Thursday 1 May 2014

FAIDA YA KUTUMIA MAFUTA YA ZAITUNI KAMA DAWA

Mafuta  Ya  Mzeituni.
Mafuta  ya  Mzeituni  (  Olive  Oil  )  yana  faida  nyingi  sana  kwenye  afya  ya  mwanadamu. Zifuatazo  ni  baadhi  ya  faida  za   mafuta  ya  mzeituni.




                                                    Tunda  la  Mzeituni.

1.   Ni  tiba  nzuri  sana  ya  vidonda, mabaka  na  makovu  ya  mwilini.
1.               Yanaweza  kutumika  kwa  kulainisha  ngozi.
2.               Yanasaidia  kutibu   tatizo  la  mzio   wa  ngozi.
3.               Yana  kiasi  kikubwa  cha  Vitamin  A,D,E na  K  ambazo  zinasaidia   kuondoa  sumu  ya  kwenye  ngozi.
4.              Matumizi  ya  mafuta  ya  mzeituni  yataifanya  ngozi  yako  iendelee  kuonekana  changa  na  yenye  afya  wakati  wote.
5.              Matumizi  ya  mafuta  ya  mzeituni  yanasaidia  kutibu  matatizo  na  magonjwa  yote  ya  ngozi.
6.              Vilevile  matumizi  ya  mafuta  ya  mzeituni  kama  chakula  yanasaidia  kuimarisha  na  kurutubisha  afya  ya   mtumiaji.
7.              Matumizi  ya  mafuta  ya  mzeituni  kama  chakula  yanasaidia  kupunguza  uzito  kwa  watu  wenye  matatizo  ya  uzito  mkubwa.
Mafuta ya zaituni yana manufaa mengi katika mwili na maisha ya binadamu kwa ujumla kama ifuatavyo;


(1)Mafuta ya zaituni hutibu maumivu ya tumbo kwa kunywa kijiko 1 mara 2 kwa siku
kwa muda wa siku 7 hadi siku 11 inshaallah utapona kabisa.



(2)Mafuta ya zaituni hutibu masheitani kwa kusomea kisomo cha Ruqia, mgonjwa atajipaka mwili mzima mara moja kwa siku pamoja na kutafuna vitunguu saumu punje tatu wakati wa kulala kwa muda wa siku arobaini inshaallah.


(3)Mafuta ya zaituni ni kinga ya masheitani wa kijini na wa kibinadamu kwa kujipaka mwili mzima mara moja kwa siku.


(4)Mafuta ya zaituni hutibu ugonjwa wa mafua kwa kupaka kwenye mwamba wa pua na ndani ya matundu ya pua mara tatu kwa siku.


(5)Tiba ya vidonda vya tumbo; Matumizi ni kutia vijiko 2 vya chakula katika uji mara mbili kwa siku kwa muda wa siku 90.


(6) Mafuta ya zaituni hutumika kama huduma ya kwanza kwa aliyekunywa sumu kwa kunywa, na kwa mwenye ganzi au kiharusi hutumia kwa kuchua mwilini asubuhi na jioni.


(7) Mafuta ya zaituni hutumika katika kuua wadudu wabaya walioko tumboni kwanjia ya kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku kwa muda wa siku saba.


(8) Mafuta ya zaituni huongeza nguvu za kiume kwa kunywa kijiko kimoja kwa siku pamoja na kuuchua uume mafuta yaliyochanganywa na vitunguu swaumu kwa muda wa siku saba hadi kumi na moja.


(9) Tiba ya ugonjwa wa kusahau: paka katika paji la uso kutwa marambili pamojana kunywa kijiko kimoja cha chai mara moja kwa siku kwa muda wa siku 7 hadi siku 11.


(10) Tiba ya degedege: hutumika kupakaa mwili mzima mafuta yaliosomewa ruqya, marambili kwa siku kwa muda wa siku 7 hadi siku 21.


(11)Kukojoa kitandani: kupakaa mafuta ya zaitun mwili mzima kutwa marambili huku akilamba matone mawili kwa muda wa siku 7 hadi siku 21.

MAFUTA  YA  MZEITUNI  YANAPATIKANA   KWENYE  MADUKA  YA  MADAWA  (PHARAMCY), VITUO  VYA  AFYA  NA   SUPERMARKETS.

2 comments:

  1. je naskia mafuta ya zaituni huweza kusaidia kuongeza kubwa wa uume hii ni kwel au ni story za mtaani

    ReplyDelete