Thursday, 14 January 2016

FAHAMU VYAKULA HATARI KWA AFYA YA MTOTO MCHANGA‏



Kuna vyakula ambavyo hutakiwi kumpa mtoto mara tu  unapomuanzishia chakula ?


Ute wa mayai, karanga na jamii ya karanga, asali,Samaki wenye gamba/wasio na mifupa  na matunda machachu (cirtrus ) ni  “vyakula visivyofaa 

kwa mtoto mchanga” Madaktari hushauri watoto wasipewe vyakula hivi adi wanapofikisha umri fulani.



Hata hivyo ni wazi kwamba Madktari wengi wa watoto huwa na mitizamo inayopingana juu ya jambo hili. Ukweli nikwamba tafiti za hivi karibuni zaonyesha kua hakuna ushahidi uliothibitika kisayansi kua Vyakula hivi havifai kwa mtoto mchabga adi afikishe umri fulani.


Je kunasababu yoyote ya msingi  kuchelewa kumpa mtoto vyakula hivi ingawa tafiti zaonyesha ni vyakula salama kwa mtoto?

Mwaka  2008,  AAP walitoa ripoti  ya utafiti wenye kichwa hiki cha habari , 



Tafiti hii ilionyesha hakuna sababu yoyote ya kuchelewa kumpa mtoto chakula cha aina yoyote pale unapomuanzishia chakula kwani vyakula vyote ni salama na hakuna ushahidi wowote wa kisayansi unaoonyesha kwamba kuchelewa kumpa mtoto vyakula hivi humlinda na kumuepusha na uwezekano wa kupata magonjwa yenye uhusiano au asili ya aleji yaani Atopic Deseases

“Repoti hii bado huacha dukuduka hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba vyakula kama maziwa ya ng’ombe namaziwa ya unga ya watoto ,mayai na karanga mara nyingi huwapa watoto wadogo magonjwa yenye asili ya aleji”.



Je hii humaanisha nisalama kumpa  mtoto wangu wa miezi 7 “vyakula visivyofaa kwa mtoto mchanga”?


Hapana,si salama. Ingawa ni kweli kwamba si vyakula hivi vyote  husababisha magonjwa yenye asili ya aleji kwa mtoto ,nikweli kwamba vyakula hivi huatarisha afya ya mtoto kwa namna nyingine .

Kumbuka unaweza muanzishia mtoto chakula kati ya miezi 4-6 na si chini ya hapo. Wataalam wa afya wanashauri kumuhusisha Daktari  wa watoto katika maamuzi yako ya kumuanzisha mtoto chakula,hasa ” vyakula visivyofaa kwa mtoto mchanga”

 Chati hii ya “vyakula visivyofaa kwa mtoto  mchanga” ni kwaajili yakukusaidia kutambua chakula kipi huweza kuleta madhara yapi katika afya ya mtoto.Piahuonyesha umri unaoshauriwa mtoto kuanza kula chakula hicho.Kama nilivyosema apo awali,si vyakula vyote hivi husababisha magojwa yenye asili ya aleji, na si lazima vyakula hivi vilete hathari kwa kila mtoto.

Chakula

Hathari

Umri wa kuanza kula chakula hiki
AsaliHuweza kusababisha food poisoning na magojwa yasababishwayo na bakteria  kwani kinga za mwili (immunity) katika utumbo wa mtoto hazijakua/komaa vyakutosha kukabiliana na bacteria hao Zaidi ya umri wa mwaka 1
Maziwa ya ng’ombe (yasiotolewa cream)Hudhoofisha afya ya mtoto kwani hayana virutubisho vyote muhimu vinavyofaa kwa makuzi na afya ya mtoto. (Maziwa ya ng’ombe hayafai kua mbadala wa maziwa ya mama au maziwa rasmi ya watoto wachanga)
Protini iliyopo kwenye maziwa yasiyotolewa cream ni ngumu kwa mtoto
kumeng’enya.
Zaidi ya mwaka 1
Matunda machachu (citrus)
Huwa na asidi (acid) nyingi ambayo huweza sababisha vipele na maumivu ya tumbo  kwa mtoto.(ingawa hii si aleji) Ni salama endapo mtoto atakula kwa kiasi kidogo kama tunda hili limechanganywa na matunda mengine yasiokua na asidi
Zaidi ya mwaka 1
Maharage na brukoliHusababisha gesi tumboniZaidi ya mwaka mmoja
Karanga na jamii ya karanga (korosho,kungu manga)Huweza kusababisha Aleji na Magonjwa yatokanayo na aleji. Protini yake ni ngumu kwa mtoto kumeng’enya
Hupalia (kupaliwa).vyema kutumia unga wake badala ya ile iliyoburuzwa
Zaidi ya miezi sita (endapo haitampa aleji) Zaidi ya Mwaka 1 au 2
Mahindi  (unga)Huweza kusababisha aleji na magonjwa yatokanayo na aleji Pia si tajiri wa virutubishoZaidi ya miezi 6
YaiHuweza kusababisha aleji na magonjwa yatokanayo na aleji. Ni salama kula kiini cha yai tu Anaweza kula vyakula vyakuoka vilivyotiwa yai zima.(keki,mikate)Zaidi ya miezi 6
ZabibuMbegu zake hupalia (kupaliwa) . Unaweza mpa maji yake yaliyochujwa endapo  umechanganya na matunda mengine (kumbuka zabibu ina asidi nyingi)Zaidi ya miaka 2 Zaidi ya miezi 6
Samaki wenyegamba/wasiokua na mifupa (Shellfish/Crustaceans)Huweza kusababisha Aleji na magonjwa yatokanayo na aleji Inashauriwa kumpa mtoto samaki wa maji baridi Baada ya miezi 6 (ikimpa aleji  jaribu baada ya miaka 2)



Chati hii na Mafunzo ya makala hii si mbadala wa Daktari  wala isikufanye upuuze ushauri wa Daktari

Nimeandika makala hii kwa kutafsiri makala iliyoandikwa katika jarida la Umoja wa madaktari wa watoto wa Marekani. Wamethibitisha kua makala hiyo imeandikwa na wataalam wa afya kwa kuzingatia tafiti za shirika la afya duniani..

“It has been researched and compiled from various medical authorities such as private pediatricians, the AAP, the AAFP, and the WHO.”

0 comments:

Post a Comment