Thursday 11 August 2016

UNAWEZA KUPONA MARADHI PASIPO NA KUTUMIA DAWA YA AINA YOYOTE ILE? PART 2



Hatari za kutumia dawa vibaya

Hii ni orodha ya makosa ya kawaida tunayofanya tunapotumia madawa ya kisasa. Matumizi mabaya ya madawa yafuatayo yanaleta vifo kila mwaka, kuwa mwangalifu Chloramphenical (chloromycetin) -Kwa bahati mbaya, dawa hii hupendelewa sana kutumiwa kwa magonjwa madogo madogo kama vile kuharisha. Hii, ni hatari sana.



- Dawa hii inatumika kutibu magonjwa kama vile homa ya matumbo. Isitolewe kwa watoto wachanga.

Oxtocin(pitocin) pituitrin na Ergonovine (Ergotrate) - kwa bahati mbaya wakunga hutumia dawa hizo 

kuharakisha kuzaliwa kwa mtoto au kumpa nguvu mzazi wakati akiwa na uchungu wa kujifungua.
Matumizi ya namna hii yana hatari sana. Unaweza kumwua mama au mtoto. Zitumie tu, kwa kuzuia kutoka damu baada ya mtoto kuzaliwa.

Sindano za dawa: Imani kuwa sindano ni bora kuliko vidonge si ya kweli. Mara nyingi dawa za kunywa zinafanya kazi vizuri zaidi kupita sindano. Pia, dawa nyingi zitolewazo kwa sindano huhatarisha maisha kuliko za kunywa. Matumizi ya sindano lazima yapunguzwe.

- Penisilini: Penisilini hufanya kazi kwa magonjwa fulani ya kuambukiza. Ni makosa kutumia dawa hii kwa shida za kustuka misuli, kujiponda, aina yoyote ya maumivu au homa.

Kwa kawaida, majeraha yoyote ambayo hayakuchubua ngozi, ijapokuwa kuna uvimbe mkubwa ni vigumu vijidudu kuingia kwa hivyo hakuna haja ya kutumia penisilini au dawa nyingine yoyote ya kuua wadudu.

Penisilini ina hatari kwa watu wengine. Kabla ya kuitumia lazima ufahamu hatari zake na namna ya kuzizuia.
Sindano za Penisilini na Streptomisini (zina majina mengine mengi)- Dawa hizi hutumika sana na mara 

nyingi kwa magonjwa yasiyohusika. Dawa hizi zisitumiwe kwa mtu aliye na mafua kwa sababu haziponyeshi ugonjwa wa mafua au fluu, zinaweza kusababisha matiti makubwa wakati mwingine, kuzimia au kifo, zikizidi 

kutumiwa ovyo ovyo, zitafanya magonjwa kama kifua kikuu na magonjwa mengine ya hatari yasiyoweza kuponyeka.

Vitamini B12; Dawa hii haisaidii kutibu ukosefu wa damu au udhaifu isipokuwa kwa wagonjwa wachache tu. Inaweza kutumika tu, kama mganga ndiye karuhusu baada ya vipimo vya damu. Karibu magonjwa mengi ya damu yanatibiwa kwa kutumia vidonge vya madini ya chuma (Ferrous Sulphate).

Vitamini Nyinginezo: Kwa kawaida, usidunge sindano za vitamini. Sindano hizo zina hatari, ni ghali na hazifanyi kazi yake vizuri kama vidonge.

Bahati mbaya, watu wengi hupoteza fedha zao kwa kununua dawa za maji ambazo zinasemekana zina vitamini. Ukweli ni kwamba nyingi kati ya dawa hizo hazina vitamini. Hata kama zingekuwa navyo ni afadhali kununua chakula kingi na kilicho bora.

Kujenga na kuhifadhi mwili kunahitaji vyakula kama mayai, nyama, matunda, mboga za majani na nafaka; ambavyo vyote vina vitamini na nguvu za kukuza mwili. Mtu mwembamba na aliyedhoofika akipewa chakula 

bora mara kwa mara, kitamsaidia sana kuliko kumpa vitamini na chumvi chumvi.
Mtu anayekula vizuri hahitaji nyongeza ya vitamini.
Njia bora ya kupata vitamini.


Kumbuka:
Waganga na madaktari wengine, hutoa dawa wakati hazihitajiki mara kwa mara ni kwa sababu wanafikiri kuwa, wagonjwa wanatazamia kupata dawa na hawataridhika kama hawatapewa.

Ni vizuri kuwaomba daktari au mganga wako dawa wakati unapohitaji tu, la sivyo, unaweza kuharibu afya yako.

Tumia dawa ukiwa na hakika kuwa inahitajika na ukiwa na huku ikiwa na uhakika namna ya kuitumia.


KALSIUM

Kuna hatari kubwa sana kumpiga mgonjwa sindano ya Kalsium kwa kutumia mshipa wa damu. Kama njia hii inatumika, ni lazima dawa inyunyizwe taratibu sana. La sivyo, itaua mara moja. Ukipiga matakoni, inaweza kusababisha jipu.
Usipige sindano ya kalsium kabla hujapata ushauri kutoka kwa mganga.


KUMBUKA:

Huko Mexico na katika nchi nyingine ambako watu hutumia sana mahindi au vyakula vilivyotayarishwa na kuchanganywa na chokaa, haifai kutumia sindano, au vidonge vya kalsium (kwani mara nyingi hutolewa ili kurejesha nguvu ya mwili au kusaidia kukua kwa mtoto).
Mwili hupata kalsium inayohitajika kutokana na chokaa.

