Monday, 7 July 2014

MATIBABU YA CHUNUSI (TREATMENT OF ACNE)

Lengo la tiba ya chunusi ni kupunguza uzalishaji wa mafuta ya sebum usoni pia kutibu vijidudu vya bakteria ambavyo hushambulia ngozi ya uso na kusababisha viupele vinavyowasha  na wakati mwingine kuleta maumivu usoni.
Uchaguzi wa dawa hutegemea na jinsi ugonjwa ulivyoshambulia uso (severity), sehemu iliyoharibika huhitaji kufanyiwa usafi wa kutosha kila siku tena uwe wa ziada zaidi ya kawaida kwa kutumia sabuni zenye antibaotiki, kubadilisha tabia ya chakula, matumizi ya kemikali za Sulfur salicylic acid na Resorcinol haisaidii kuondoa chunusi.
Matibabu hugawanywa sehemu kuu tatu ambazo kwanza ni wale wenye chunusi kidogo (mild acne), pili wenye chunusi za wastani (moderate acne) na tatu ni wale walioathirika sana yaani hali yao ni mbaya (severe acne).
Wale wenye vipele au chunusi kidogo hutumia dawa moja tu ambayo hujulikana kama Benzoyl peroxide au pia huchanganya na dawa ya antibaotiki, mgonjwa hutumia kila siku kwa kipindi cha wiki sita na zaidi.
Pia dawa kama Adapalene gel na nyingine kama Tazarotene gel hutumika. Dawa zipo nyingi nyingine ni kama vile Azelaic acid cream na Glycolic acid.
MADHARA YA DAWA
Madhara ya hizi dawa siyo makubwa na baadhi ni kama vile uso kukauka sana na baadhi ya dawa hizo hutumika kwa wanawake kipindi ambacho hawana mimba.
Lakini kwa wanawake wajawazito wasitumie dawa zozote bila ushauri wa daktari kwa kuwa baadhi ya dawa ni hatari kwa akinamama wenye mimba.
Wale wenye chunusi za wastani huhitaji dawa za antibaotiki kama vile Tetracycline, Doxycline, Minocycline na Erythromycin.
Dawa hizi hutumika kwa kipindi kisichopungua wiki 12 na hutolewa na daktari baada ya kuridhika kuwa haziwezi kumuathiri mgonjwa, hivyo basi naomba msinunue dawa hizi hovyo.
Wale wenye chunusi nyingi dawa ya kunywa ya Isotretinoin ndiyo dawa sahihi na hutibu vizuri na hutumika baada ya kupima uzito na hutumika kwa wiki 16 hadi 20. Itumike kwa ushauri wa daktari.

0 comments:

Post a Comment