Wednesday 14 May 2014

KUONDOA CHUNUSI KWA KUTUMIA MANJANO


Mahitaji  ya kuondoa chunusi kwa manjano
- Vijiko viwili (2 tbs) vya unga wa binzari ya Manjano (Turmeric powder)

- Kijiko kimoja (1 tbs) cha unga wa Riwa – wengine huita Liwa (Sandalwood)
- Vijiko vinne (4 tbs) Maji masafi
- Nusu kijiko (1/2 tbs) cha mafuta ya Haradali (Mustard Oil)
- Kijiko kimoja (1 tbs) cha maji ya ndimu/limao (Lemon juice)

Jinsi ya kufanya
Safisha uso wako kwa sabuni uwe msafi. Changanya vyote kisha upake usoni (kasoro eneo lililozunguka jicho). Kaa nayo usoni mpaka ikauke au kwa muda wa dakika 15. Kisha nawa uso wako kwa
maji ya kawaida – usitumie sabuni. Fanya hivi mara 3 kwa wiki na utaona mafanikio ya chunusi kuisha.
Kama una chunusi nyingi sana chukua glasi moja ya maziwa ‘fresh’; weka kijiko kimoja (tea spoon) cha unga wa binzari ya Manjano, koroga na unywe – kunywa mara 3 kwa wiki (sio kila siku) – Itasaidia kuboost ‘immunity’ yako na pia kuisaidia system yako mwilini katika kutibu chunusi.
Haya, hangaika nayo mwenyewe..shukran nyingi kwa shear illusions

0 comments:

Post a Comment