Sunday 20 April 2014

UGONJWA WA BAWASIRI (HEMORRHOIDS)




Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.
 

AINA ZA BAWASIRI
  1. NJE
    Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.
  2. NDANI
    Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.

    Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.
Je bawasiri husababishwa na nini?


BAWASIRI HUSABABISHWA NA NINI?
Bawasiri husababishwa na;

  • Tatizo sugu la kuharisha
  • Kupata kinyesi kigumu
  • Ujauzito
  • Uzito kupita kiasi (obesity)
  • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
  • Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
  • Umri mkubwa
DALILI ZA BAWASIRI
  • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
  • Maumivu au usumbufu
  • Kinyesi kuvuja
  • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa

MATATIZO YANAYOWEZA KUTOKEA KUTOKANA NA BAWASIRI

  • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
  • Strangulated hemorrhoids

VIPIMO NA UCHUNGUZI

  • Digital rectal examination
  • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
  • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)

MATIBABU

Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri

  • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
  • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
  • Coagulation (infrared, laser and bipolar)
  • Upasuaji;
         Hemorrhoidectomy 
         Stapled hemorrhoidopexy

 

NJIA ZA KUZUIA BAWASIRI
  • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
  • Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)
  • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa 
TIBA YA MARADHI YA BAWASIRI
TIBA: Jambo la kwanza kabla ya tiba mgonjwa aweze kutibiwa maradhi ya kutopata choo vizuri ikiwa anayo kwa sababu huzidisha maradhi haya. Pia epuka kula Nyama hasa ya ngombe, Pilipili na vitu vikali. Halkadhalika usinywe maziwa kwa wingi.
Kanuni ya kwanza: Kunywa juisi ya tikiti maji asubuhi kabla ya chakula na usiku kabla ya kulala.Dawa hii hutibu na kuondoa maumivu ya bawasiri.

Kanuni ya pili: Chukua asali nusu lita , unga wa kamun aswad vijiko vitatu vikubwa,unga wa Habat soda vijiko vitatu vikubwa na unga wa kamun abyadh vijiko viwili vikubwa. Vitu vyote hivi vichanganye pamoja kwa kuvikoroga kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vikubwa vya mchanganyiko huu kisha ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto. Yakishapoa uchuje halafu unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Ikiwa ni bawasiri ya kutoka nje au yenye vidonda, paka mafuta ya nyonyo au mafuta ya lozi.

0 comments:

Post a Comment