Thursday 1 May 2014

UTAFITI: NGONO YA MDOMO NI HATARI



Hata hivyo wapo wenye kuvimba hivi lakini
si kwa sababu walifanya ngono kwa
kutumia mdomo, isipokuwa yaweza kuwa
ni sababu nyingine zikiwemo kurithi.
Wataalamu wa masuala ya afya wanashauri
kwamba ni muhimu sana watu wakaachana
kabisa na tabia hii kutokana na ukweli
kwamba siyo tu kwamba ni hatari kwa afya,
pia ni sawa na kujiua mwenyewe, kwani
kitendo hicho kinachangia magonjwa
mengi.
Nchini idadi ya
vijana ambao ni tegemeo la taifa inazidi
kupungua kutokana kuangamia kwa
saratani ikiwemo ya koo.
Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani
(WHO) nchini umeonyesha asilimia 20 ya
saratani ya koo husababishwa na ngono ya
mdomo maarufu kama 'Oral Sex".
Utafiti huo unaonyesha saratani ya koo licha
ya kuambukizwa na njia mbalimbali
ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye pilipili,
 pombe kali, vitu vyenye uchachu pamoja na
kurithi kutoka kwa wazazi.

Utafiti unaonyesha watu wengi hasa vijana
wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya
kufanya ngono wakitumia midomo hasa
ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao.
Katika utafiti  huo wa hivi karibuni, ulibaini
wanaume 747  na wanawake wakiwa 472
hugundulika kila mwaka kuwa na saratani
hiyo huku wanaopoteza maisha kila mwaka
ni wanaume 444 wakifuatiwa na
wanawake 270 kutokana na ugonjwa huo.
Utafiti unabainisha kuwa asilimia kubwa ya
vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45
wanatumia staili ya kuwanyonya wenza
wao sehemu za siri lengo likiwa ni
kuwavutia wapenzi wao katika  kushiriki
ngono.

Vijana  wenye umri huo ndio wahanga
wakubwa kwa sasa kutokana na ugonjwa
huo kuonekana kuwaathiri kwa kasi, huku
wengi wakiwa hawajui athari zake. Baadhi
hujisifia kwamba ni wajuzi, kumbe
wanajitafutia kifo kwa kufanya vitendo
hivyo.
Utafiti unaonyesha kwa watu wazima walio
wengi hawana muda wa kufanya hayo
wanayofanya vijana, hivyo kujikuta angalau
wanakuwa salama na kupatwa na saratani
ya koo kwa njia hiyo inayoonekana kama ni
chafu pia.

Daktari  Bingwa wa Magonjwa ya Saratani
kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk
Crispin Kahesa anasema saratani ya  koo ni
ya pili katika mtiririko wa saratani
zinazowapata wanaume  nchini, ikiongozwa
na ile ya  ngozi (Karposi's Sarcoma) ambayo
huambukizwa kwa njia ya kujamiana. Kuna
saratani aina zaidi ya 24 zinazoisumbua
Tanzania.
Anasema mbali na staili hiyo pia, kuna
baadhi ya watu hupata saratani ya  koo kwa
kurithi kutoka kwa wazazi wao na wengine
kuwa na  umri mkubwa ambao huchangia
kupata tatizo hilo, lakini siyo kwa asilimia
kubwa kama ile ya ngono ya mgomo.

"Hali hii ya vijana wenye umri huo
kuwanyonya wanawake inatokana na ujana,
wengine wanaiga kwenye mitandao, lakini
mambo haya hayakuwepo zamani tofauti na
sasa, utakuta wanaume ili aweze  kumvutia
mwanamke anamfanyia hivyo sehemu za
siri, lakini zamani staili hii haikuwepo
kabisa," anasema  Dk Kahesa na kuongeza.
"Kuna njia nyingi tu za kumvutia mwanamke
lakini siyo hii bila kujua madhara yaliyopo,
vijana wengi nchini wanaona njia rahisi ya
kupendwa na mwanamke ni hiyo wakati
kuna njia nyingi za kufanya. Nje ya hiyo
wanawake wengine huwa na magonjwa
mbalimbali, kwa jumla hakuna usalama
wowote kwa wanaume kufanya kitendo
hicho,"anaongeza

Sababu nyingine zaidi
Anasema staili ya maisha nayo imechangia
kuongezeka kwa ugonjwa huo, vijana
wengi kwa sasa hutumia muda mwingi
kuangalia video za ngono na staili
zinazofanywa na wenzetu wa nje na hivyo
kuongezeka kwa matumizi ya ngono ya
mdomo.
Dk Kahesa anasema asilimia 12 ya
wagonjwa wote wa saratani  nchini
wanasumbuliwa na saratani ya koo, hivyo
kuna kila sababu kwa vijana kubadilisha
tabia na kuepuka kuiga mitindo ya wenzetu
wazungu ambayo mara nyingi inapotosha
mila na tamaduni za Kiafrika.

