Thursday 1 May 2014

IJUE KINGA YA MWILINI MUHIMU SANA


Kinga ya mwili ni muhimu sana katika mwili
wa mwanadamu. Inapokuwa sawa
inatusaidia miili yetu kuishi bila magonjwa
yatokanayo na uambukizi wa virusi na
bakteria. Au hutusaidia mwili kutorudiwa na
magonjwa mara kwa mara.

KINGA YA MWILI INAVYOFANYA KAZI: Kila
unapoumwa, mwili unajitahidi kutafuta
wavamizi (virusi & bakteria) ambao
wamesababisha kuugua. Kinga ya mwili
inapambana ili kuwaangamiza wavamizi.
Baada ya hapo, kinga hiyo (hizo) hutengeneza
protini ili kwa siku za baadae ziweze
kuwatambua hawa wavamizi endapo
watajirudia. Endapo watajirudia tena, basi
kinga ya mwili itapambana nao na
kuwamaliza kabla hali ya ugonjwa kujitokeza, na hatimaye mtu kutojihisi kuumwa. 
Hii
husaidia mtu kutopata magonjwa mara kwa
mara, au magonjwa kutojirudia. Mfano tatizo
la mafua, wapo ambao wanaweza kumaliza
hata miaka 2 bila kuugua, ingawa virusi wa
mafua wakati mwingine huwa anajibadilisha
harudi mara ya pili kwa style kama aliyokuja
nayo mwanzo, kitu ambacho husababisha
kwa wengine kuugua mafua mara kwa mara.

VYAKULA VINAVYOSAIDIA KUONGEZA KINGA YA
MWILI

1. Mboga za majani
 
2. Matunda

3. Viazi vitamu

4. Karoti

5. Kitunguu saumu
6. Maziwa mgando
 
7. Uyoga
 
8. Mbegu za maboga (tafuna zilizokauka)

0 comments:

Post a Comment