Saturday 10 May 2014

KULA MATUNDA MBALIMBALI KWA FAIDA ZAIDI KIAFYA YAKO



Uchunguzi mpya umeonyesha kwamba watu wanaweza kukabiliana kirahisi na magonjwa mbalimbali kwa kula matunda ya aina mbalimbali na mboga mboga badala ya kuongeza idadi ya matunda na mboga mboga hizo.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo uliotolewa katika Kongamano la Majaribio ya Kibiolojia huko Anahein California, baadhi ya matunda na mboga mboga yana faida kubwa ya lishe kuliko mengineyo.


Uchunguzi huo umeeleza kwamba,ingawa karoti inaaminiwa kuwa ni chanzo kikubwa cha beta-carotene lakini kula viazi vitamu badala ya karoti kunaweza kuupatia mwili beta-carotene mara dufu kuliko karoti.

Papai nalo lina beta-cryptoxanthin mara 15 zaidi ya machungwa. Halikadhalika mboga aina ya Kale huupatia mwili mada ya lutein/zeaxanthin mara tatu zaidi ya spinachi.

Pia imeelezwa kuwa stroberi na rasberi zina ellagic asid mara tatu zaidi huku kikombe kimoja cha maji yanayotokana na mmea uotao majini wa watercress ikiwa na mada ya isothiocyanate sawa na inayopatikana katika vijiko vine vya chai vya haradali au mustard.

Bi. Keith Rabdolph aliyeongeza uchunguzi huo anashauri kwamba, watu wajitahidi kujua umuhimu wa vyakula wanavyokula na kujua pia ubora na faida za matunda na mboga mboga wanazokula kwa afya ya miili yao.

0 comments:

Post a Comment