Anasema  katika mtiririko wa saratani
zinazoongoza nchini saratani ya koo
inashika nafasi ya tano, wagonjwa wengi
wanaopatwa na ugonjwa huo ni watu
wenye umri mkubwa wa miaka 60 na
kuendelea  hiyo inaonyesha kuwa wengi
wao walianza  ngono ya mdomo muda
mrefu wakati wakiwa  bado wadogo.

"Asilimia kubwa ya wagonjwa
wanaopatikana na kansa ya koo nchini,
inawapata  watu wenye umri wa kuanzia
miaka 60 na kuendelea  kutokana na wengi
wao kuanza mapema vitendo vya ngono
kwa njia ya mdomo wakati  bado wadogo
au wengine kurithi kutoka kwa wazazi
wao," anasema Dk Kahesa.

Aina ya kansa ya koo
Tafiti zinaonyesha kuna aina mbili za
saratani ya koo; aina ya kwanza ni
"Oesophagus Carcinoma na Squamous cell
carcinoma, zote  hutofautiana wakati
zinapimwa kwenye darubini lakini matibabu
yake yanafanana.
Aina hizo ndizo zilizopo nchini na huanza
mapema  kuharibu seli ambazo zipo katika
utandu uliopo katika ukuta wa koo kabla ya
kuenea katika  maeneo mengine ya koo.
Visababishi vya kansa ya koo:
Moja kati ya vitu vinavyosababisha kansa ya
koo ni mwenendo wa maisha yetu kwa kula
vyakula vyenye  asidi, vyakula  vichachu,
vyakula vyenye pilipili, pombe kali na
vyakula vigumu ambavyo hukwaruza koo na
hivyo kusababisha saratani.

Anasema  asilimia 90 ya wagonjwa
wanaopokelewa katika Taasisi ya Saratani
ya Ocean road wanakuwa na  historia ya
kutumia vikali kama pombe kali, kuvuta
sigara kwa kupindukia, kula pilipili kwa
wingi na kutumia vitu vyenye uchachu.
 
Dalili za saratani ya koo
Moja kati ya dalili za  mgonjwa wa saratani
ni chakula kukwama kwenye koo, siku za
mwanzo mgonjwa anaweza kushindwa
kumeza chakula kigumu kisha cha majimaji
na baadaye akashindwa kumeza hata mate.
Ugonjwa huo unachukua muda mrefu
kugundua na kuona  viashiria kwani
mwanzo  mgonjwa huanza kupata shida
kumeza chakula na kwamba wagonjwa
wengi wanaofika katika Taasisi hiyo ya
Saratani wanakuwa tayari wamechelewa
kwani wanakuwa katika hatua ya mwisho.

"Unaweza usionyeshe dalili lakini kadri  siku
zinavyokwenda  ndiyo kunakuwa na dalili
zinajitokeza pia katika kipindi hicho mtu
anakuwa na maumivu wakati wa kumeza
chakula, maumivu katika kifua na mgongo
na hata kupungua uzito pamoja na kikohozi
kikavu kinachoweza kudumu mwezi
mmoja," anasema.

Njia ya kuzuia saratani ya koo.
Kwanza mtu mwenye ugonjwa huo
anapaswa kuhawi hospitali ili aanze
matibabu mapema kutokana na ukweli
kwamba mgonjwa anayewahi kupata
matibabu ana uwezekano wa kupona kuliko
yule ambaye amechelewa kugundulika na
kuanza matibabu.

Kama  saratani hiyo itakuwa imeshambulia
viungo  vyote vilivyopo jirani na koo na hadi
kufika katika tezi  au kiungo kingine cha
mwili, mgonjwa anaweza kutibiwa  kwa njia
ya upasuaji, kutumia mionzi na hata kifaa
maalumu ambacho ni kemikali.

Tafiti zilizofanywa nchini
Wataalamu mbalimbali nchi wamefanya tafiti
zinazohusiana na ugonjwa huo na kusema
kuwa kati ya mwaka 1983 hadi 1992
kulikuwa na kati ya watu 546 waliopimwa,
wanaume 430 na wanawake 116
waligundulika kuwa na ugonjwa huo.
Utafiti huo ulishirikisha watu  wenye  umri
wa miaka 21 hadi 90, ulibaini kuwa
wagonjwa wengi walikuwa wenye umri wa
miaka 50-59 tofauti na hali iliyopo sasa
ugonjwa wa kansa ya koo unawaathiri
vijana wenye umri wa miaka 40.

