Thursday 1 May 2014

SABABU ZA WATU WENGI KUSHINDWA KUFANYA DIET NA KUPUNGUZA UZITO WAO

 
Ukweli nikwamba kufanya diet ni
ngumu,na kuna mambo mengi
yanayochangia ugumu huo:

1.   Kutokujua aina ya vyakula vinavyofaa
Wengi hushindwa
kufanya diet kwa muda mrefu
kwani hajui chakula gani humfaa
zaidi,matokeo yake wengi hushinda
njaa au laa hula matunda na mboga
tu na mwisho wasiku njaa huwa
kali,mwili hudhoofika na wanaacha
diet.
 
2.    Gharama ya vyakula hivyo
Diet nyingi huwa na ratiba ya kula
pamoja na aina ya vyakula
unavyotakiwa kula kwa kila
mlo.Mara nyingi vyakula hivi huwa
na gharama kubwa au laa
huongeza gharama katika familia
na kufanya wengi washindwe diet
hizo.
 
3.   Njaa kali
Diet nyingi huelekeza
mtu ale chakula kidogo sana,na
wakati mwingine vyakula hivi
havishiki tumbo kwa muda mrefu
au laa mtu hapati kushiba.hivyo
huwa na njaa kali muda wote.hali
hii uchosha na huwa kama
mateso,wengi huacha diet kwa
kushindwa kuvumilia hali hii. 

4.   Hamu ya kula vyakula wanavyokula
wengine hapo nyumbani
 Harufu nzuri na muonekanoo wa chakula
wanachokula wengine hapo
nyumbani mara nyingi huleta hamu
ya kula na pia huongeza njaa,hii
ufanya wengi waharibu diet zao
kwa kula vyakula hivyo ambavyo si
sehem ya diet zao.
 
5.   Ugumu wa kuacha vyakula unavyovipenda
Ni wazi kabisa
kwamba ni ngumu sana kuacha
kula vyakula unavyovipenda na
ulivyovizoea.Ni ngumu zaidi kama
kuna aina fulani ya chakula ambayo
imekua kama kilevi kwako.Mfano
kuna watu asipokunywa soda fulani
au juice fulani basi siku kwake
haijaisha.

6.   Kuvunjwa moyo na wanaokuzunguka
Mara nyingi
watu wanaokuzunguka hukuvunja
moyo kwa maneno yao,hasa pale
unapofanya juhudi alafu
wanakwambia hakuna mabadiliko
au laa wengine hudiriki hata
kukwambia wewe huwezi
kupungua.
Kutaka matokeo ya haraka – wengi
wanataka kupunguza mzito
mkubwa kwa muda mfupi jambo
ambalo si rahisi,Ingawa juhudi zako
huchangia uaraka wa kupungua.

7.   Uzito mkubwa
uzito mkubwa
sana unafanya Mtu aone
haiwezekani kupungua kwani
inachukua muda mrefu kuona
matokeo makubwa.Ni vyema kujua
kua kila hatua ndogo unayochukua
husaidia,na matokea huja baada ya
muda.
 
8.    Kero mara nyingi marafiki na
ndugu huwa kero kwa maneno yao
hasa pale wanapotaka kukwambia
fanya nini na uache nini ili
upungue.Ni vyema kujua kwamba
unapoona ndugu au rafiki
ameamua kupunguza uzito basi
anasababu za kufanya hivyoo na
anajua ni nini afanye au asifanye ili
apungue.
Naamini kwamba pale
anapoitaji msaada wako basi
ataomba msaada Wazungu husema

0 comments:

Post a Comment