Thursday 1 May 2014

UGONJWA WA MATENDE NA MADHARA YAKE (ELEPHANTIASIS)


Ugonjwa wa matende ni aina ya ugonjwa
unaosababisha ngozi na tishu zilizo chini
ya ngozi ya mwanadamu kuwa nene
(thickening of skin and underlying
tissue).
Ugonjwa huu huathiri miguu,
mikono, figo, korodani na kusababisha
korodani kuvimba na kuwa kubwa
sana.

Inakisiwa watu milioni 120 duniani
wana maambukizi ya ugonjwa huu
ambapo kati yao milioni 40 wamepata
madhara makubwa kutokana na ugonjwa
huu.
Kati ya hawa walioathirika theluthi
moja huapatikana katika bara la Afrika,
theluthi moja nyingine hupatikana India,
na kiwango kilichobakia hupatikana katika
visiwa vya Pacific, Marekani na Asia ya
kusini.

Ugonjwa wa matende husababishwa na
vimelea aina ya minyoo (parasitic worm)
vinajulikana kama Wuchereria bancrofti,
Brugia malayi, B. timori ambavyo
huenezwa na mbu jike aina ya culex
quinquefasciatus mosquitoes na jamii
fulani ya mbu dume(Anopheles species)
wakati minyoo aina ya Brugia
roundworms huenezwa mbu
wanaojulikana kama Mansonia
mosquitoes.
Mbu hawa hueneza ugonjwa
huu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa
mwengine.
Aina nyingine ya ugonjwa wa matende
inayojulikana kama nonparasitic
elephantiasis au podoconiosis ambayo
haisababishwi na vimelea vyovyote
hupatikana katika nchi za Afrika Mashariki
(Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda,
Burundi) Sudan, Egypt na Ethiopia.
Asilimia
6 ya maambukizi ya aina hii ya
podoconiosis hupatikana nchini Ethiopia.

 
Nini hutokea baada ya maambukizi?
Kwa kawaida mtu aliyeambukizwa
ugonjwa huu huwa na mabuu (larvae)
kwenye mfumo wa damu mwilini mwake
wanaojulikana kama microfilariae. Mabuu
haya husafiri kutoka kwenye mfumo wa
damu hadi kwenye mfumo mwingine
unaojulikana kama mfumo wa limfu
(lymphatic system) na kukua kuwa minyoo
kamili (adult worms) ambayo huziba
mfumo huu wa limfu ambao
unategemewa sana katika kuweka uwiano
sawa wa maji (fluid balance) kati ya mfumo
wa damu na tishu ndani ya mwili na
husaidia kuupa mwili kinga dhidhi ya
magonjwa mbalimbali.
Minyoo hii huishi
kwa miaka minne hadi sita na katika uhai
wake huzaa mamilioni ya mabuu
(microfilariae) mengine wakati ikiwa
kwenye mfumo wa damu.

 
Mbu huenezaje ugonjwa huu?
Mtu ambaye ameambukizwa ugonjwa huu
huwa na mabuu kwenye mfumo wake wa
damu na anapongatwa na mbu ambawo
wanauwezo wa kuchukua mabuu haya
ambayo huendelea kukua na kufikia hatua
ya kuambukiza mtu mwingine ndani ya
mwili wa mbu.
Kwa kawaida, ukuaji huu
wa mabuu ndani ya mwili wa mbu
huchukua wiki moja hadi tatu na baada ya
kukua na kufikia hatua ya kuambukiza mtu
mwingine, mabuu haya husogea mpaka
kwenye sehemu ya mdomo wa mbu
ambayo ndio huwa humng'ata mtu wakati
mbu anapofyonza damu kutoka kwa mtu.
Mbu mweye mabuu kwenye mdomo wake
anapomngata mtu ili kufyonza damu,
ndipo mabuu haya yanapoingia kwenye
mwili wa mtu na hivyo kusababisha
maambukizi ya ugonjwa huu.

 
Dalili za ugonjwa huu ni zipi?
• Dalili kubwa ya ugonjwa huu ni kuvimba
sehemu ya chini ya mwili yaani kwenye
miguu na vidole.Pia mtu anaweza kuvimba
sehemu ya mikono au mkono wote
pamoja na vidole vya mkononi. Wengine
huvimba kwenye korodani (wanaume).

• Kuhisi uzito na kukamaa kwa mikono au
miguu kutokana na uvimbe uliopo.
• Kutoweza kutumia kiungo husika
kilichovimba.

• Maumivu au kutohisi vizuri kwenye
mikono au miguu.
• Kupata maambukizi ya mara kwa mara
kwenye sehemu iliyovimba.

• Ngozi kuwa nene na ngumu kwenye
mikono au miguu.
 
