Saturday, 3 May 2014

ASALI, ASALI NI ZAIDI YA CHAKULA

 
ASALI inafahamika kwa muda mrefu
kama chakula muhimu ambacho pia
kinasaidia sana katika kupambana na
magonjwa mbalimbali na matatizo
yatokanayo na uzee.
 
Kwa mujibu wa tafiti mpya za
wataalamu wa madawa lishe na vifaa
tiba, imedhihirika kwamba, uwezo wa
asali kutibu unaweza kuongezeka
maradufu kama itachanganywa na
mdalasini.

Aidha, uchunguzi wa kila wiki
unaofanywa na jarida la World News
kuhusu tiba unasema, wataalamu wa
madawa yatokanayo na mimea,
imeonekana kwamba kuna dazani
nyingi za umuhimu wa asali na
mdalasini katika kujenga afya bora.

 
Asali ikishachanganywa na mdalasini
pamoja na mafuta ya vuguvugu ya
mzaituni, hutoa kichocheo maridhawa
cha kuotesha nywele kinachotumika
katika dawa ya Dork.

Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa
kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa
dakika 15. Kwa mujibu wa watafiti wa
madawa tiba, Dk Alexander Andreyed na
 
Eric Vogelmann, madhara yaletwayo na
vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza
kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa
matumizi ya mara kwa mara ya chai
iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko
wa asali na mdalasini.

Ugunduzi wao huo, uliyakinishwa vema
kwenye jarida mashuhuri
linalozungumzia masuala ya tiba la
nchini Denmark la Julai 1994. Uchunguzi
mwingine pia umeonesha kwamba
matumizi ya kila siku ya asali
yanapunguza viwango vya lehemu
mwilini.

Asali inatajwa pia kuwa dawa ya jino,
inaponya pia ngozi iliyoharibika, ni
dawa asilia ya shinikizo la juu la damu ni
kiungo muhimu katika utengenezaji wa
asilimia kubwa ya madawa mmimiko na
asilimia kubwa ya vipodozi na mafuta ya
kupaka.

 
Ugonjwa wa mafua ambao huwakera
na kuwanyima watu wengi raha
imegundulika na wataalamu kwamba
 
hupungua na kupotea kabisa ikiwa
watatumia kijiko kimoja cha chai cha
asali vuguvugu iliyochanganywa na robo
kijiko cha chai cha mdalasini. Mtafiti
 
mmoja wa Hispania imethibitisha
kwamba, aina ya dawa moja asilia
iliyofanikiwa kuharibu vimelea viletavyo
mafua ilitengenezwa kwa kiwango
kikubwa na asali.

Mchanganyiko huo pia ni mahususi
katika kusaidia kupunguza na kuondoa
chafya na kuvimba kwa koo. Asali
inaaminika pia huamsha hamu ya tendo
la ndoa. Wale ambao mambo katika
eneo hilo si mazuri wanashauriwa
angalau kunywa vijiko viwili vya mezani
 
kila siku kabla ya muda wa kulala usiku.
Kuna wakati asali ilipigwa marufuku
kwa makasisi katika baadhi ya dini za
Mashariki mwa dunia ili isiwe sababu ya
kuwaongezea mihemko.

Asali inaaminika kuwa dawa ifaayo
katika kuondoa mchafuko wa tumbo
pamoja na kichefuchefu. Ukiwa katika
 
kadhia hiyo, unashauriwa kuongeza
kiasi kidogo cha mdalasini na asali
kwenye chai ama maji, itapunguza hali
hiyo na maumivu yaletwayo na vidonda
vya tumbo.

Utamaduni wa kula asali pamoja na
mdalasini, huweza kuondoa mchafuko
wa tumbo na utumbo uletwao na gesi
kwa mujibu wa uchunguzi mahsusi
uliofanywa huko India na Japani kwa
 
miaka mingi. Unaweza kukinga kupata
ugonjwa wa moyo na kuzuia
mkusanyiko wa mtandao wa mafuta
kwenye mishipa ya damu kwa kula asali
na mdalasini mara kwa mara wakati wa
kifungua kinywa.

Kula mkate uliopakwa asali kijiko kimoja
cha mezani kila siku nyuzi nyuzi zake ni
muhimu pia kiafya. Tiba hii, iliweza
kupunguza kuganda kwa mishipa ya
 
damu kwa asilimia 74 ya wagonjwa
waliofanyiwa utafiti. Shinikizo la damu,
pamoja na matatizo yaambatanayo na
maumivu ya kifua na kizunguzungu
 
yalitoweka kutoka kwa wagonjwa
wengi wiki chache tu baada ya watafiti
wa Kiitaliano kuwapa dozi za mara kwa
mara za asali iliyochanganywa na
mdalasini.

