Sunday 28 September 2014

MBINU ZA KUWA MTU MAARUFU KATIKA JAMII-3



Kwa muda wa wiki mbili tangu tumenza kujifunza somo hili, nimepokea ujumbe wa watu wengi sana wakikiri kwamba mada imewasaidia kujitambua na sasa wanaelewa jinsi ya kuishi na watu na kuwa maarufu kwenye jamii zao. Leo tunaendelea kuangalia vipengele vingine vinavyozungumzia sheria ya kuwa mtu maarufu na mwenye mamlaka kwa watu.
MWANGAMIZE KABISA ADUI YAKO
VIONGOZI wote maarufu tangu Musa wamefahamu kwamba adui anayeogopewa ni lazima aangamizwe kabisa. 
(Wakati fulani wamelitambua hilo kwa matatizo.)  Iwapo ukuni mmoja ukiachwa unawaka, hata kama una moto mdogo kiasi gani, hatimaye moto utalipuka.  Mambo mengi hupotea kwa kufanywa nusu nusu badala ya kuyamaliza kabisa: Kumwacha adui yako akinusurika kunaweza kuleta kisasi kitatachokugharimu maisha.
KUTOONEKANA SANA KUNAONGEZA HESHIMA
Kuonekana mno kunapunguza thamani ya mtu: Unapoonekana sana na kusikika kila mara, ndivyo unavyozidi kuonekana mtu wa kawaida. 
Ikiwa umejijenga katika kundi fulani, jiondoe kwa muda, jambo ambalo litakufanya uzungumziwe zaidi na kupendwa zaidi.  Jifunze ni wakati gani wa kujitokeza hadharani.  Unapoadimika ndivyo unavyokuwa na thamani mbele za watu.
WAFANYE WENGINE WAISHI KATIKA WOGA
Binadamu ni viumbe wanaopenda kufahamu mambo ya wengine.  Wakikufahamu kwa undani wanaweza kukutawala.  Wachanganye: uwe mtu usiyetabirika.  Tabia isiyofahamika itawafanya washindwe kukuzoea na hivyo kujenga hofu kwako: “Mmmm…huwa hatabiriki unaweza kusema hatajali akaja kukuadhibu.”
USITAKE KUJITENGA KWANI NI HATARI
Dunia ni ya hatari na maadui wako kila mahali, kila mtu anabidi kujilinda. Kujitenga kunaonekana kuwa ndiyo njia salama zaidi. 
Lakini kujitenga kunakuweka katika hatari zaidi kuliko kukulinda.  Kunakunyima fursa ya kupata habari muhimu.  Ni vyema kuchanganyika na watu na kupata marafiki.  Uhusiano na watu wengine ni kinga ya maadui zako.
MFAHAMU MTU UNAYESHUGHULIKA NAYE
Kuna watu wa aina nyingi duniani, na huwezi kudhani kwamba kila mmoja atakabiliana nawe katika namna ile ile.  Walaghai na kuwachanganya baadhi ya watu ili ikitokea uadui au hali ya kutotaka kukuunga mkono wao kwa wao waanze kupingana. Ni muhimu kuwafahamu walio karibu nawe.

USITAKE KUJIUNGA NA UPANDE WOWOTE
Mpumbavu huharakisha kujiunga na upande fulani.  Usitaka kujiunga na upande wowote au suala fulani bali tumikia nafsi yako.  Ukiendelea kuwa mtu huru, utakuwa ni bwana wa watu wengine, ukiwagonganisha watu na kuwafanya wafuate utashi wako. Kama uko mtaani usikubali kuwa mwanachama wa makundi hasimu.

JIFANYE MNYONGE: UBADILI UNYONGE WAKO KUWA NGUVU
Ukiwa mnyonge, kamwe usijaribu kupigana; badala yake jifanye umesalimu amri.  Kusalimu amri kunakupa muda wa kujipanga upya, muda wa kumchanganya na kumkasirisha adui yako, muda wa kusubiri hadi nguvu zake ziishe.   
Usitake kumpa heshima ya kupigana halafu akakushinda .  Wewe salimu amri tu. Ukifanya hivyo utamuudhi na kumfanya achanganyikiwe.   Lichukulie suala la kusalimu amri kama chombo cha kukupatia nguvu.
IMARISHA NGUVU ZAKO
Imarisha nguvu na juhudi zako kwa kuhakikisha ziko katika hali ya juu.  Siku zote nguvu zinazokwenda sehemu moja hushinda zaidi ya zile zinazogawanywa mara nyingi. Kwenye harakati zako za kutafuta umaarufu na kuwashusha maadui zako hakikisha unachagua upande mmoja wa kuelekeza mashambulizi, usikubali kupigana kote kote. Utaelemewa.
JIFUNZE KUBEMBELEZA KATIKA MAMBO YENYE MANUFAA 
Mtu anayejua kubembeleza hufanikiwa katika dunia hii ambayo inategemea nguvu na umahiri wa kisiasa.  Mtu anayebembeleza na kujikomba kwa wakuu wake, hufanikiwa kupata nguvu na ustawi.
UWE MTU SAFI KATIKA JAMII
Lazima uwe mfano wa ustaarabu na ufanisi.  Hakikisha mikono yako haichafuliwi na  makosa na vitendo viovu.  Endesha maisha ya uadilifu ambayo yatawafanya watu wengine waonekane si waadilifu.
EPUKA KUSEMA UKWELI
Ukweli kila mara hukwepwa kwani ni mbaya na unaudhi.  Usikimbilie kusema ukweli labda kama uko tayari kupambana na hasira na maudhi yanayotokana na kufanya hivyo. Maisha ni magumu kiasi kwamba watu wanaoweza kuanzisha uwongo hupendwa na watu wengi.  Kila mtu huwaendea.  Kuna nguvu kubwa kwa kutumia uwongo kwa watu.

0 comments:

Post a Comment