Thursday 1 May 2014

HIZI NDIO ALAMA/ISHARA/DALILI ZA MWILI WAKO ZITAKUFAHAMISHA OVULATION IMEWADIA



 
OVULATION ni hali ya kutoka kwa yai la kike baada ya kukomaa kutoka kwenye follicle baada ya kukua na kukomaa katika ovary. Hali hii hutokea katika hali ya kawaida katika siku ya 14 katika mzunguko wa siku 28.

Alama/dalili hizo
za Ovulation si ngumu kuzitambua, iwapo
utafahamu unatafuta alama gani. Kuna
baadhi ya alama za mwili
 
Zinazokutahadharisha kwamba Ovulation
iko njiani, hivyo kuweza kukusaidia
kupanga vyema muda wa kujamiiana kwa
ajili ya kupata mimba.
Alama/ dalili nyinginezo
zinakufahamisha kwamba Ovulation
imewadia au imeshapita. Ingawa alama hizo
ziko nyingi na nitazungumzia baadhi ya
hizo, lakini usifikiri kwamba unatakiwa
utumie zote, kwani kufanya hivyo kunaweza
kukuchanganya.
 
Iwapo hutoona alama zozote za Ovulation
au iwapo siku zako za mwezi hazina
mpangilio maalum, ni bora umuone daktari
ambaye atakusaidia zaidi.

1.Mabadiliko ya joto lako la Mwili
Tunaweza kusema kuwa Joto lako la mwili
au (Body Basal Temperature) ndio alama/ dalili
maarufu inayotumiwa na wanawake wengi
ili kufahamisha kwamba Ovulation
 
imewadia pale wanapotaka kubeba mimba.
Hii ni kwa sababu joto lako la mwili
huongezeka kwa kiasi kidogo na huendelea
 
kuongezeka baada ya Ovulation. Ongezeko
hilo la joto husababishwa na homoni ya
progesterone, ambayo huongezeka sana
punde baada ya Ovulation.
Kwa kujipima
joto lako la mwili na kuandika chati ya
mabadiliko hayo unaweza kufahamu
ongezeko hilo la joto lako la mwili.
Unahitajia kipimamoto kwa ajili ya
 
kufanikisha suala hilo. Zipo pimajoto
maalum kwa ajili hiyo lakini unaweza
kutumia pimajoto ya kawaida pia. Hakikisha
unapima joto la mwili wako asubuhi baada
ya kuamka na uhakikishe huna homa,
hukukosa usingizi, hukunywa pombe, si
 
mgonjwa wala huna wasiwasi na fikra
nyingi. Ni bora ufanye hivyo kwa mizunguko
kadhaa ya siku zako ili uweze kuijua vyema
chati ya mabadiliko ya joto la mwili kwa
mujibu wa mzunguko wako wa mwezi.

Ingawa njia hii haiainishi moja kwa moja
kuwa Ovulation imewadia, lakini joto la
mwili huongezeka kidogo kabla ya kipindi
hicho na huongezeka kwa kwa degree 0.4
hadi 0.6 baada tu ya kumalizika Ovulation.
 
Kuongezeka joto kwa kiasi kikubwa baada
ya Ovulation huendelea hadi siku
utakayopata siku zako ambapo hupungua
na mzunguko wako wa mwezi huanza tena.
Iwapo utakuwa umepata mimba joto lako la
mwili litaendelea hivyo hivyo kuwa juu.
Kwa
 
kuwa mabadiliko ya joto hutokea wakati wa
Ovulation iwapo unajaribu kubeba mimba,
kufuatilia mabadiliko hayo kwa muda
 
usiopungua miezi miwili ni jambo la
dharura ili uweze kujua wakati wa Ovulation
ambapo una uwezekano mkubwa wa
kubeba mimba.

2.Mabadiliko ya majimaji ya ukeni

Wakati Ovulation inakaribia majimaji ya
ukeni hubadilika pia kwa kiasi na hali. Ikiwa
hakuna Ovulation majimaji ya ukeni huwa
yanayonata au kama kremu au hukosekana
 
kabisa. Wakati Ovulation inakaribia majimaji
ya ukeni huongezeka na huwa katika hali ya
majimaji na wakati mwingine huwa rangi
nyeupe kama ya yai bichi. Iwapo utapima
kwa vidole vyako huvutika kwa inchi au
zaidi kati ya vidole vyako.

