Tuesday 20 May 2014

BRAIN CANCER UGONJWA WA SARATANI KANSA YA UBONGO



Kupambana na ugonjwa huu ni vigumu na unatisha.Kuna aina nyingi ya saratani jambo linalofanya kuwa gumu kukabiliana nao.

Saratani ya ubongo 

Ubongo ni mojawapo ya kiungo kitovu cha mtandao wa mishipa ya kusafirisha damu mwilini.Ubongo na uti wa mgongo huweza kuwa na uvimbe wa saratani ingawa ni nadra sana, ugonjwa huu ni hatari sana ikiwa hautatibiwa mapema.


Kisababishacho saratani ya ubongo haijulikani, lakini kuna mambo mengi yanayoweza kusababisha ugonjwa huu:
  • Ukiwa na saratani katika sehemu zengine za mwili huweza kusambaa hadi katika ubongo
  • Kufanya kazi katika kampuni za kusafisha mafuta, bidhaa za mipira , zinazotengeza madawa.

Dalili
Uvimbe unaweza kujitokeza katika sehemu yoyote ya ubongo,kwa hivyo dalili zitatofautiana.


Sehemu ya mbele (frontal)
  • Kuumwa na kichwa
  • Ulegevu mwilini
  • Kufa ganzi sehemu moja ya mwili
  • Mabadiliko ya haraka mwilini,hisia ,moyo na tabia
  • Kuchanganyikiwa na akili

Sehemu sawia (parietal)
  • Kuumwa na kichwa
  • Kushikwa na kifafa
  • Kufa ganzi
  • Shida unapoandika hati
  • Shida unapojaribu kusonga kwa namna Fulani
  • Shida kufanya hesabu rahisi

Sehemu ya nyuma (occipital)
  • Kuumwa na kichwa
  • Kushindwa kuona vizuri
  • Kuona mazingaumbwe yako tu
  • Kushikwa na kifafa

Kwa muda mfupi (temporal)
  • Kuumwa na kichwa
  • Kushikwa na kifafa
  • Shida ya kufuata maagizo kwa pamoja
  • Kutong’amua usumbufu wa hali ya anga.
Uvimbe katika mtandao wa mishipa huweza kumfanya mtu ashindwe kusimama wima, kutapika,na kubadilika kwa ghafla kwa hisia.



Saratani ya Matiti Wanawake walio hatarini kuupata ugonjwa huu ni:

  • Ajuza
  • Wenye asili ya kihindi au kizungu
  • Wanawake ambao washaugua saratani ya matiti mbeleni
  • Walio na jamaa wa karibu ( mama,dada,binti) ambao washawahi kuuguwa ugonjwa huu
  • Wanawake wenye hitilafu ya kinasaba kutoka kwa mzazi aliyeugua ugonjwa huu
  • Wanawake tasa au waliowapata watoto baada ya umri wa miaka 30.
  • Wanawake waliopata damu yao ya hedhi wakiwa na umri mdogo kabla miaka 12.
  • Wanawake waliokatika hedhi wakiwa wamechelewa baada ya miaka 50.
  • Wanawake wenye matiti makubwa(daktari anaweza kukuelezea baada ya uchunguzi wa mammogram)
  • Wanawake waliotumia tembe za uzazi,waliokosa kunyonyesha, wanaokunywa pombe kila siku,wanaonenepa sana baada ya kukatika hedhi,wanaomeza vidonge vya kubadilisha nasaba,na wale ambao hawakunyonyesha.

Dalili ya saratani ya Matiti:
  • Uvimbe kwenye matiti au kwapa
  • Mabadiliko katika umbo la matiti
  • Chuchu kutoa usaa ama titi kuwa nyororo
  • Chuchu kupotelea ndani ya matiti badala ya kujitokeza nje
  • Madutamaduta kwenye matiti kama yale ya maganda ya machungwa
  • Kubadilika kwa ngozi ya matiti na chuchu kuonekana zimefura

Ukiwa na mojawapo ya dalili hizi muone daktari,ni vyema kufanyiwa uchunguzi wa mammograms.
Fanyiwa uchunguzi wa matiti mapema ili kutambua saratani ya matiti mapema.Kujichunguza kila mwezi na kufanyiwa uchunguzi wa mammograms mara moja kwa mwaka hasa wanaozidi miaka 40 in bora.

0 comments:

Post a Comment