Saturday 3 May 2014

JE UNAUJUWA UGONJWA WA KIFAFA-2 ?

 

 

Ni vipi naweza kujilinda mimi mwenyewe na familia yangu dhidi ya kifafa?

·         Njia moja muhimu ya kuwalinda watoto dhidi ya hatari ya kifafa ni kuhakikisha ya kwamba wanapata chanjo zao kwa wakati unaofaa. BCG kwa mfano humlinda dhidi ya kifua kikuu. Ugonjwa wa kifua kikuu umekuwa ugonjwa wa kawaida hivi leo na 
unapoathiri mtoto mdogo ambaye hajapata chanjo, hatari ya kupata ugonjwa homa ya uti wa mgongo (meningitis) huongezeka. Homa ya uti wa mgongo itamweka mtoto kwenye hatari kubwa ya kupata kifafa. Chanjo zingine maalumu kwa aina tofauti za homa ya uti wa mgongo zinapatikana hospitalini lakini kwa ada.
·         Homa ni kitu kinachoongezea hatari ya kupatwa na mshtuko ilhali inaweza kudhibitiwa vyema. Mtoto ambaye homa yake inaruhusiwa 
kupanda juu yuko katika hatari ya kupatwa na mshtuko. Ni muhimu kwa homa kudhibitiwa vizuri pindi tu inapoanza. Udhibiiti wa homa unajumuisha; kutumia dawa kama Panado (paracetamol) ama Brufen(Ibuprofen), mtoe mtoto nguo kisha umpanguze na kitambaa  kilicholoweshwa ndani ya maji yenye joto la kadri na la muhimu zaidi ni kutafuta msaada wa matibabu.
·         Ulinzi dhidi ya jeraha, haswa jeraha kwenye kichwa ambayo ndiyo sababu nyingine ya kifafa. Ulinzi hutokana na kuhakikisha ya 
kwamba watoto hawezi kuanguka kwa urahisi kutoka katika sehemu iliyo juu, usimamizi unaofaa wanapocheza na kuweka mbali vitu ambavyo vinaweza kuwaletea madhara wanapocheza. Unaposafiri kwenye gari, ni muhimu kutumia mishipi ya usalama ili kupunguza hatari ya kujeruhiwa ikiwa kutatokea ajali. Jeraha la kichwa ndilo jeraha ambalo hutokea mara kwa mara kukitokea ajali.

 

Ni wapi naweza kuenda ikiwa sitapata usaidizi?

·         Kuzirai ambako hakuwezi kudhibitiwa kunaweza kuwa hatari kwa mgonjwa.Huwa hakuwezi kubashiriwa na unaweza kufanyika wakati mgonjwa yuko karibu na moto, anaendesha gari ana jaribu kuvuka 
barabara, anaogelea ama anafanya kazi akiwa juu (k.m juu ya paa la nyumba). Katika hali hii, kuzirai kutamweka mtu katika hatari kubwa kwani anaweza kuchomeka, kupatwa na ajali, kuzama ama kuanguka na kuumia. Hii ni sababu moja muhimu ambayo inahitaji kifafa kudhibitiwa.
·         Pili, ugonjwa wa kifafa unaweza kutokea mara kwa mara ukiwa hautadhibitiwa. Kuzimia kunaweza kutokea mara kwa mara na kuonekana ni kama unaendelea. Hii ni dharura ya kimatibabu 
ambayo inaweza kusababisha kifo katika mda mfupi. Kwa hivyo ikiwa mgonjwa ataathiriwa na kifafa kwa zaidi ya dakika 5, mpeleke katika hospitali iliyo karibu haraka iwezekanavyo kwa sababu kuzimia hakuwezi kuisha bila ya dawa

Nitapata usaidizi wapi?

·         Hospitali iliyo karibu nawe itakutolea usaidizi. Watakuwa na dakitari ambaye atakuchunguza na atakushauri kuhusu uchunguzi wowote ama matibabu ambayo unaweza kuhitaji kutumia.

Tambua uwongo unaozungumziwa kuhusu Kifafa

“Kifafa ni aina ya ulemavu kwani huathiri utenda kazi wa ubongo”
·         Ulemavu ulielezewa vizuri na Shirika la Afya Duniani mnamo mwaka wa 1976. Unatofautisha dhana tatu ambazo hutumiwa sana na unadhihirisha baina ya kudhoofika, ulemavu na upungufu.
·         Kudhoofika ni upungufu wowote ama hali ya akili isiyo ya kawaida (saikolojia), utenda kazi wa mwili (fiziolojia) ama muundo wa mwili wa binadamu (anatomia) ama utenda kazi; Ulemavu ni kikwazo ama kukosa uwezo (unaotokana na upungufu) wa kufanya shughuli kwa njia inayochukuliwa kuwa ya kawaida kwa 
binadamu; Upungufu ni kasoro inayotokea kwa mtu kwa sababu ya kudhoofika ama ulemavu ambao huzuia kutimilika kwa wajibu unaochukuliwa kuwa wa kawaida (kwa kutegemea umri, jinsia na mambo ya ushirikiano wa jamii na utamaduni) kwa mtu huyo.
·         Kifafa ni matokeo ya utenda kazi wa ubongo usio wa kawaida ama kudhoofika kwa utenda kazi wa ubongo.Huathiri utenda kazi wa ubongo kwa kuendelea na kuwacha. Kuna hali zingine ambazo huwa na athari inayoendelea na ya mda mrefu. Hizi hali hutokea kama kutoona vizuri, kutowiiana vizuri,kuongea pole pole,kutoweza kumakinika na kusahausahau. Hali hizi huitwa ulemavu ama taahira ya akili.
·         Ugonjwa wa kifafa unaweza kumshika mtu mwenye hali/ulemavu mwingine. Unaweza pia kutokea tu wenyewe. Mgonjwa wa kifafa ambaye yuko chini ya matibabu na anafuatiliwa mara kwa mara anaweza kutimiza majukumu yake kama mtu yeyote mwingine. 
Katika hali hii hadhaniwi kuwa na ulemavu wowote. Ikiwa kuzirai kunakosababishwa na kifafa kumeongezeka na kunamzuia mtu kufanya kazi yake ya kawaida, basi hili huchukuliwa kuwa ulemavu.

“Kifafa hutokea kwa sababu ya kupagawa na mapepo”

0 comments:

Post a Comment