Dk Kahesa anasema katika kipindi cha miaka
saba iliyopita takwimu za taasisi yake
imeongezeka kutoka kutoka wagonjwa 167
hadi kufikia wagojwa 277. Hali inaonekana
huenda ikaongezeka kutokana na ukweli
kwamba wengi wa watu wanaonekana
kuendeleza tabia hatarishi zikiwemo hizo za
kutumia midomo.

Magonjwa mengine sehemu za siri
Miongoni mwa magojwa ambayo yanaweza
kumpata mtu ambaye ananyonya au
kulambana sehemu hizo ni pamoja na
gonjwa wa  gonoreha, ambapo ugonjwa
huu huanzia katika koo na mwanzoni huhisi
kama ni ukavu wa kifua au maradhi ya
kawaida ya kifua, ila baadaye hushuka na
kuelekea katika viungo vya uzazi.
Ugonjwa mwingine ni kaswende ambao
huambukizwa kirahisi zaidi kupitia mdomo
na hasa pale inapotekoa mdomo
unapokutana na kiungo chenye athari hizo.

Vile vile ugonjwa wa chlamydia ni moja
wapo kati ya magonjwa ya zinaa ambao
huambukizwa kwa bakteria  na kwamba
ugonjwa huu pia  huambukizwa kupitia
mdomo, ingawa waathirika wanaweza
wasijijue maana huwa hauna dalili kwa
muda mrefu.

Hepatitis A: 
Hiki ni  ni kirusi
kinachopatikana  katika kinyesi cha
binadamu, kirusi hiki huwaingia wale
wanaopenda kunyonya na kulambana
sehemu za haja kubwa. Ni kwamba kwa
ugonjwa huu mtu anaweza akaharibika
macho hadi kupofuka.

Hepatitis B: 
Ugonjwa huu huambukizwa
kama virusi vya Ukimwi kwa sababu virusi
vyake hukaa katika majimaji yanayotoka
katika sehemu za siri na damu. Mtu akiwa
na ugonjwa huu, mwili wake unakuwa na
vipele vingi na hata majipu ambayo huwa
magumu kupona na wapo wanaokufa.

Vile vile ugonjwa wa Hepatitis C:  
ni ugonjwa
ambao hupatikana pindi damu inapotoka
maana vijidudu vyake vinakaa katika damu.
Ugonjwa huu humfanya mtu kuvimba
viungo na hata kukatika.

Hata hivyo kupitia staili hii yaupeana raha
kwa kunyonyana sehemu za siri, kuna
uwezekano wa kupata maambukiz ya virusi
vya Ukimwi kwa uchache lakini  kwa nchi
zilizoendelea wamebuni aina ya kondom
ambazo huvaliwa katika mdomo  wa
binadamu na hivyo kupunguza hatari ya
kupata madhara hayo.

JE NGUVU ZA KIUME ZINACHANGIA?
Dk Kahesa anasema  hakuna utafiti wa moja
kwa moja unao onyesha kuwa baadhi ya
wanaume wanaofanya ngono kwa njia ya
mdomo wanakuwa na upungufu wa nguvu
za kiume.
"Utafiti wa mtu mmoja hautoshi kuonyesha
kuwa baadhi ya wanaume wanafanya
ngono kwa njia ya mdomo wanakuwa na
ukosefu wa nguvu za kiume, hivyo
kinachotakiwa ni kufanya utafiti wa kina ili
kubaini kama tatizo hilo lipo licha ya
kuwepo kwa kesi nyingi zinazodaiwa kuwa
baadhi ya wanaume hawana nguvu za
kiume na wapenzi wao huwafichia siri kwa
kufanya nao mapenzi kwa njia yam
domo"anasema.

NINI KIFANYIKE:
Wataalamu wa masuala ya ndoa na
saikolojia wanasema kuna njia nyingi za
kuandaana wakati wa tendo la ndoa tofauti
na kunyonyanyana sehemu za siri.
Wataalamu hao wanasema sio sahihi kwa
mwanaume au mwanamke kunyonyana
sehemu za ndoa mwenzake  na kwamba
staili hizo  ni staili za wanzetu wa nje lakini
kitu kinachosababisha kukua kwa kasi kwa
staili hiyo ya kunyonyonyana sehemu za siri
au kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo ni
kutokana na kasi ya  utandawazi.

Wadadisi wa mambo wanadai kuwa baadhi
ya watu huiga staili hizo kutoka katika
mitandao bila kujali kuwa kuna zina
madhara makubwa, hivyo ni jukumu la kila
mtu kulinda afya yake na ya mwenza wake.
Sio kila kitu kinachowekwa katika mitandao
ya kijamii  kina  manufaa la hashaa!  vitu
vingine vinachangia kuhatarisha maisha.

0 comments:

Post a Comment