Wednesday, 30 April 2014
UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UGONJWA WA FIGO UNAOTOKANA NA KISUKARI (DIABETIC NEPHROPATHY)
YAPO madhara ya ugonjwa wa kisukari katika mwili wa binadamu na moja wapo ni ugonjwa wa figo (diabetic nephropathy) pamoja na ukosefu wa nguvu za kiume.
Matatizo haya huwapata watu wenye kisukari na hutokea muda mrefu baada ya mtu kugunduliwa kuwa na maradhi ya kisukari.
Tutaeleza baadaye kwa nini wenye ugonjwa wa kisukari wanakuwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume lakini leo tuangazie tatizo la figo ambayo ina mamia kwa maelfu ya vijiumbo vidogo viitwavyo Nefroni
(Nephrons).
Kazi ya hizi Nefroni ni kuchuja damu na kutoa uchafu mwilini mwako kwa njia ya mkojo.
Kwa watu wenye kisukari, Nefroni huwa na tabia ya kunyauka, kuzeeka na kuwa na makovu kadiri miaka inavyopita. Baada ya muda fulani, hushindwa kabisa kazi yake ya kuchuja uchafu, matokeo yake protini ambazo kwa kawaida huwa haziwezi kuchujwa, hufyonzwa na kutoka katika mkojo.
Chanzo hasa
chakunyauka na kuzeeka huko au kuwa makovu kwa Nefroni hakijulikani lakini udhibiti mbaya wa sukari husababisha uharibifu wa figo, na madhara huongezeka maradufu kwa watu wenye shinikizo la damu lisilodhibitiwa.
Ifahamike kuwa
si kila mwenye kisukari anaweza kupata ugonjwa wa figo lakini watu wengi wenye maradhi haya kwa upande wa wanaume huwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Wagonjwa wa kisukari ambao pia ni wavutaji wa
sigara, na wale wenye aina ya kwanza ya kisukari (type 1 Diabetes Mellitus) kilichoanza kabla hawajafika miaka 20, wana hatari kubwa ya kupata matatizo ya figo.
Dalili
Kwa kawaida, mtu mwenye tatizo hili anaweza asioneshe dalili zozote katika miaka ya mwanzo ya ugonjwa. Mara nyingi dalili huanza kujitokeza miaka 5 mpaka 10 baada ya figo kuathirika nazo ni kukosa hamu ya kula, kujihisi uchovu na kwa ujumla kutojihisi vizuri.
Dalili nyingine
ni pamoja na kuumwa kichwa, kichefuchefu na kutapika na kuvimba miguu.
Vipimo
Kwa watu wenye kisukari,
wanashauriwa kufanya uchunguzi wa figo zao mara moja kwa mwaka ambapo utachunguzwa kama una dalili zozote zinazoashiria matatizo ya figo. Utapimwa mkojo kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha protini iitwayo Albumin au Microalbuminuria.
Kuwepo kwa kiasi kingi cha protini katika mkojo ni mojawapo ya dalili za kuwepo kwa tatizo katika figo.Vipimo vingine ni pamoja na kiasi cha Urea Nitrogen katika damu (BUN), kiwango cha Creatine katika
Damu
(serum creatinine), kiasi cha protini katika mkojo wa saa 24 (24-hour urine protein), kiasi cha madini ya Phosphorus, calcium, bicarbonate, PTH, na Potassium katika damu, kiasi cha wingi wa damu (Hemoglobin), na wakati fulani kufanya Biopsy ya figo kwa ajili ya uthibitisho wa tatizovipimo vya watu wenye kisukari, tukasema wanashauriwa kufanya uchunguzi wa figo zao mara moja kwa mwaka ambapo utachunguzwa kama una dalili zozote zinazoashiria matatizo ya figo. Utapimwa mkojo kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha protini iitwayo Albumin au Microalbuminuria.
Kabla ya kuanza
kueleza matibabu ya matatizo haya nikumbushe kwa kusema kuwa kuwepo kwa kiasi kingi cha protini katika mkojo ni mojawapo ya dalili za kuwepo kwa tatizo katika figo.
Mgonjwa wa maradhi
haya ni lazima katika vipimo atakavyofanya daktari aangalie kiasi cha Urea Nitrogen katika damu (BUN), kiwango cha Creatine katika damu (serum creatinine) na kiasi cha protini katika mkojo wa saa 24 (24-hour urine protein).
Kabla ya kufafanua tiba
ni muhimu kukumbusha pia kuwa ni vyema mgonjwa akaangaliwa kiasi cha madini ya Phosphorus, Calcium, Bicarbonate, PTH, na Potassium katika damu.
Itakuwa vema kama daktari ataangalia kiasi cha wingi wa damu (Haemoglobin), na wakati fulani kufanya Biopsy ya figo kwa ajili ya uthibitisho wa tatizo.
Matibabu
Matibabu ya ugonjwa wa figo unaotokana na kisukari ni muhimu sana kufanyika haraka baada ya dalili kujitokeza. Lengo kuu la matibabu ni kufanya figo zisiendelee kuathirika. Mojawapo ya njia bora kabisa za kusaidia hilo ni kudhibiti kiwango cha shinikizo la damu kuwa chini ya 130/80 mmHg.
Zipo dawa
ambazo husaidia tatizo hili kama vile zile za jamii ya Angiotensin Converting Enzyme Inhibitors kwa mfano Captopril pamoja na zile za Angiotensin Receptor Blockers zimeonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kushusha shinikizo la damu wakati huohuo kudhibiti kasi ya kuharibika kwa figo kutokana na kisukari.
USHAURI
Wagonjwa wanashauriwa kula lishe yenye kiwango kidogo cha mafuta, matumizi ya dawa za kudhibiti kiasi cha mafuta mwilini, na kufanya mazoezi mara kwa mara kama vile kutembea kwa saa mbili na wawe wanakunywa maji kwa wingi
kabla na baada ya matembezi kwani husaidia sana kuzuia au kupunguza kasi ya kuathirika kwa figo.
Wagonjwa wanashauriwa kubadilisha aina ya chakula wanachokula, kutumia dawa za kisukari kama inavyoshauriwa na daktari na kuchunguza kiwango cha sukari kila mara kwani husaidia kuzuia tatizo hili.
Waliopatwa na ugonjwa wa kisukari wanaweza kuwa na chombo cha kujipima wenyewe kiwango cha sukari mwilini mwao, ugonjwa huu huchangia sana kuua nguvu za kiume.
0 comments:
Post a Comment