Kulisha kwa kutumia mishipa ya damu

Katika sehemu nyingine, watu walio na ukosefu wa damu au wadhaifu sana, hutumia fedha zao hadi senti ya mwisho kwa ajili ya kuwekewa dawa za maji katika mishipa yao ya damu.
Wanaamini kuwa kufanyiwa hivyo, kutawafanya wawe na nguvu za kuwa na damu safi. Lakini, wanajidanganya.

Hakuna kitu chochote katika dawa hii inayotolewa kupitia katika mshipa wa damu isipokuwa, ni maji matupu pamoja na chumvi chumvi au sukari. Haiongezi nguvu kuliko kipande kikubwa cha pipi na inafanya damu iwe nyepesi na sio nzito kama vile wanavyofikiria.

Haiponyeshi upungufu wa damu wala kumfanya mnyonge kuwa mwenye nguvu.
Na kama inatolewa na mtu asiye na ujuzi, kuna hatari ya kuingia vijidudu vibaya katika damu, na hii inaweza kumwua mgonjwa.

Dawa hii itumike tu, kwa mtu ambaye hawezi au haruhusiwi kula au ana ukosefu mkubwa wa maji mwilini.
Kama mgonjwa anaweza kumeza, mpe maji yaliyochanganywa na sukari pamoja na chumvi kiasi kipatacho painti mbili(tazama vinywaji vya kurudisha maji) - Dehydration drink, itamsaidia sana kuliko ukimpa kwa kupitisha katika mshipa wa damu.

Kwa wale ambao wanaweza kula, wanaweza kupata nguvu za kutosha kwa kula chakula bora kuliko kutumia aina yoyote ya dawa za maji zinazolishiwa kwa njia ya mishipa ya damu.
Kama mgonjwa anaweza kumeza na kuyahifadhi maji tumboni


Dawa za kuharisha na kulainisha tumbo
Wakati wowote kuna hatari ikiwa utampa mtoto au mtu mzima aliye mdhaifu mwenye ukosefu wa maji mwilini au mwenye tumbo la kusokota, dawa ya kuharisha au kulainisha tumbo.

Kwa bahati mbaya, watu wengi wana imani kuwa dawa ya kuharisha inamrudishia mtu afya nzuri au inasafisha vitu vyote mwilini. Sura ya kwanza imeelezea kuwa dawa za kuharisha au dawa za kulainisha tumbo, zinaleta matatizo zaidi kuliko inavyotegemewa.



Ni Wakati gani dawa zisitumike?

Watu wengi wanaamini kuwa kuna vitu ambavyo hawawezi kufanya au kula wakati wanapotumia dawa.
Kwa sababu hii, wanaweza kuacha kutumia dawa ambazo inabidi watumie.
Ukweli ni kwamba hakuna dawa ambayo inaweza kuleta madhara eti kwa sababu imenywewa wakati wa kula chakula fulani- hata kama iwe ni nyama ya nguruwe, pilipili, mapera, machungwa au chakula cha aina yeyote.

Lakini, vyakula vyenye mafuta au viungo, vinaweza kukuletea tatizo la tumbo hata kama hukumeza dawa. Kuna dawa nyingine zinaweza kudhuru iwapo mtu atakunywa pombe.

Kuna nyakati ambapo si vizuri kutumia dawa, kwa mfano:

- Mjamzito au mama mwenye kunyonyesha, hana budi kuepuka dawa ambazo si lazima atumie (lakini anaweza kutumia vitamini na vidonge vya damu bila kudhuru chochote).
- Kwa upande wa watoto wachanga ni vizuri kuwa mwangalifu sana kwa kuwapa dawa.

Ikiwezekana na afadhali upate ushauri wa waganga kabla ya kuwapa dawa yoyote.
Hakikisha huzidishi kipimo.

- Mtu yeyote ambaye amekwisha pata matatizo kama kuvimba, kuwashwa, na kadhalika, baada ya kutumia penisilini, Ampisilini, Sulfonamide au dawa nyingine zozote, inambidi aache kabisa kutumia dawa hiyo kwa muda wa maisha yake yote kwa sababu inaweza kumletea hatari kubwa.

  • Watu wenye vidonda tumboni au kiungulia, lazima waepuke dawa zilizo na aspirini.
 Kuna dawa maalumu ambazo ukizitumia, zinadhuru wakati ukiwa na ugonjwa fulani kwa mfano mtu mwenye ugonjwa wa ini, hatibiwi na dawa za kuua vijidudu au dawa zozote kali, kwa sababu ini halifanyi kazi hivyo, dawa hizo zinaweza kudhuru mwili.
 Watu ambao wamepungukiwa maji ya mwili au wana ugonjwa wa figo, ni lazima wawe waangalifu wa dawa wanazotumia.

Usitoe zaidi ya kipimo kimoja cha dawa ambayo inaweza kudhuru mwili mpaka uwe na uhakika kama mgonjwa anakwenda haja ndogo kama kawaida.


  • Kwa mfano, mtoto mwenye homa na upungufu wa maji mwilini, usimpe zaidi ya kipimo kimoja cha aspirini mpaka ameanza kukojoa. Usimpe mtu sulfonamide ambaye ana upungufu wa maji mwilini. Asanteni mwisho.

0 comments:

Post a Comment