Ni vipi naweza kujilinda mimi mwenyewe na familia yangu dhidi ya kifafa?
·
Njia moja muhimu ya
kuwalinda watoto dhidi ya hatari ya kifafa ni kuhakikisha ya kwamba wanapata
chanjo zao kwa wakati unaofaa. BCG kwa mfano humlinda dhidi ya
kifua kikuu. Ugonjwa wa kifua kikuu umekuwa ugonjwa wa kawaida hivi leo na
unapoathiri mtoto mdogo ambaye hajapata chanjo, hatari ya kupata ugonjwa homa
ya uti wa mgongo (meningitis) huongezeka.
Homa ya uti wa mgongo itamweka mtoto kwenye hatari kubwa ya kupata kifafa.
Chanjo zingine maalumu kwa aina tofauti za homa ya uti wa mgongo
zinapatikana hospitalini lakini kwa ada.
·
Homa ni kitu
kinachoongezea hatari ya kupatwa na mshtuko ilhali inaweza kudhibitiwa
vyema. Mtoto ambaye homa yake inaruhusiwa
kupanda juu yuko katika hatari
ya kupatwa na mshtuko. Ni muhimu kwa homa kudhibitiwa vizuri pindi tu
inapoanza. Udhibiiti wa homa unajumuisha; kutumia dawa kama Panado (paracetamol) ama Brufen(Ibuprofen), mtoe mtoto nguo kisha
umpanguze na kitambaa kilicholoweshwa ndani ya maji yenye joto la kadri
na la muhimu zaidi ni kutafuta msaada wa matibabu.
·
Ulinzi dhidi ya jeraha,
haswa jeraha kwenye kichwa ambayo ndiyo sababu nyingine ya kifafa. Ulinzi
hutokana na kuhakikisha ya
kwamba watoto hawezi kuanguka kwa urahisi kutoka
katika sehemu iliyo juu, usimamizi unaofaa wanapocheza na kuweka mbali vitu
ambavyo vinaweza kuwaletea madhara wanapocheza. Unaposafiri kwenye gari, ni
muhimu kutumia mishipi ya usalama ili kupunguza hatari ya kujeruhiwa ikiwa
kutatokea ajali. Jeraha la kichwa ndilo jeraha ambalo hutokea mara kwa mara
kukitokea ajali.
Ni wapi naweza kuenda ikiwa sitapata usaidizi?
·
Kuzirai ambako hakuwezi
kudhibitiwa kunaweza kuwa hatari kwa mgonjwa.Huwa hakuwezi kubashiriwa na unaweza
kufanyika wakati mgonjwa yuko karibu na moto, anaendesha gari ana jaribu kuvuka
barabara, anaogelea ama anafanya kazi akiwa juu (k.m juu ya paa la nyumba).
Katika hali hii, kuzirai kutamweka mtu katika hatari kubwa kwani anaweza
kuchomeka, kupatwa na ajali, kuzama ama kuanguka na kuumia. Hii ni sababu moja
muhimu ambayo inahitaji kifafa kudhibitiwa.
·
Pili, ugonjwa wa kifafa
unaweza kutokea mara kwa mara ukiwa hautadhibitiwa. Kuzimia kunaweza kutokea
mara kwa mara na kuonekana ni kama unaendelea. Hii ni dharura ya kimatibabu
ambayo inaweza kusababisha kifo katika mda mfupi. Kwa hivyo ikiwa mgonjwa
ataathiriwa na kifafa kwa zaidi ya dakika 5, mpeleke katika hospitali iliyo
karibu haraka iwezekanavyo kwa sababu kuzimia hakuwezi kuisha bila ya dawa
Nitapata usaidizi wapi?
·
Hospitali iliyo karibu
nawe itakutolea usaidizi. Watakuwa na dakitari ambaye atakuchunguza na
atakushauri kuhusu uchunguzi wowote ama matibabu ambayo unaweza kuhitaji
kutumia.
Tambua uwongo unaozungumziwa kuhusu Kifafa
“Kifafa
ni aina ya ulemavu kwani huathiri utenda kazi wa ubongo”
·
Ulemavu ulielezewa
vizuri na Shirika la Afya Duniani mnamo mwaka wa 1976. Unatofautisha dhana tatu
ambazo hutumiwa sana na unadhihirisha baina ya kudhoofika, ulemavu na upungufu.
·
Kudhoofika ni
upungufu wowote ama hali ya akili isiyo ya kawaida (saikolojia), utenda kazi wa
mwili (fiziolojia) ama muundo wa mwili wa binadamu (anatomia) ama utenda kazi; Ulemavu ni kikwazo ama kukosa uwezo
(unaotokana na upungufu) wa kufanya shughuli kwa njia inayochukuliwa kuwa ya
kawaida kwa
binadamu; Upungufu ni kasoro inayotokea kwa mtu kwa
sababu ya kudhoofika ama ulemavu ambao huzuia kutimilika kwa wajibu
unaochukuliwa kuwa wa kawaida (kwa kutegemea umri, jinsia na mambo ya
ushirikiano wa jamii na utamaduni) kwa mtu huyo.
·
Kifafa ni matokeo ya
utenda kazi wa ubongo usio wa kawaida ama kudhoofika kwa utenda kazi wa
ubongo.Huathiri utenda kazi wa ubongo kwa kuendelea na kuwacha. Kuna hali
zingine ambazo huwa na athari inayoendelea na ya mda mrefu. Hizi hali hutokea
kama kutoona vizuri, kutowiiana vizuri,kuongea pole pole,kutoweza kumakinika na
kusahausahau. Hali hizi huitwa ulemavu ama taahira ya akili.
·
Ugonjwa wa kifafa
unaweza kumshika mtu mwenye hali/ulemavu mwingine. Unaweza pia kutokea tu
wenyewe. Mgonjwa wa kifafa ambaye yuko chini ya matibabu na anafuatiliwa mara
kwa mara anaweza kutimiza majukumu yake kama mtu yeyote mwingine.
Katika hali
hii hadhaniwi kuwa na ulemavu wowote. Ikiwa kuzirai kunakosababishwa na kifafa
kumeongezeka na kunamzuia mtu kufanya kazi yake ya kawaida, basi hili
huchukuliwa kuwa ulemavu.
“Kifafa hutokea kwa sababu ya kupagawa na mapepo”
0 comments:
Post a Comment