Friday 9 May 2014

FAHAMU UGONJWA WA HERNIA



Kuna magonjwa ya hernia 
ya aina nyingi kama zile ziitwazo kitaalamu inguinal, umbilical, femoral, epigastric, incisional, inguinal hernia  na diaphragmatic hernia.
Lakini watu wengi hukumbwa na hernia iitwayo inguinal hernia ambayo hutokeza karibu kabisa na sehemu ya siri ambako hapa kimrija kinachochukua mbegu za kiume kutoka kwenye korodani na kuingia kwenye tumbo na kuingia kwenye kiungo cha kiume.
Hapa panaweza kuwa 
na uwazi na uwazi huo ukaingia utumbo mdogo na kusababisha hernia hii. Aina hii ya hernia kama nilivyosema hapo juu ndiyo inayosumbua sana watu wengi duniani.
Kuna aina nyingine ya hernia inayoweza kutokea kwenye kitovu, sehemu ambayo kunakuwa na mshipa unaopitisha damu yenye chakula na hewa safi ya oksijeni kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto akiwa tumboni.
Sehemu hiyo mtoto anapozaliwa panaweza pasijifunge vizuri, hivyo mtoto huyo kupata hernia hii baadaye kwani utumbo mdogo huingia katika kijinafasi hicho kisichojifunga vizuri, hivyo kusababisha uvimbe wa hernia hii.
Lakini tatizo hili ikiwa mtoto amezaliwa na akaishi zaidi ya miaka miwili bila kujitokeza tena, basi atakuwa salama kwa sababu kwa muda huo sehemu hiyo huwa imejifunga kabisa.
TIBA
Ikitokea sehemu hiyo ikaacha kujifunga kwa kipindi hicho cha miaka miwili, basi daktari huamua kumfanyia upasuaji mtoto huyo.
Kwa watu wazima hernia 
kwenye kitovu ambayo kitaalamu huitwa umbilical hernia inaweza ikatokea kwa akina mama wenye mimba au kwa wale ambao ni wanene kupita kiasi kwani presha kwenye tumbo inakuwa kubwa na kufunga sehemu hii ya kitovu ambayo inawezekana awali ilikuwa wazi.
Hernia nyingine huweza kutokea kwenye kiungo cha njia ya kumezea chakula kinapoungana na tumbo. Kama sehemu hii haikufunga vizuri utumbo unaingia kwenye kinafasi hicho na kujitokeza kwenye kimfuko kilichopo kifuani kinachoitwa kitaalamu diaphragm.
Ndiyo maana hernia hii huitwa diaphragm hernia.
Hernia nyingine iitwayo femoral hernia hutokea pale mishipa ya damu iendayo kwenye mguu inapopita kwenye tumbo na ikiwa kwenye maungio pana nafasi basi hernia hii hutokea kwenye paja karibu na kiunoni.
Kuna hernia ingine
inayotokea kwenye chembe ya moyo ambapo misuli inaachia na kusababisha kingozi cha tumbo na utumbo kuingia katika sehemu hiyo hivyo kuvimba na kusababisha hernia.
Tiba za uhakika za hernia ni kufanyiwa upasuaji kama tulivyofafanua hapo juu.

0 comments:

Post a Comment