Tuesday 29 April 2014

FAIDA MBALIMBALI ZA MTI WA MNYONYO




Mti  wa  mnyonyo  una  faida  nyingi  sana  kwa  afya  ya  mwanadamu.  Karibu  kila  kitu  kinachopatikana   kwenye  mmea  wa  mnyonyo  kina  faida   za  kiafya  kwa  mwanadamu.
Majani ya nyonyo ni tiba ya kifua kikuu  na  mizizi yake ni dawa ya mafindofindo, kuungua, macho yanjano, uvimbe, koo, kisonono  na  kaswende.

Kikonyo  chake  ni  dawa  ya  kwikwi.

JINSI  YA  KUTUMIA  MMEA  WA  MNYONYO  KUJITIBU  MAGONJWA  &  MATATIZO   MBALIMBALI  YA  KIAFYA.

i.             Kwikwi :
Jaza maji kwenye kikonyo, mpe mgonjwa anywe kila baada ya dakika 3 mpaka kwikwi iishe.
ii.           Kuungua  :
Meza  punje  za  mti  wa  nyonyo kwa  maji  kiasi  cha  glasi  moja  kwa siku  kwa  muda  wa  siku  tano.
iii.         Kutibu  miguu  inayo  uma :
Tumia majani kwa kufungia miguu inayouma.
iv.         Maumivu  Ya  Mgongo :
v.           Majani yake ukiyapasha moto yafaa kukanda mgongo  wenye  maumivu.

vi.         Kutibu  Kaswende  na  Kisonono  :
Ponda  mizizi  ya    mti  wa  mnyonyo, kisha  chemsha  na  tumia  kunywa  glasi moja  mara  mbili  kwa  siku  kwa  muda  wa  siku  saba.
vii.       Kuondoa  Kondo  La  Nyuma :
Mizizi  ya  mti  wa  mnyonyo  ikitafunwa  na  mama  mjamzito  yafaa  kwa  kutoa  mfuko  wa  uzazi  ( kondo  la  nyuma  )  kwa  urahisi  na  usalama  zaidi.


Myonyo/Mbarika (Castor)


Mnyonyo (KiSwahili) Erand (KiHindi) Kastorka (KiRusi) ni mmea wa jamii ya Mbono Kaburi, kwa jina la kitaalamu Japtropha - nitauzungumzia siku zijazo.

Baadhi ya faida za mnyonyo na mazao yake.
Mbali na kuweza kutumia mnyonyo kama uzio hai, njia hii inaweza kutumika kwa wale wasio na eneo kubwa la shamba ndiposa wakapata faida zake kama ifuatavyo:

Majani
ya mnyonyo yanaweza kutumika kama tiba ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB), kukanda (massage) ili kuondoa maumivu na majani haya yakifungwa kwenye mguu unaouma huleta nafuu hasa kwa maumiviu yanayokuja baada ya kuteguka, pia hutumika kutibu uvimbe kwa wanyama.

Mizizi ya mnyonyo huweza kutumiwa kama dawa ya mafundo fundo, uvimbe, kuungua, macho ya manjano, kuumwa koo na magonjwa ya kuambukiza ya kisonono na kaswende. Ukijaza maji baridi kwenye kikonyo cha mnyonyo na kumpa mtu mwenye kwikwi kila baada ya dakika mbili au tatu hivi, mara nyingi huondoa usumbufu unaoletwa na kwikwi.

Mbegu/Punje/Tunda/Njugu

za mnyonyo zikimezwa na maji bilauri moja kila siku kwa muda wa siku tano huweza kutibu maumivu yaliyosababishwa na kuungua. Vile vile, mbegu hizi huweza kusagwa na kisha kuenguliwa mafuta kwa ajili ya kulainisha mashine na mitambo viwandani.
 

Mbegu za mnyonyo kabla ya kukomaa
Mafuta yatokanayo na mbegu za nyonyo mfano Ricinoleic Acid, Oleic Acid, Linoleic Acid nk hutumika kutibu ugonjwa wa wa jongo (rheumatism) unaowakumba watu wengi wanaoishi maeneo ya miinuko na baridi, pia hutibu ugonjwa wa mifupa ujulikanao kwa jina la kitaalamu kama arthritis na gauti.Mafuta ya mnyonyo pia yanaweza kutumika kama njia ya

kupanga uzazi
 

kwani yana kiasi fulani cha sumu ya protini ijulikanayo kitaalamu kama ricin ambayo ikitumiwa kwa kiasi kidogo huharibu utungo, huweza pia kutumiwa kama mafuta ya kupaka ama losheni katika sehemu za siri ili kuua mbegu za uzazi za kiume wakati wa tendo la kujamiiana. zazi wa mpango.