Ni bora nikumbushe hapa kwamba, kuangalia
wakati unaweza kuwa na majimaji ya ukeni
yanayofanana na ya wakati wa Ovulation
hali ya kuwa huko katika Ovulation. Hali hiyo
ni ya kawaida kwa watu wenye PCOS.
Kutumia dawa za Clomid au Antihistamin
 
huweza kufanya majimaji ya ukeni yakauke
na hivyo kuwa vigumu kutumia njia hii ili
kujua ni zipi siku zennye uwezekano
mkubwa wa mimba. Njia hii huhesabiwa
kuwa yenye itibari zaidi.

3.Ongezeko la Matamanio
Inaonekana kuwa maumbile nayo
hutusaidia kujua ni siku gani tunaweza
kubeba mimba! Wataalamu wameonyesha
(jambo ambalo pengine wengi
wameshalihisi) kwamba wanawake
 
wanapokuwa katika siku zenye uwezekano
mkubwa wa kupata mimba, matamanio yao
ya kufanya mapenzi huongezeka. Hizo ni siku chache
kabla ya
kujiri Ovulation, ambapo ndio wakati
unaofaa wa kujamiiana iwapo unataka
kubeba mimba.

Hata hivyo njia hii si ya kutumainiwa sana
kwani baadhi ya hali kama vile
msongamano wa mawazo, fikra nyingi na
wasiwasi huweza kupunguzaa matamanio.
Au mtu anaweza akahisi matamanio katika
muda wote wa mzunguko wa mwezi.


4.Mabadiliko ya Ukeni:
Kama ambavyo majimaji ya ukeni
yanavyobadilika wakati wa Ovulation, uke
nao (cervix) hubadilika wakati wa kukaribia
Ovulation. Wakati huo uke husogea mbele,
huwa laini na hufunguka zaidi.

 
 5.Maumivu kidogo katika Matiti:
Baadhi ya wanawake wakati wanapokaribia
Ovulation au baada ya hapo matiti yao huwa
 
na maumivu kidogo. Suala hili huhusiana na
mabadiliko ya homini mwili ambazo
hujitayarisha kwa ajili ya mimba. Hata hivyo
njia hii sio yenye kutegemewa sana kwani
 
maumivu ya matiti huweza kusababishwa
na masuala mengine. Pia maumivu ya matiti
hutokea kabla ya hedhi au baada ya kutumia
baadhi ya dawa za kusaidia uzazi.

Alama/ dalili nyinginezo
Baadhi ya wanawake huhisi maumivu
kidogo ya tumbo
ambayo baadhi huyaita
Middle Pain. Maumivu hayo kwa kawaida
hutokea upande ule yai linapotoka yaani
upande wa Ovulation. Maumivu hayo
 
hutokana na mwendo wa yai wakati
linapopenya kwenye mirija. Maumivu hayo si
ya kuendelea na wala si makubwa na huisha
haraka. Hali hiyo huweza kutokea mara
kadhaa katika siku za Ovulation.
Kuna
baadhi ya alama kama vile baadhi ya
wanawake huhisi kichefuchefu, gesi,
kukojoa mara kwa mara na maumivu wakati
wa kujamiina,
hali ambayo haitokei kwa
watu wengi. Pia kuna baadhi ya vifaa
vinavyopaatikana katika maduka ya dawa
 
katika baadhi ya nchi ambavyo huweza
kukusaidia kujua wakati wako wa Ovuation
umewajia, vifaa hivyo hujulikana kama
'Ovulation Kit"

La muhimu ni kufahamu kuwa wanawake
hutofautiana katika kupata alama hizi,
kwani kuna baadhi wanaweza wakapata
 
baadhi ya alama hizi na wengineo wakapata
nyinginezo. Kuuelewa vyema mwili wako ni
jambo zuri linaloweza kukusaidia kuzijua
siku zako la Ovulation na hivyo kuweza
kujua siku zako za kubeba mimba.

0 comments:

Post a Comment