Kinga ya mwili, itaongezeka mara tatu
zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara
asali na mdalasini kwa pamoja,
wataalamu wanasema. Utafiti wa kitiba
unaonesha kwamba, asali ina hazina
 
kubwa ya virutubisho na madini pamoja
na michanganyiko mingine iondoayo
magonjwa pamoja na kinga, itolewayo
na chembechembe nyeupe za damu,
 
husaidia kuzuia magonjwa pamoja na
kuharibu vimelea virusi na bakteria.
Vijiko viwili vya asali iliyonyunyiziwa
mdalasini kabla ya mlo, huondoa
kiungulia pia. Inasemekana kuwa,
 
unaweza kuishi hadi miaka 100
ukifurahia maisha ya afya bora na
madhubuti kwa kunywa kila siku
kikombe baridi cha chai iliyowekwa
mdalasini na asali.
Kutengeneza kinywaji
hiki kitamu, weka vijiko vinne vikubwa
vya mdalasini katika vikombe vitatu vya
maji na koroga kwa dakika 10, kunywa
robo kikombe kutwa mara tatu au nne,
watafiti wanasema.

Asali ni tiba rafiki na asilia kwa watu
wenye shida ya chunusi. Ili kutibu tatizo
hilo watafiti wanasema changanya vijiko
vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja
cha mdalasini na pakaa kwenye chunusi.
 
Uwezo wa asali wa kuua bakteria
utaufanya uso wako kuwa kawaida
katika muda wa wiki mbili pekee.
Asali, wanasema inairudisha ngozi
iliyoharibiwa na wadudu waharibifu
 
kama dondola, washawasha na hata
ngozi iliyopata madhara kutokana na
kuungua moto. Pakaa asali na mdalasini
moja kwa moja kwenye sehemu
zilizoathirika na rudia wakati mwasho
unapokuathiri. Rudia tena hadi uvimbe
unapotoweka.

Utafiti uliofanywa karibuni nchini
Australia na Japan, umeonesha kuwa,
asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya
mgonjwa kwa mtu anayetumia madawa
ya kutibu saratani. Katika utafiti
uliofanywa kwa wagonjwa waliokuwa
wanaugua kwa kiwango kikubwa
 
saratani ya mifupa na tumbo, wale
waliokuwa wakitumia kila siku dozi za
asali na mdalasini, walionesha kupata
nafuu maradufu kuliko wale waliokuwa
wakitumia madawa ya saratani pekee.
 
“Tuliwapa kijiko cha mdalasini na asali
kutwa mara tatu kwa mwezi,” anasema
Dk Hiroki Owatta. Upo ushahidi mpya
kwamba, sukari asilia zilizopo kwenye
asali, zina uwezo wa kuongeza nishati
mwilini. Zikitumika ipasavyo, sukari hizi
zinaweza kuwasaidia wazee na
wengine wanaosumbuliwa na uchovu.

Wataalamu wanapendekeza
kuchanganya nusu kijiko cha asali katika
nusu bilauri ya maji kisha nyunyizia
mdalasini na kunywa masaa mawili
baada ya kuamka asubuhi. “Kunywa
 
tena saa 9:00 alasiri wakati nishati
(nguvu) inapoanza kushuka,” anashauri
Dk Milton Abbozza ambaye kazi zake
kuhusu asali na mdalasini kama
kichocheo cha nishati mwilini
zinatambulika kimataifa.

Asali inao uwezo mkubwa wa
kupunguza na kuponya miguu
iliyopasuka kwenye kisigino. Chua asali
na mdalasini vuguvugu katika miguu au
 
nyayo zilizoathirika baada ya siku ndefu
na kazi au baada ya mazoezi marefu.
Rudia kila siku asubuhi halafu, osha
nyayo zako kwenye maji baridi na vaa
viatu.

Baadhi ya watu Marekani ya Kusini,
wanasukutua maji ya vuguvugu
yaliyowekwa asali na mdalasini kila
asubuhi ili kufanya harufu mdomoni
 
kuwa nzuri na safi kiasilia. Katika Asia ya
Kusini Mashariki, watu hutumia kijiko
cha mdalasini na asali ili kuondoa harufu
mbaya mdomoni (halitosis).

Wataalamu wanaamini kwamba, uwezo
wa kuua bakteria uliopo kwenye asali
ndiyo unaopigana na harufu mbaya
itokayo mdomoni. Dozi za kila siku za
asali na mdalasini, hufanya hali ya
 
usikivu murua kwa wanafunzi wawapo
darasani au viongozi mkutanoni kama
ilivyogunduliwa na Wagiriki wa zamani.
Hiyo ndiyo asali. Ni chakula na dawa.

Lakini inayozungumzwa hapa ni asali
mbichi ambayo inapatikana kwa wingi
Tanzania, lakini tatizo ni kubwa ipo pia
feki inayouzwa kama mbichi!

Makala
haya, yametayarishwa kwa msaada wa
Mtandao, kwa kushirikiana na Neema
Herbalist ya jijini Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment