Thursday 1 May 2014

JINSI YA KUISHI NA VIDONDA VYA TUMBO




Kama una vidonda vya tumbo, matibabu
yako yatategemea sababu ya vidonda vya
tumbo. Kama ni bakteria H.pylori, dawa za
kuua na kuondoa bakteria hutumiwa.

Kama ni Non-Steroidal Anti-Inflamantory
Drugs 'NSAIDS' mfano Aspirin & Ibuprofen
utapaswa kutumia Proton Pump Inhibitor
'PPI' mfano Omeprazole & Esomeprazole.
Ingawa matibabu ya siku hizi husisitiza
kuchanganya dawa za kuua bakteria na
Proton Pump Inihibitors 'PPI'.
Mambo yafuatayo yatakusaidia kuishi vizuri
ukiwa na 'Vidonda Vya Tumbo':-
1.     Acha kutumia kahawa na chai, kwa
maana vitu hivi huongeza kiwango cha
asidi kinachotengenezwa na tumbo lako.
Unaweza tumia chai ya mitishamba 'Herbal
tea' kama mbadala.

2.      Kunywa maziwa na ule vitokanavyo na
maziwa kama maziwa mgando 'Yoghurt',
jibini 'Cheese'. Maziwa hufikiriwa kufunika
utumbo na kupunguza athari za asidi ya
tumboni.
3.      Jitahidi kupunguza uzito kama uzito
umezidi na hauendani na kimo chako.
4.      Kula walau kidogo mara kwa mara. Hii
itasaidia kupunguza athari za asidi
inayotengenezwa na tumbo.
5.      Acha au kunywa vileo siku maalumu tu
kwa maana unywaji wa pombe mara kwa
mara hutonesha kwenye vidonda vya
tumbo vinavyotaka kupona.

6.      Epuka matumizi ya viungo vya vyakula
kwa maana hufanya hali kuwa mbaya zaidi.
7.      Acha kuvuta sigara/tumbaku/bangi.
Uvutaji wa sigara utakuweka kwenye hatari
zaidi ya kuanza vidonda vipya na kuzuia
vidonda vingine visipone.

0 comments:

Post a Comment