Tuesday 23 September 2014

MIFUPA YA N'GOMBE TIBA YA KUONDOWA FLORAIDI MAJINI



UTAFITI mbalimbali uliofanywa na Wizara ya Maji
na Umwagiliaji, umebaini kwamba mifupa ya
ng’ombe ina uwezo mkubwa wa kupunguza kiasi
cha madini ya floraidi katika maji ya kunjwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wiazara ya Maji na
Umwagiliaji, Mhandisi Bashiri Mrindiko, alisema
madini hayo ya floraidi katika maji husababisha

ulemavu kwa binadamu, ukiwemo wa matende,
kuwa na vichwa vikubwa, matege na kuharibika
kwa meno kwa kuwa na rangi ya kahawia.
“Utafiti wetu umeonyesha kwamba madini ya

floraidi yana madhara makubwa kwa afya ya
binadamu, na katika utafiti huo tumebaini
kwamba mkaa wa mifupa ya ng’ombe

iliyolainishwa kitaalamu ina uwezo mkubwa wa
kuondoa madini hayo katika maji ya kunjwa,”
alisema Mrindiko katika mkutano huo na
waandishi wa habari uliolenga kuzungumzia
mafanikio ya wizara yake na kuongeza:

“Maeneo mengi ya vyanzo vya maji, yana madini
aina ya floraidi yanayozidi kiwango
kilichopendekezwa na Shirka la Afya Duniani
(WHO), ambacho ni miligramu 1.5 katika kila lita
moja ya maji ya kunjwa. Zaidi ya kiasi hicho,
huhatarisha afya za binadamu.”

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, maji ya kunywa
na kupikia yanayotumiwa na binadamu
yanapokuwa na kiasi cha floraidi ya kati ya
miligramu 1.5 na 3.0, husababisha meno kuwa
na rangi ya kahawia, wakati kiwango cha
miligramu kuanzia 4.0 hadi 8.0, huathiri mifupa
na zaidi ya miligramu 8.0 huweza kupindisha
mifupa ya miguu, kwa maana ya kuwa na matege.

Akizungumzia ongezeko la huduma ya maji safi
na salama, Mrindoko alisema kwa mijini hali ya
huduma ya maji si mbaya kwa kuwa imefikia
asilimia 57, huku kwa upande wa vijijini ikiwa ni
asilimia 47 kutokana na uchambuzi wa mpango
wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kwa kipindi cha
mwaka mmoja uliopita.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maji, Nadhifa
Kemikimba, alisema madini ya floraidi yanaathiri
watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano
wanaozaliwa katika maeneo yenye madini hayo.
Aliitaja mikoa yenye vyanzo vya maji yenye
madini hayo kuwa ni pamoja na Arusha,
Kilimanjaro, Singida, Manyara, Tabora, Shinyanga,
Mwanza na Mara.

0 comments:

Post a Comment