Friday, 20 June 2014

NI KITU GANI KINACHOSABABISHA UUMWE KIPANDA USO?



DALILI ZA KIPANDA USO

Kipanda uso (Migraine) ni ugonjwa au maumivu makali ya kichwa anayokuwa nayo mtu baada ya mshipa wa damu (Enlargement of Artery ) kutanuka katika kichwa chake. Baada ya kutanuka kwa mishipa hii ya damu, pia kuna kemikali ndani ya mwili zinazozalishwa na kuizunguka 


mishipa hii na kupelekea mtu apate maumivu makali ya kichwa na kutanuka zaidi kwa mishipa.Maumivu makali ya kichwa hupelekea mfumo wa utendaji kazi wa mwili pia ubadilike, 


mtu atapatwa na kichefuchefu, kutapika, kuharisha, katika utumbo chakula hakitanyonywa vizuri kiingie mwilini, mtu atashindwa kuona vizuri maeneo yenye mwanga na kutopenda kukaa mazingira yenye sauti au kelele.Vipo vitu mbalimbali vinavyoweza kuchangia mtu apate tatizo 

la kipanda uso, vitu hivi haimaanishi kuwa ni lazima vikusababishe upate na hata kama haupo katika mazingira ya vitu hivi haimaanishi kuwa huwezi kupata tatizo la kipanda uso, miongoni 

mwa vitu hivyo ni kama vile: sauti kali au kelele, harufu kali, aleji, mwanga mkali, kuvuta sigara, matatizo ya kukosa usingizi, kukaa bila kula kwa muda mrefu, pombe, kubadilika badilika kwa siku za mwanamke (menstrual cycle fluctuations).Inawezekana ukawa na tatizo 

hili la kipanda uso, miongoni mwa vitu vinavyowasaidia watu wenye kipanda uso ni kutumia dawa mbalimbali ukijumuisha dawa za maumivu zenye mchanganyiko na caffeine, pia utumiaji wa chai au kahawa umesaidia baadhi ya watu kuwapa nafuu ya maumivu makali ya 

kichwa.Tunaweza kupunguza hatari (risk) ya kupata kipanda uso kwa kubadilisha staili ya maisha yetu ya kila siku, kuepuka vitu vyenye harufu kali, kuepuka utumiaji wa tumbaku 

(sigara), kupata muda wa kutosha kuupumzisha mwili (kulala), kufanya mazoezi, kutokaa bila kula kwa muda mrefu, kunywa maji ya kutosha.Je, unalo tatizo la kipanda uso (Migraine), 

dalili zako ni zipi na ni vitu gani ukitumia unapata nafuu ?.


JITIBU KIPANDAUSO: 
(maumivu ya kichwa katika paji upande) chukua manemane gram 5

Bakalhadi gram 5 na shubiri vidonge hata viwili ponda lain loweka na ujipake kichwani hadi sehemu ya paji angalia isiingie machoni. Fanya 2x1 siku3 ni vizuri uwe na nywele zisizo kubwa

0 comments:

Post a Comment