Saturday 27 September 2014

MAUMIVU WAKATI WA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA NI KIASHIRIA CHA NINI? - 3



KUVIMBA kwa kuta za uke kutokana na kushambuliwa na fangasi (candida Albicans) au bakteria. Kuta hizi huanza kuwa na vijitundu vidogo vidogo na kadiri muda unavyokwenda bila kutibiwa, vitundu hivi huongezeka ukubwa na kuwa kama vidonda na hatimaye kuta za uke kuanza kumomonyoka na hali hii huondoa kabisa hamu ya kushiriki tendo.
Matatizo ya shingo ya kizazi (cervical incompetence) kutokana na maambukizi ya fangasi maeneo hayo. Kutoka kwa mbegu za kiume muda mfupi  au saa kadhaa baada ya tendo ni dalili kuu ya tatizo hili. Pia mwanaume anapogonga shingo hii ya kizazi mwanamke huwa kama anatoneshwa kidonda. Hali hii ya mbegu kurudi nje husababisha mwanamke kutoshika ujauzito.
Kuwa na uvimbe kwenye mji wa mimba/mfuko wa uzazi (Uterus). Uvimbe huu kitaalam hujulikana kwa majina mengi lakini `fibroid` ni maarufu Zaidi. Huanza kama mbegu ndogo ya mchicha na hu kua kama boga kubwa. Mwanamke huongezeka ukubwa wa tumbo na baadaye huonekana kama ana mimba kubwa na watu hushangaa kwa nini hajifungui kipindi chote.
Maumivu wakati wa tendo hasa chini ya kitovu huashiria tatizo kwenye mirija ya uzazi. Yawezekana ikawa ni tatizo la mirija ya uzazi kujaa maji machafu kutokana na kuzaliana sana eneo hilo, tatizo ambalo hujulikana kitaalam kama Hyrosalpinx.
Kitu hiki husababisha mirija ya uzazi kuziba kwani maji haya huwa mazito, kitu ambacho husababisha mayai ya uzazi na mbegu za kiume kushindwa kupenya. Kutoshika mimba kwa mwanamke aliye kwenye ndoa au uhusiano kwa zaidi ya mwaka mmoja na anasikia maumivu ya aina hii ni kiashiria kikubwa cha tatizo hili.

0 comments:

Post a Comment