

Inasemekana huko 
 visiwa vya pemba na unguja (Zanzibar) karafuu ililetwa na sultani mmoja ikiwa imewekwa kwenye fimbo ya mwanzi leo hii Zanzibar ndio mzalishaji anayeongoza kwa kuzalisha karafuu nyingi ulimwenguni.

Sifa ilizonazo karafuu
ni wanga (carbohydrates), Protini, mafuta (Volatile oil), nyuzinyuzi (crude fibre), jivu la hydrochloric acid, calcium, phosphorus, iron, sodium,

Potassium, thiamine (Vit B1), Riboflavin (Vit B2), Niacin (Vitamin B3), vitamin A na C.
Mafuta hupatikana kwenye vitumba vya karafuu, kikonyo na majani.
Karafuu hutibu magonjwa mengi kama kutuliza maumivu ya meno, kutoa gesi tumboni, kuchafuliwa moyo, kuyeyusha chakula tumboni, kuimarisha viungo vya kiume (Sex Stimulant), kuimarisha mzunguko wa damu mwilini, kuzuia kutapika,

Kipindupindu, kikohozi, Asthma, Masikio, maumivu ya Misuli (Muscular Cramps), kuumwa kichwa, styes (an inflammation around the eyelash)
.

Matumizi mengine
ya karafuu huchanganywa kwenye curry powder, pilipili, mdalasini,

Binzari na viungo vingine. Wahindi hutumia kuongeza ladha kwenye betel quid (pan pati). Mafuta ya Karafuu pia hutumika katika viwanda ya perfume, sabuni, ni kuongeza ladha kwenye madawa n.k

Tunashauri kila familia kuzingatia matumizi ya karafuu ili kulinda afya zetu.

Maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea),
 kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto,

Vidonda vya tumbo,
kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

0 comments:

Post a Comment