Tunda la Mzambarau : Majani ya Mzambarau ni dawa ya asili inayo saidia kuzuia kutoka kwa mimba.
Tatizo
la mimba kuharibika na kutoka (kuchoropoka) kabla ya umri wake
unaotakiwa kukamilika, limekuwa likiwasumbua wanawake wengi.
MISCARRIAGE NI NINI ?
Kwa
kawaida, ili mtoto azaliwe, ni lazima mwanamke afanye tendo la ndoa
akiwa katika siku zake za kupata ujauzito ambapo mimba hutungwa. Baada
ya mimba kutungwa, mtoto hukaa tumboni kwa muda wa miezi tisa ambapo
hupitia hatua mbalimbali za mabadiliko hadi kuwa binadamu aliyekamilika. Inapotokea
kuwa kitoto kimetoka tumboni kwa namna yoyote ile, kikiwa na umri wa
chini ya miezi mitano (wiki ishirini), tatizo hilo huitwa Miscarriage. Katika
hali hii, kitoto kinakuwa hakijakamilika na hakiwezi kujitegemea
chenyewe kwa mahitaji muhimu kama kupumua, jambo ambalo husababisha
kifo.
NB: Mtoto akitoka akiwa ameshapita umri wa miezi mitano, tatizo hilo huitwa Pre-mature birth (kuzaa njiti).
NINI HUSABABISHA MISCARRIAGE? Zipo sababu nyingi zinazosababisha ujauzito uchoropoke.
Matatizo ya Vinasaba (Genetic Factors) Hitilafu
katika Kromosomu (Chromosomal abnormalities) ambayo husababisha
vinasaba kuwa katika hali isiyo ya kawaida, inatajwa kuwa sababu kubwa
zaidi inayosababisha ujauzito uchoropoke ukiwa na umri wa chini ya wiki
13. Matatizo haya husababisha damu ya mama ishindwe kuendana na ya
mtoto na kusababisha reactions ambazo humdhuru mtoto na kumfanya
ashindwe kuhimili hali ya tumboni kwa mama. Hivyo ujauzito kuharibika.
2. Upungufu wa Homoni (Progesterone Deficiency) Homoni
ya Progesterone hufanya kazi kubwa kuanzia mimba inapotungwa mpaka
mtoto anapozaliwa. Progesterone ndiyo huchochea uimara wa ukuta wa
Placenta ambao mtoto hujishikiza. Upungufu wa homoni hii husababisha
ukuta wa mji wa mimba kushindwa.
3. Umri Mkubwa
Kwa
kawaida, mwanamke anapofikisha umri wa miaka 35 au zaidi, misuli
(sphincters) ya mji wake wa uzazi hulegea na kupungua nguvu za kuweza
kuhimili na kutunza kiumbe kinachokuwa ndani ya mji wa uzazi. Kulegea
kwa misuli hii husababisha mimba kuchoropoka kwa urahisi.
4. Magonjwa
Wanawake
wanaosumbuliwa na magonjwa kama kisukari, unene kupindukia (obesity),
Polycystic Ovary Syndrome, malaria kali, magonjwa ya zinaa na mengineyo
huwa katika hatari kubwa ya mimba zao kutoka.
5. Hitilafu Katika Kizazi
Baadhi
ya wanawake huwa na mfuko wa mimba (uterus) ambao muundo wake siyo wa
kawaida (T- Shaped Uterus). Wanawake wenye tatizo hili, huwa na hatari
kubwa ya mimba zao kuharibika kabla ya kutimiza umri wa miezi tisa.
6. Maambukizi ya bakteria au fangasi
Maambukizi
ya bakteria au fangasi husababisha misuli ya kizazi kushambuliwa na
kisha kupoteza uwezo wake wa kuhifadhi ujauzito, jambo ambalo
husababisha mimba kuchoropoka.
Sababu nyingine ni pamoja matumizi ya pombe kali, uvutaji sigara, matumizi ya dawa za kulevya, kemikali, matatizo ya kurithi n.k
DALILI ZA MIMBA KUCHOROPOKA (Symptoms of a miscarriage):
1. Kutokwa na damu sehemu za siri
Dalili
kubwa za miscarriage ni mama mjamzito kutokwa na damu (nzito au
nyepesi) sehemu za siri kwa vipindi au mfululizo. Damu hizi hutoka kama
zile zitokazo mwanamke anapokuwa kwenye siku zake na huambatana na
maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu.
2. Maumivu makali ya viungo
Dalili
nyingine za mimba inayotaka kuchoropoka ni maumivu makali ya mgongo,
kiuno, nyonga na tumbo chini ya kitovu. Maumivu haya huanza taratibu
lakini huongezeka kadiri muda unavyozidi kusonga mbele. Pia huambatana
na kutokwa na damu kama ilivyoelewa hapo juu.
3. Kutokwa na uchafu sehemu za siri
Dalili
nyingine kubwa ya Miscarriage ni mama mjamzito kuanza kutokwa na uchafu
wenye rangi sambamba na mabonge ya damu sehemu za siri.
ANGALIZO:
Dalili hizi pekee hazitoshi kuashiria kuwa tayari ujauzito umeharibika
ila mama mjamzito anapoona moja kati ya dalili hizi au zote, anashauriwa
kuwahi hospitali kuonana na daktari haraka iwezekanavyo.
Endapo
mama atachelewa, atakuwa anajisababishia matatizo zaidi kwani sumu za
kiumbe kilichoharibika huharibu mfuko wa uzazi na kusababisha matatizo
makubwa siku za mbeleni ikiwemo ugumba.
TIBA ASILIA KUZUIA TATIZO LA KUCHOROPOKA KWA MIMBA.
Zipo tiba za aina mbalimbali zinazo tibu tatizo la kuzuia kuchoropoka kwa mimba. Miongoni mwa tiba hizo ni hii ifuatayo :
MAHITAJI :
i. Majani ya Mzambarau
ii. Maji safi na salama kiasi cha lita moja.
MATAYARISHO NA MATUMIZI :
Chemsha majani machanga ya mzambarau kwenye lita moja ya maji mpaka yatakapo anza kutoa supu.
MATUMIZI :
Kunywa ujazo wa robo glas 1 mara 2 kwa siku asubuhi na jioni kwa muda wa siku ishirini na moja.
|
0 comments:
Post a Comment