Wednesday 23 April 2014

FUKUZA VIDONDA VYA TUMBO FANGASI NA MAPUNYE





NI mpapai! Mara nyingi nimekuwa nikiongea kuwa Tanzania tuna miti mingi sana kiasi kwamba bado hata robo yake hatujaijua majina yake, achilia mbali kitu muhimu kama kujua matumizi.

Mungu alipomuumba binadamu na kumleta duniani, alihakikisha hapatwi na maradhi kama fangasi, madonda tumbo, ukurutu, mapunye n.k, kwa kuumba na mpapai. Mungu hakuumba hata zahanati pale Bustani ya Eden, badala yake bustani ile iliumbwa ili wakila vilivyomo basi iwe ni hoteli washibe, hospitali wajitibie, saluni wawe warembo n.k.
Mpapai ulikuwepo. Mpapai toka mizizi, mti wake, matunda, majani mpaka maua yake yanabeba maji na utomvu ambao nakuhakikishia msomajikama utayadondoshea maji hayo katika sehemu iliyoshambuliwa na maradhi niliyotaja hapo juu, basi hutarudia kupaka tena maji hayo maana kesho yake tu utaona mambo yamekuwa sawa.

VIDONDA VYA TUMBO:
Kula kipande cha papai kisichoiva vizuri kila siku alfajiri, ukimaliza shushia na mbegu moja tu ya kitunguu swaumu. Hakikisha unazidisha kiwango cha kunywa maji siku zote utakazo jitibia vidonda hivyo, na ikifika siku 13 hadi 16 utanipigia simu kunitaarifu kuwa vidonda vimepona.

Kama kipato chako ni kidogo na kupata papai kila siku ni gharama, basi usikonde. Chuma majani mawili ya mpapai kisha katakata kama mboga ya kupikwa, tia katika chupa kubwa ya lita mbili za maji na kunywa kutwa nzima kidogo kidogo hadi yaishe. Waweza kutia vipande vya mapapai machanga yaliyokatwakatwa pia badala ya majani.

FANGASI NA MAPUNYE

Hili ndiyo tatizo la watu wengi hapa Dar na popote kwenye joto kali. Kama umeshindwa kuvaa viatu kwa sababu ya fangasi na mapunye wala usikonde. 
Fua soksi zako, suuza na maji safi, chuma majani ya mpapai mawili au matatu fikicha pamoja na soksi kabla hujazikamua. 
Zikishafikichika na majani basi anika hivyo hivyo. Zikikauka, pukuta majani kisha vaa soksi zako endelea na shughuli zako maana kama fangasi wote watakufa na wala soksi hazitatoa harufu tena.

MAPUNYE KICHWANI
Huu ni ugonjwa wa watoto zaidi. Watoto wanasumbuliwa sana na mapunye, ukurutu, vipele na fangasi kwapani na kichwani. Chuma papai changa, mpake mtoto utomvu katika mapunye mara moja tu yataisha. Yasipoisha,rudia hata mara tatu lakini ukiona hayakauki, basi naomba unitafute nikuelekeze la kufanya maana maradhi mengine huja na matatizo hayo hivyo atakuwa anaumwa zaidi ya mapunye na fangasi na atahitaji tiba kali zaidi. 

Angalia. Kama mtoto ni mdogo wa miaka mitatu kushuka chini basi usimpake utomvu, badala yake mpake masalia ya maganda ya papai bivu maana utomvu huponyesha haraka lakini ni mkali na unaleta maumivu ambayo mtoto mdogo hatavumilia.
Mpapai umeumbwa na unaishi na binadamu kwa ajili ya kazi hii tu. Tuweke akilini kuwa mimea ni viumbe hai visivyotembea lakini vipo kwa ajili yetu hivyo tuvipende na kuvithamini viumbe hivi.

Tuviulize majina yao, tuulize pia kila mmea una kazi gani hapa duniani n.k. Mpapai umeumbwa mahususi kuwa sabuni ya mwili nje na ndani. Ukiwa na tatizo lolote la shambulio la ngozi basi kimbia, chuma mpapai fikicha utoe majimaji hapo kwenye tatizo na mara moja utaona mafanikio tena kwa haraka mno.

0 comments:

Post a Comment