Tahadhari:

  • Mnyonyo ni mti wenye sumu inayoweza kuua binadamu au wanyama endapo itatumika kuzidi kipimo.
  • Mazao yoyote yatokanayo na mnyonyo huhatarisha au/na kuharibu mimba na hata kuweza kusababisha kifo cha mjamzito, hivyo, matumizi yake lazima yawe ya uangalifu mkubwa.
  • Mafuta ya Ricinoleic acid yanayopatikana kutokana na mnyonyo vile vile yanaweza kutumika kurekebisha hedhi (mzunguko wa damu ya mwezi kwa wanawake) ikiwa mzunguko umechelewa ama kusimama katika umri usiotarajiwa. Huweza pia kupunguza maumivu makali yanayotokea wakati wa hedhi.
  • Mafuta ya mnyonyo yanayojulikana kitaalamu kama Undecylenic Acid huweza kutumika kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi na vidonda vinavyosababishwa na bakteria ama ukungu (fungus). 
Mbegu za mnyonyo baada ya kukomaa

   


Akina mama wanao nyonyesha 
pia wanaweza kutumia mafuta baridi ya mnyonyo (kiasi kidogo ili kuepuka madhara ya mafuta hayo kwa mtoto, kumbuka hapo awali nimeandika kuwa mafuta haya yakitumiwa kwa kiwango kikubwa ni sumu) kuongeza wingi na mtiririko rahisi wa maziwa. 

Nywele
nzuri, safi, nadhifu na zisizokatika pia ngozi imara inapatikana kutokana na matumizi ya mafuta ya mnyonyo.Mafuta ya mnyonyo pia ni dawa nzuri ya kufungua tumbo la uyabisi (kuvimbiwa).

Faida nyinginezo

Mnyonyo unaweza pia kuwafaa watu wanaoishi na VVU (Virusi Vya UKIMWI) kwani mafuta yake ni sumu ya kuua vimelea vya magonjwa kama vile bakteria na ukungu (fungus).

Njia:

  1. Kupakaza: Chukua kipande cha nguo ama kitambaa, kisha kiloweke kwenye mafuta ya mnyonyo ndipo ufunge katika kiwiko ama eneo lenye maumivu ama kidonda. Vinginevyo, chukua kiasi cha mafuta na kupaka eneo linalohusika mfano, penye kidonda, kuugua ama pakaza kichwani au juu ya tumbo wakati wa maumivu ya hedhi nk. Unaweza kuacha kwa muda wa saa moja kabla ya kunawa ili uipe ngozi muda wa kunyonya kiasi cha mafuta. Unaweza kujifunga kitambaa hicho tumboni ama mgongoni kama kibwebwe na kuendelea na shughuli za kawaida.
  2. Kunywa: Chemsha mbegu chache za mnyonyo pamoja na maji na maziwa kisha unywe kiasi kidogo kadiri ya nusu hadi bilauri moja ya ujazo wa mili lita mia mbili na arobaini.
  3. Kusafisha utumbo: Kunywa mafuta ya mnyonyo vijiko viwili vikubwa vya chakula asubuhi, kisha pumzika kwa saa mbili ndipo unywe maji glasi mbili na endelea kunywa maji glasi moja kila baada ya saa moja.

6 comments:

  1. Dr kanyas mtaalamu wa tiba asili anatibu magonjwa mbalimbali pia anazo dawa kwa ajili ya kuongeza uume na kurefusha uume...anatibuu ugumba.hedhi isiyo na mpangilio..mtafute kupitia 0764839091

    ReplyDelete
  2. Dr kanyas mtaalamu wa tiba asili anazo dawa mbqlimbali kwa kutumia mitishamba na dawa za kisuna anazo dawa za kurefussha uume na kunenepesha uume....mtafute kupitia 0764839091

    ReplyDelete
  3. Mi nimekuwa msomaji sana wa makala zako hasa jamii forum. Vipi kuhusu kutibu infertility kwa wanaume. Mfano kupaka sehemu ya dhakar na pia nigejua kuhusu ngiri hasa ya kwenye kondo au anal hernia. Asante

    ReplyDelete
  4. Mimi nimenunua mafuta ya nyonyo natumia kupaka kama lotion napia napaka kichwani,je kuna madhara yoyote nitakayoyapata?

    ReplyDelete
  5. Mti uyo unasaidiya mtu kupata uzazi

    ReplyDelete