 Dalili nyingine ni pamoja na;
- Homa
- Maumivu ya kichwa
- Maumivu kwenye jointi na mifupa
- Kutapika

- Vidonda kwenye mikono au miguu
- Mistari ya rangi nyekundu inayoonekana
kwenye mikono au miguu (red streaks)

 
Vipimo vya uchunguzi
• Blood examination under microscope -
Kipimo cha kuangalia damu kwenye
hadubini ili kuangalia kama kuna mabuu
ya ugonjwa huu wa matende.
Kwa wale
ambao wana ugonjwa huu kwa muda
mrefu, mabuu hayaonekani kwenye damu
kwani tayari yatakuwa yameshaingia
kwenye mfumo wa limfu. Hivyo,
kutoonekana kwa mabuu kwenye damu
kwa kutumia hadubini si kigezo cha
kusema kwamba mgonjwa hana ugonjwa
huu wa matende.

• Vipimo vyengine vinavyoweza kutumika
ni pamoja na CT Scan, MRI, Doppler
Ultrasound, Radionuclide Imaging ili
kuweza kutofautisha ugonjwa huu na
magonjwa mengine yanayosababisha
kuvimba kwa miguu au mikono kama
saratani za aina mbalimbali, kuganda kwa
damu kwenye mishipa ya damu(blood clot)
na kadhalika.

• Kwa wale wenye kuvimba korodani, ni
muhimu kwa daktari kuchukua kipimo
kwa kukwangua sehemu husika kisha
kuchanganya na potassium hydroxide na
kutazama kwenye hadubini kama kuna
dalili (Meddler bodies, sclerotic bodies) za
ugonjwa wa fangasi unaojulikana kama
chromobalstomycosis (unaosababishwa
na fangasi aina ya Fonsecaea pedrosoi,
Phialophora verrucosa, Cladosporium
carrionii, au Fonsecaea compacta).
Pia
ukungu huu huweza kuoteshwa maabara
ili kuangalia kama kuna fangasi aina
yoyote ile niliyotaja hapo juu watakaota.

 
Tiba ya ugonjwa wa matende ni nini?
Tiba ya ugonjwa wa matende hutegemea
na sehemu husika. Kwa wagonjwa walio
katika jangwa la sahara, tiba ni dawa aina
ya albendazole pamoja na ivermectin.
Kwa
wagonjwa waliopo sehemu nyingine
duniani tiba huusisha matumizi ya
albendazole pamoja nadiethylcarbamazine.
Kusafisha sehemu iliyoathiriwa na
ugonjwa wa matende mara kwa mara
husaidia kupunguza dalili na viashiria vya
ugonjwa huu.
Kwa wale waliovimba korodani kutokana
na ugonjwa wa matende,
 
tiba yake ni upasuaji.
Wakati mwingine, kama mgonjwa
atakuwa amevimba sana korodani, basi
baada ya kufanyiwa upasuaji wa kawaida,
atahitaji kufanyiwa upasuaji kurekebishwa
ngozi yake (plastic surgery)
.
Katika utafiti uliofanywa na chuo cha
Liverpool school of tropical medicine
mwaka 2005, umeonyesha dawa ya
antibiotiki hususan doxycyline inaweza
kutumika kutibu ugonjwa huu wa
matende kutokana na minyoo (adult
worms) kuwa na bakteria aina ya
wolbachia wanaoishi ndani ya minyoo hii,
hivyo dawa hii hutibu kwa kuua bakteria
hawa na kusababisha minyoo hii kufa, na
kuondosha kabisa microfilariae kwenye
damu ya mgonjwa na hivyo mgonjwa
kupona.
Dawa hii hutumika kwa muda wa
wiki 8. Hata hivyo, kama mgonjwa
atakuwa na mabuu ndani ya mfumo wake
wa limfu, basi itakuwa vigumu kwake
kupona.
Utafiti zaidi unahitajika ili kuwa na
uhakika zaidi juu ya dawa hii kutibu
ugonjwa huu.

 
Kinga ya ugonjwa wa matende ni nini?
• Shirika la afya duniani (WHO) limeanzisha
jitihada za kutokomeza ugonjwa huu wa
matende ifikapo mwaka 2020.

• Matumizi ya dawa aina ya albendazole
kwa wale walio katika hatari kupata
ugonjwa wa matende unaosababishwa na
vimelea.

• Kuvaa viatu wakati wa kutembea nje ili
kujikinga kupata maambukizi ya aina ya
podoconiosis.

• Kuosha miguu na mikono kwa kutumia
maji na sabuni
• Kuosha miguu kila siku kwa kutumia
antiseptic (bleach).

0 comments:

Post a Comment