Tuesday, 27 May 2014

FAIDA ZA KULA NDIZI MBIVU KIAFYA YAKO

  Ndizi ni aina ya tunda linalopendwa na watu wengi yawezekana huwa unakula tunda hili bila kujua faida zake, lakini pia yawezekana wewe hupendi kabisa kula ndizi mbivu, lakini ni vyema kufahamu kuwa tunda hili ni muhimu sana kwa afya yako inasaidia kama wewe hujapatwa na vidonda vya tumbo, kwa kula ndizi mara kwa mara unajipa kinga madhubuti na kama tayari umeathirika na vidonda, kwa kula ndizi utajipa ahueni kubwa.

Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi kuhusu tunda hili, ndizi ni chanzo kikubwa cha madini aina ya ‘Potassium’, ambayo ni muhimu sana katika kuweka shinikizo la damu mwilini katika hali yake ya kawaida (Normal Blood Pressure), na huboresha utendajikazi mzuri wa moyo. Ndizi moja tu kwa siku inaweza kukukinga na maradhi ya shinikizo la damu na matatizo ya moyo.

0 comments:

Post a Comment