Kila mwanamke hupitia
hatua ya kupatwa na hedhi
mara moja kwa mwezi, ikiwa
ni maumbile ya kawaida
waliyoumbwa nayo. Lakini
wanawake wengi
husumbuliwa na matatizo
kadhaa siku chache kabla au
wakati wa siku zao, matatizo
hayo hutofautiana kati ya
mtu na mtu kutegemeana na
afya ya muhusika.
DALILI ZA MATATIZO YA
HEDHI
Siku chache kabla ya hedhi,
baadhi ya wanawake
hupatwa na hofu na huwa
wenye hasira. Husumbuliwa
na mfadhaiko wa akili,
huumwa na kichwa, matiti
hujaa maziwa, hukosa
usingizi na kuvimba sehemu
za siri. Hali hii
husababishwa na
kukosekana kwa uwiano wa
homoni (Homone imbalance)
na hali hii huweza kukoma
ndani ya saa 24 baada ya
kuanza hedhi.
MAUMIVU MAKALI YA HEDHI
Wengine hupatwa na
maumivu makali sana wakati
wa hedhi. Maumivu hayo
huwapata akina mama ama
siku mbili ama tatu kabla au
mara tu waanzapo siku zao.
Hali hii pia inasababishwa
na kutokuwepo kwa uwiano
wa homoni mwilini, ambako
kumesababishwa na ukosefu
wa virutubisho
fulani.Wengine hutokwa na
damu nyingi kuliko kawaida
au kukaa katika siku za
hedhi kwa kipindi kirefu
kuliko kawaida. Kuna sababu
nyingi zinazoweza kuchangia
hali hii, ikiwemo kuugua kwa
muda mrefu, kupatwa na
hofu, huzuni, mshtuko na
sababu nyingine za kitabibu.
JUISI YA MBOGA ZIFUATAZO
HUTIBU
Kwa kutumia vyakula asilia
unaweza kuepukana na
maumivu ya mara kwa mara
wakati wa siku zako. Katika
orodha ndefu ya juisi za
mboga zinazotibu kwa
uhakika matatizo yote ya
hedhi, ni Kotimiri (Parsley),
mboga ya majani ambayo
upatikanaji wake ni rahisi.
Kwa mujibu wa watafiti,
Kotimiri ina uwezo wa
kurekebisha uwiano wa
homoni hivyo kuondoa
matatizo kadhaa ya
hedhi.Inaelezwa kuwa uwezo
wa Kotimiri kurekebisha
matatizo ya hedhi unatokana
na kuwa na aina ya
kirutubisho kiitwacho ‘Apiol’
ambacho pia kimo miongoni
mwa homoni za jinsia ya
kike (estrogen). Maumivu na
mvurugiko wa siku hurejea
katika hali ya kawaida kwa
kunywa juisi ya Kotimiri
mara kwa mara.Aidha, juisi
hiyo inapochanganywa na
juisi ya viazi pori (Beet
Root), karoti au matango
huwa na nguvu zaidi.
Kiwango kinachoshauriwa
kuchanganya kiwe na ujazo
sawa kwa kila aina ya juisi
utakayochanganya. Juisi
yenye mchanganyiko huo ni
rahisi kutengeneza na ni
dawa inayoweza kumsaidia
mwanamke wakati wote wa
maisha yake bila kuhitaji
kutumia dawa zingine kali za
kuzuia maumivu (pain
killers) ambazo huwa na
madhara baadaye.
TANGAWIZI NAYO HUTIBU
Tangawizi nayo ni dawa
nzuri sana ya kutibu
matatizo yatokanayo na
hedhi, hasa katika tatizo la
maumivu makali na
kutokupata hedhi. Chukua
kipande cha tangawizi
mbichi, kiponde na kiweke
kwenye kikombe cha maji ya
moto kwa dakika chache,
kisha tia sukari kiasi na
unywe mchanganyiko huo,
kwa siku mara mbili kila
baada ya mlo.
UFUTA NAO NI DAWA
Ufuta (Sesame) nao ni
miongoni mwa mbegu za
asili unazoweza kula na
kutibu matatizo ya hedhi.
Saga ufuta na pata unga
wake kisha uchanganye na
maji ya moto, kunywa mara
mbili kwa siku. Kinywaji hiki
huondoa maumivu wakati
wa hedhi kwa wasichana
wadogo.Ukitumia mara kwa
mara kinywaji hiki cha ufuta,
hutibu pia tatizo la kupata
hedhi kidogo. Pia unaweza
kuchangaya maji ya kuoga ya
uvuguvugu na mbegu za
ufuta zilizopondwa pondwa
kiasi cha kiganja kimoja,
nayo hutoa nafuu kubwa
kwa wanaosumbuliwa na
maumivu, hasa ukitumia
siku mbili kabla ya siku
zako.
PAPAI NALO NI DAWA
Mwenyezi Mungu
ametuumba na kutupa
mazao mengi ambayo yana
uwezo wa kutatua matatizo
yetu ya kiafya, iwapo
tutagundua siri hiyo. Papai
bichi nalo linaelezwa na
watafiti wetu kuwa lina
uwezo wa kulainisha misuli
ya njia ya uzazi hivyo
kufanya utokaji wa hedhi
kuwa mwepesi usio na
maumivu. Papai huwa na
manufaa zaidi kwa
wasichana haswa kwa wale
wenye tatizo la kutopata
siku zao kutokana na kuwa
na ‘stress’ au mawazo.
Utapata faida hiyo kwa kula
mara kwa mara tunda hilo
bichi (ambalo halijaiva lakini
limekomaa)
0 comments:
Post a Comment