Sunday, 27 April 2014

NAMNA YA KUTUMIA TANGAWIZI KWA TIBA

Kutibu kutokusagika kwa chakula tumboni, Gesi tumboni, Msokoto wa tumbo (bila kuharisha), Kutapika, Mshtuko/Mkazo wa ghafula (wa Msuli),Maumivu ya tumbo na Kibofu cha mkojo ikiambatana na Homa, Mafua, Kukohoa na Pumu.


TUMIA JAMU YA TANGAWIZI.
JINSI YA KUTENGENEZA JAM YA TANGAWIZI.


Kamua TANGAWIZI mbichi kisha changanya maji yake (Juice) na Sukari. Chemsha mpaka mchanganyiko huo uwe mzito. Ongeza Zafarani iliyosagwa,Iliki iliyosagwa, Kungumanga zilizosagwa na karafuu iliosagwa. Iweke dawa hii vizuri na tumia inapo hitajika.
KWA KUVIMBIWA NA KUTAKA HAMU YA KULA.
Changanya Juice ya TANGAWIZI, Juice ya Limau na Chumvi Mawe kwa vipimo vilivyo sawa. Hakikisha umechanganya vizuri. Kunywa dawa hii kabla ya Chakula.


Vingineyo changanya vipimo vilivyo sawa sawa vya Juice ya TANGAWIZI na Sukari Mawe. Koroga vizuri, kunywa kabla ya kula chakula. Dawa hii husafisha Ulimi na Koo na hukuongeza hamu ya kula na kukufanya mchangamfu.MAUMIVU YA KOO NA KUKAUKA SAUTI
Tafuna vipande vidogo vya Tangawizi.KWA KUHARISHA
Chua sehemu zinazozunguka kitovu kwa Juice ya Tangawizi.KWA KISUKARI
Kunywa Juice ya Tangawizi iliyochanganywa na Sukari mawe.KIUNGULIA, KUKOSA HAMU YA KULA NA BAWASIRIKICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA
Kunywa mchanganyiko wa Juice ya Tangawizi na Juice ya Kitunguu.MAUMIVU YA KICHWA CHA WASIWASI
Changanya Juice ya Tangawizi na Maziwa, kisha kausha. Nusa unga huo kama Tumbaku.MAUMIVU MAKALI YA TUMBO
Changanya kijiko kimoja cha au viwili vya Tangawizi iliyosagwa na kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya Kastoroli. Kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku.BARIDI YABISI SUGU
Changanya kijiko kimoja cha Tangawizi ya unga na vijiko 24 vya maji kunywa mchanganyiko huu ukiwa vuguvugu. Ulale na ujifunike mpaka utoe jasho.KUUMWA JINO NA MAUMIVU YA KICHWA
Chukua Tangawizi ya Unga koroga na maji kidogo iwe nzito kama tope. Jipake na uchue kwenye paji lako la uso kabla ya kulala. Kwa Jino jipake na uchuwe kwenye Shavu.

ZIJUE FAIDA YA KUTUMIA TANGAWIZI, HUTIBU MAGONJWA 72
Ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa Tangawizi. 
Mmea huu unafanana sana na Binzari ikiwa bado haijamenywa maganda yake. Na kwa hapa Tanzania 

Tangawizi hulimwa sana mikoa ya nyanda za juu Kusini na baadhi ya mikoa kama Kilimanjaro, baadhi ya maeneo ya mkoa wa Manyara, Morogoro, na kwingineko nchini.
Pia kama bidhaa inapatikana nchi nzima kwa bei nafuu kabisa na kila mtu mwenye uwezo wowote wa kiuchumi anaweza kununua aidha kwa kipande kimoja, fungu au kwa kilo pia.


Tangawizi inatumikaje ?:
Mmea huu unaweza kuonekana kama mmea wa kawaida na watu kuutumia tu kama mazoea lakini Kiungo hiki kinaweza kutumiwa kama Dawa. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kikiwa kimekaushwa na kutengen
ezwa unga.


Nini Faida ya Tangawizi?


Tangawizi ni mmea kati ya mimea mingi yenye maajabu, Mmea huu unaweza kutumika kama dawa na kutibu magonjwa mengi tu zaidi ya 72 yaliyo ndani ya miili yetu na kutuacha tukiwa wazima na kutekeleza majukumu yetu ya kila siku.


Pia kiungo hiki kinafaida zaidi kwa Wagonjwa hasa walio athirika na Ugonjwa wa UKIMWI. Hivyo chonde kwa wale wenye matatizo kama haya wanaweza kupata faida zaidi ya Maajabu ya Mmea huu wa Tangawizi.


Jinsi ya kuitumia kama Dawa:
Tangawizi ikiwa imesagwa au Mbichi iliyopondwa pondwa inaweza kutumika kama Kinywaji kama ilivyozoeleka kwa watu wengi.
Namna rahisi ya kuitumia Tangawizi ni katika chai, inakuwa ni mubadala wako wa majani yale meusi ya chai ambayo yenyewe huwa na kaffeina ambayo hupelekea magonjwa mengi mwilini (soma kuhusu 

kansa na uzito kupita kiasi kuyajuwa madhara ya kutumia majani ya chai nyeusi), Pia inaweza kutumika katika vyakula hasa nyama na mbogamboga zingine, inaweza kuongezwa katia juisi freshi pia na kuleta radha nzuri ambayo ni dawa pia.
Hutibu Magonjwa gani ?
Tangawizi husaidia yafuatayo:
Kuongeza hamu ya kula
Kupunguza kichefuchefu
Kutapika, kuharisha
Kisukari
Shinikizo la damu
Kuongeza msukumo wa damu
Kutoa sumu mwilini
Maumivu ya tumbo na
Gesi tumboni.

Pia husaidia uyeyushwaji wa chakula tumboni. Vilevile husaidia wakati wa matatizo ya mafua au flu na magonjwa mengine mengi.
Kama utakuwa makini au kuwahi kuwahudumia wagonjwa wa UKIMWI basi magonjwa hayo hapo juu ni 
kati ya Magonjwa nyemelezi yanao wasumbua sana hawa ndugu zetu hivyo wakitumia Tangawizi basi wataweza kuondokana kabisa na matatizo hayo na kuishi vizuri na kutekeleza majukumu yao ya kila siku na kuepukana na kulala tu kitandani.

0 comments:

Post a Comment