Thursday 2 March 2017

TIBA YA MARADHI YA SARATANI YA DAMU (LEUKEMIA)


SARATANI YA DAMU (LEUKEMIA) Leukemia ni Saratani
inayoshambulia tishu za mwili zinazohusika na utengenezaji wa damu zikiwemo supu ya mifupa (bone marrow) na mfumo wa lymph
(lyphatic system). Kwa maneno rahisi, leukemia humaanisha saratani ya damu. Kuna aina mbalimbali za leukemia, nyingine zikiathiri watoto na nyingine zikiathiri zaidi watu wazima.
Kwa kawaida leukemia huanzia kwenye chembe nyeupe za damu yaani white blood cells, ambapo mwili huzalisha kiwango kikubwa cha seli zenye maumbo mabaya ambazo hazina uwezo wa kufanya kazi zake sawasawa. Kazi ya chembe nyeupe za damu ni kulinda mwili dhidi ya vimelea waletao maradhi mbalimbali.
Leukemia husababishwa na nini
Kama zilizo kwa aina nyingi za saratani, mpaka sasa chanzo halisi cha leukemia hakijulikani. Hata hivyo, wanasayansi wanadai kuwa leukemia hutokea kutokana na mkusanyiko wa vyanzo mbalimbali vikiwemo vinavyohusu sababu za kinasaba (genetic factors) na kimazingira.
Kwa ujumla, leukemia hutokea pindi chembe nyeupe za damu zinapobadilika muundo wake wa kinasaba yaani viasili vyake vya
DNA, ambavyo kwa kawaida hubeba maelekezo yanayoifanya seli yeyote ya kiumbe hai iweze kuishi, kutenda kazi zake, kujizaa na hata kufa, vinapobadilika maumbile na muundo wake kutokana na
sababu mbalimbali. Kitendo cha kubadilika kwa maumbile na muundo wa DNA hujulikana kama mutation. Ndiyo kusema basi, seli yeyote iliyopatwa na tatizo hili huwa na tabia ya kukua kwa haraka na kujizaa (kujigawa) kwa kasi zaidi kuliko kawaida, na pindi
inapofikia muda wake wa kufa seli hiyo hugoma kufa badala yake huendelea kujizaa zaidi hatimaye
kusambaa kwa wingi katika mfumo mzima wa damu, hali inayosababisha saratani ya damu.
Je, kuna vihatarishi vya leukemia
Ndiyo vipo! Pamoja na kwamba chanzo halisi cha saratani ya damu hakijulikani, lakini kuna mambo ambayo humuongezea mtu hatari ya kupata ugonjwa wa saratani ya damu.
Mambo ambayo yanaweza kuongeza uwezekano wa kupata saratani ya damu ni pamoja na:
Historia ya matibabu ya saratani hapo kabla: Watu ambao wamekuwa kuwa na aina nyingine za saratani hapo awali, na wakati wa matibabu wakapewa tiba ya mionzi au madawa makali ya
saratani, wapo katika hatari kubwa ya kupata saratani ya damu kwa sababu baadhi ya dawa hizi pamoja na mionzi huwa na tabia ya kuathiri pia seli nyeupe za damu pamoja na tishu zinazotengeneza seli hizo.
Kuwa na magonjwa mengine ya vinasaba: Ingawa haieleweki sawasawa uhusiano wake ulivyo, kuwa na baadhi ya magonjwa ya kinasaba kama vile ugonjwa wa Down syndrome, yasemekana huongeza uwezekano wa muathirika kuugua pia ugonjwa wa saratani ya damu.
Baadhi ya magonjwa mengine ya damu: Watu wenye magonjwa mengine ya damu kama vile ugonjwa wa damu unaoshambulia tishu za supu ya mifupa na kuzifanya zizalishe seli nyingi za damu bila uwiano unaotakiwa yaanimyelodysplastic syndromes, huongeza pia uwezekano wa mtu kuugua saratani ya damu.
Kupigwa na kiasi kikubwa cha mionzi: Watu ambao wamewahi kupigwa na kiasi kikubwa cha mionzi kama vile mlipuko wa mabomu au kulipuka kwa vinu na mitambo ya nuklea (nuclear reactors), wana hatari kubwa zaidi ya kupata saratani ya damu pamoja na saratani nyingine.
Kupigwa/kutumia baadhi ya kemikali: Watu waliowahi kukumbana na baadhi ya kemikali kama vile benzene au zile zinazotumika kwenye viwanda vya kuyeyusha vyuma au kutengeneza
magurudumu au mabomba ya plastic, nao pia wapo katika uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya damu.
Uvutaji sigara: Jambo hili pia huongeza uwezekano wa kupata aina mojawapo ya saratani ya damu.
Kuwa na historia ya ugonjwa huu katika familia: Watu ambao, baadhi ya ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu, nao pia wana uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya damu. Hata hivyo, hii haina maana kwamba leukemia inaambukizwa isipokuwa kuna uhusiano wa kifamilia tu katika kusababisha ugonjwa huu.
Jambo moja la kufahamu ni kuwa, wapo watu wengi ambao wamewahi kukumbana na vihatarishi nilivyovieleza hapo juu bila kupata leukemia, kadhalika wapo waliopata leukemia bila kukumbana na kihatarishi hata kimoja kati ya hivi.
MATIBABU YA SARATANI YA DAMU
Matibabu hutolewa kulingana na hatua ya ugonjwa ilipofikia.
Kwanza safisha damu yako
Zipo dawa nyingi za asili ambazo hutibu kansa , dozi ni kulingana na aina ya kansa na stage ilipofikia
Mfano Majani ya mstafeli yana uwezo wa kuziua seli za kansa aina yeyote mara 10,000 ya mionzi.
Chukua majani ya mstafeli yaasafishe vizuri kisha yaponde kwa Blenda Tia ndani yake glasi 2 za maji kutengeza juisi yake
Mgonjwa anywe nusu kikombe kutwa mara tatu siku 90

1 comments:

  1. I am FRED and i want quickly recommend DR NCUBE for a Job well done by
    curing me from the genital herpes disease that have be giving me sleepless night. if you want to contact him, Simply do that via email drncube03@gmail.com or 
    call/whatsapp +2348155227532
    he also have #herbs for
    #hiv/aids
    #cancerdisease 
    #fibroid 
    #diabetes

    ReplyDelete